Friday, January 18, 2013

IJUMAA YA LEO NA MWANAMTINDO WETU NDANI YA KITENGE TUDUMISHE HILI VAZI!!!

Unapopata zawadi unapaswa kuchukuru ahsante Dada mkuu msaidizi..Mija na hii ni kazi ya mikono ya shemeji Manju...kuona kazi zake zaidi unaweza kuingia hapa
Mimi ndani ya kitenge ..huwa kila niendapo kunyumba nashona kitenge ..napenda sana vazi hili. Kitu kimoja huwa kinaniletea taabu pale nishindwapa kuchagua mshono/mtindo..huu nimechaguliwa na fundi kama kuna mtu anaweza kunipa mbinu naomba...
Hapa ni zawadi kutoka kwa dada Ester Ulaya nilipata ile siku tuliyokutana,,Ahsante sana Dada Ester na Shemeji ..nimeipenda sana zawadi hii..si unajua mwanamke kanga/kitenge..kudumisha utamaduni wetu ni msingi mzuri..mpiga pcha ni dada Camilla. NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA NJEMA NA PIA MWANZO WA MWISHO WA JUMA UWE WENYE FURAHA..PAMOJA DAIMA...

18 comments:

Ester Ulaya said...

kwakweli Manju yupo juu, umependeza sana dada na vitenge hivyo........pia asante kushukuru kwa zawadi hiyo, twakutakia ijumaa njema pia

Yasinta Ngonyani said...

Ester! ahsante sana. Pia nakubaliana nawe Manju yupo juu na mungu amzidishie ujuzi.

Emmanuel Mhagama said...

Dada umependeza kuliko maelezo. Nitamshonea wifi yako kama hizo.

sam said...

Bado kilemba,nguo ninzuri sana.zimekukaa vizuri.kaka s.

Rachel siwa Isaac said...

Umependeza sana KADALA.....Dada Mkuu Mija pia ni mtaalamu saana wa UBUNIFU WA MAVAZI NA UREMBO...Ndiyo anayetuvalisha na kutupamba huku tulipo.......

kwamishono na Mitindo mingine unaweza kuipata MITINDO AFRICA.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta una maji ya nguo...!!!

Umependeza sana, Asante kushukuru...

Halafu mpiga picha mkuu wa blogu hii anaiweza sana kazi yake, mpe hongera sana..

@Rachel mpambaji mkuu..sina la kusema, Mungu azidi kukubariki na akuongezee kila lililo la heri..

Mbarikiwe sana..

ray njau said...

Ili kuanzisha mtindo fulani, wanaobuni mitindo hutumia mambo matano ya msingi: rangi, maumbo, mikunjo, mifumo, na mapambo ya kitambaa. Kadiri ambavyo miaka imepita, kumekuwa na vitambaa vya rangi, maumbo, mikunjo, mifumo, na mapambo chungu nzima, ambavyo wabuni na washonaji wanaweza kutumia. Kwa mfano, katika Misri ya kale, kitani kinachoonyesha mwili ambacho kilitengenezwa nchini humo ndicho kilichopendwa sana, nacho kilifaa wakati wa joto. Lakini kwa kuwa kitani hakingeweza kutiwa rangi kwa urahisi, kwa kawaida kilikuwa cha rangi moja tu, nyeupe. Hata hivyo, wabuni Wamisri walishona vitambaa na kuvitia mikunjo na maumbo yenye kupendeza. Basi, mojawapo ya mitindo yenye kudumu zaidi ulimwenguni ikabuniwa.

Kufikia karne ya kwanza W.K., vitambaa na rangi mpya zikapatikana. Waroma matajiri walinunua hariri kutoka China au India, ingawa gharama ya kuzisafirisha ilifanya hariri zilizofumwa ziwe ghali kama dhahabu. Sufu iliyotiwa rangi kutoka Tiro ilipendwa sana pia. Kilo moja ya sufu hiyo iligharimu dinari 2,000—mshahara wa miaka sita wa mfanyakazi wa kawaida. Kuwapo kwa rangi hizo mpya pamoja na vitambaa hivyo vipya, kuliwawezesha wanawake Waroma wenye mali kuvaa stola, yaani vazi refu la nje la pamba la bluu kutoka India au hariri ya manjano kutoka China.

Ingawa mitindo mipya ilizuka pindi kwa pindi, katika enzi zilizopita mavazi ya bei ghali yangeweza kudumu kwa muda mrefu. Mitindo hiyo ilibadilika polepole na mara nyingi iliathiri wastaarabu tu. Hata hivyo, mvuvumko wa kiviwanda ulipoanza, mitindo ilianza kuwaathiri hata zaidi watu wa kawaida.

Katika karne ya 19, viwanda vizima-vizima vilianzishwa ili kutengeneza nguo kwa ajili ya matajiri na maskini. Mashine za kufuma pamba na sufu zikawa nyingi, nazo bei za vitambaa zikashuka. Kwa sababu ya mashine za kushona, mavazi yangeweza kutengenezwa kwa bei rahisi zaidi, na rangi mpya za sanisia zikawezesha kuwapo kwa vitambaa vya rangi nyingi.

Mabadiliko ya kijamii na ya kitekinolojia yalitimiza fungu kubwa hata zaidi katika kutengeneza mavazi kwa ajili ya watu wa kawaida. Katika Ulaya Magharibi na Amerika Kaskazini, watu walikuwa na pesa nyingi zaidi za kutumia. Katika miaka ya 1850, magazeti ya wanawake yakatokea, na punde baadaye maduka makubwa yakaanza kuuza nguo zilizoshonwa tayari za saizi mbalimbali. Pia katika karne ya 19, Charles Frederick Worth alianzisha maonyesho ya mitindo akitumia watu mbalimbali ili kuchochea hamu ya waliotarajiwa kununua mavazi hayo.

Katika karne ya 20, nyuzi mpya za sanisia, kama vile rayoni, nailoni, na poliesta, ziliwawezesha watengenezaji kupata vitambaa vya aina nyingi zaidi. Violezo vilivyohifadhiwa katika kompyuta vilifanya iwe rahisi kubuni mitindo mipya, na kwa sababu ya muungano wa ulimwengu, mitindo mipya ingeweza kutokea karibu wakati uleule katika majiji ya Tokyo, New York, Paris, na São Paulo. Wakati huohuo, wabuni na watengenezaji wamepata njia mpya za kuuza bidhaa zao.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama wala hamna taabu ukitaka nitakuongoza hadi kwa fundi ...kunyumba kuSongeya:-)..ahsante ..

Kachiki..asanti ..nimepita huko MITINDO Afrika..KAZI NZURI ALO...

Dada mkuu msaidizi hapa sijui kama nipo nawe kuwa nina maji ya nguo..fafanua kiduchu..na salamu zishafika kwa mpiga picha ..Ahsante kwa yote:-)

Kaka Ray ahsante kwa ufafanuzi...mwanana.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam..Duh..umenikumbusha nimesahau kilemba kweli na pia mtandio:-(..Ahsante

Anonymous said...

Dada Yasinta umependeza sana tena sana. Imarisha utamaduni wa Mtanzania, inapendeza sana. Jamani hiyo ya kwanza skirt na blouse umenunua wapi? au ulishonesha? sijakupata vizuri kwani nahitaji kujua kwa Mpanju TZ anapatikana wapi?

Mija Shija Sayi said...

@Anonymous hapo juu, Manju Msita anapatikana Dar Chang'ombe, Jengo la MIKONO... zamani HANDICO..

Mtafute kwa namba hizi atakupendezesha bila wasiwasi..
255 772 411 441
+255 784 411 441
+255 655 411 441
+255 766 411 441

@ Yasinta..Maji ya Nguo maana yake, kupendeza katika kila nguo unayovaa hata kama ni ya kujitupia tu..

Mbarikiwe wote..!!!

EDNA said...

Umependeza sana, nitakuja kuazima hiyo ya kwanza.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mashaalllah!

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapo juu ahsante na naona umeshapata jibu wapi hiyo nguo ya kwanza nimeipata...

Dada mkuu msaidizi ..nimekupata ahsante

Dada Edna wala hakuna taabu we njoo tu utapata:-)

Kaka Wambura ..Ahsante!!

batamwa said...

ya fundi kakuchagulia mshono mzuri sana hasa hilo vazi la pili umependeza na watoto wa mujini wanasema umetoka chichaa........kweli nguo za vitenge zinakutoa sana ubarikiwe

emu-three said...

Heri mimi sijasema, ila sitasita kusema kuwa mpendwa kwa vazi hilo, umetokelezea na kuwa `kasichana'

Penina Simon said...

Hi Yasinta, Umependezeje? hongera sana,
Hivi vitenge washona ukija huku au huko kuna fundi anakushonea? nimependa fundi wako anakushonea nguo unayoweza kwenda nayo popote

Markus Mpangala said...

afrika yangu nakupenda sana. na hakika unaipenda afrika yako