Tuesday, January 29, 2013

MILO AMBAYO NINGEPENDA SIKU YA LEO NILE NI HII HAPA...!!!

 
Chai ya rangi na ndizi mzuzu za kuchemsha
Mlo kama huu kwangu ni mali sana kuliko chai ya maziwa kwa mikate. Vyakula vyetu kama viazi, mihogo, magimbi na ndizi hakika jamani tuendelee kula kwanza unakula unashiba na halafu vina faida. Karibuni....na mchana...mmmmmhhh

 

Mchana, Nimekaa hapa naota mlo huu ugali, samaki, chuzi, mbogamboga na kachumbali kidogo bila kusahau pilipili... ila duh naona niishie kula kwa macho tu....au ...na jioni sijui itakuwaje ..hii ndiyo mara nyingi akina mama huwa tunawaza ili familia ipate chakula..tuna kazi kweli kweli......

5 comments:

ray njau said...

Hakika maandalizi mema sana kwa ajili ya familia nami naungana na familia yako katika mlo huu wenye ladha zote.Ukiwa ni mwanamke mwema jisikieni kuwa ni fahari kwako kuihudumia familia yako katika nyanja mbalimbali na kamwe utendaji huo usitajwe kuwa ni mzigo kwako wala laana.
--------------------------
Ndiyo sababu tunasema:-
"Ni nani kama mama"?
"Mama ni nguzo ya dhahabu isiyoisha thamani."
---------------------------
Wanawake endeleeni kutafakari maneno haya kutoka katika biblia:-
---------------------------
"Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."_Mwanzo 1:18
------------------------------
Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.Mithali 31:12-15, 17, 20
---------------------------------

Yasinta Ngonyani said...

kaka Ray! karibu sana kujumuika nasi...na Ahsante sana kwa neno hilo kuhusu mke/mwanamke...pamoja daima.

ray njau said...

Asante sana!!

Yasinta Ngonyani said...

karibu sana...wahi kidogo usije ukakuta ndizi zimekwisha:-)

ray njau said...

Hakika nitafanya hivyo!