Friday, October 25, 2013

IJUMAA YA LEO NA KAZI YA MIKONO YA KAPULYA...KUOKA MIKATE!!

Nimechoka kununua mikata, nikaamua kuoka mwenyewe leo. Halafu ni mitamu zaidi kwa kweli. Ni rahisi sana. Maji lita moja, unga wa ngano lita moja na nusu, chumvi kijiko cha mezani cha chakula, Sukari vijiko 2 vya mezani, mafuta ya kula kikombe kimoja kidogo cha chai(1dl) na hamira pkt moja (50g) au kama ya unga ni vijiko 2 vya chai. Unachanganya vyote na moja kwa moja unakanda unga mpaka unaona umekuwa laini. Unafunika na kitambaaa kizuri kwa dakika 30 ili uumuke. Baadaye unatengeneza utakavyo na kuumua tena dakika 30. Baada ya hapo unapaka maji au maziwa na kuingiza kwenye oven kwa dakika 8-10 na hapo mikate tayari. NAWATAKIENI IJUMAA PIA MWANZO MZURI WA MWISHO WA JUMA HILI. IJUMAA NJEMA!!!

13 comments:

Anonymous said...

Ama kweli da Yasinta ni mahiri sana katika kuunga msosi. sasa si utumwagie kidogo mapishi na sisi tuweze kuunga kidogo. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu! unaweza kufafanua hapa tafadhali!...Ahsante kwa kutochoka kupita hapa Maisha na Mafanikio.

Anonymous said...

Da Yasinta, mi nachosema wewe ni mkali sana kwa mapishi kutokana na post mbalimbali za misosi hapa jamvini, kwa mfano ukitaka kuunga ugali na mchuzi wa dagaa, utaanza kuchemsha maji ya ugali na kumimina unga wa ugali polepole ukiwa unausonga mpaka kuiva. kupita hapa Maisha na Mafanikio najihisi nipo nyumbani. By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ! nimekuelewa..na nimeweka maelezo tayari..Samahani kusahau..na ahsante kunikumbusha...

Anonymous said...

Asante da Yasinta1 Somo limeeleweka. Ijumaa njema kwa wote. By Salumu.

Unknown said...

hiyo mikate mi naitaka na chai ya rangi. Tafadhali usimalize yote... kazi nzuri dada.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mrope...je chai yako unataka iweje tangawizi...sukari au?...sitamaliza nakufichia.....ahsante kaka.

Unknown said...

ya rangi huwa napenda na tangawizi mbichi. Ya maziwa ikiwa na chai masala hapo mwishoooooo!!!! Ahsante kwa kunikaribisha!

Interestedtips said...

asante kwa somo dada. nami nitapika kwakweli.

Unknown said...

Mmmh, Da yasinta hongera sana mn hku mpk mate yananiteremka.

Unknown said...

Mmmh, Da yasinta hongera sana mn hku mpk mate yananiteremka.

Anonymous said...

Usisahau kunipostia yangu Dada.

ray njau said...

Unastahili cheti cha mapishi bora!!