Sunday, January 27, 2013

UJUMBE WA JUMAPILI HII YA NNE YA MWAKA 2013 NI KAMA IFUATAVYO!!

Unapotafakari mema ya Mungu ya leo:-

WASAMEHE WALIOKUKOSEA,
WAKUMBUKE WALIOKUSAHAU na UILINDE AMANI YA MOYO ISIPOTEE.
Kwani utakuwa na furaha daima!!!
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!

4 comments:

Anonymous said...

Asante dada Yasinta. Furaha na upendo kwa binadamu wote!
By Salumu.

ray njau said...

Asante sana kwa madokezo mazuri hapa kibarazani wikiendi hii.Nasema asante sana kutoka moyoni kutokana na sehemu ya programu yetu mafundisho ya biblia ulimwenguni pote katika Jumapili ya Januari 27,2013[Mashahidi wa Yehova]ilizingatia kusameheana:-
-----------------------------------
JE, UNAPASWA KUONA KWAMBA UMEKOSEWA KIMAKUSUDI?
===========================
Kuna hali nyingi maishani zinazomfanya mtu akasirike. Tuseme kwamba unaendesha gari, na karibu ligongwe na gari lingine. Utatendaje? Umesoma kuhusu visa vingi vya madereva wenye hasira waliowashambulia madereva wengine. Hata hivyo, ukiwa Mkristo, bila shaka hungependa kufanya jambo kama hilo.
Itakuwa bora zaidi kutua kidogo ili kuchanganua mambo. Labda wewe pia una makosa kwa sababu ulikengeushwa na jambo fulani. Au huenda gari la yule dereva mwingine lilikuwa na tatizo. Somo ni kwamba tunaweza kupunguza hasira, hisia za kukata tamaa, na hisia nyingine zisizofaa tukitumia uelewaji, tukiona mambo kwa njia tofauti, na kuwa tayari kusamehe. Andiko la Mhubiri 7:9linasema hivi: “Usiwe na haraka kuudhika katika roho yako, kwa maana kuudhika hukaa katika kifua cha wajinga.” Usione kwamba umekosewa kimakusudi. Mara nyingi, huenda tukafikiri kwamba mtu fulani ametukosea kimakusudi lakini huenda sivyo ilivyo; labda ni kwa sababu tu ya kutokamilika au kutoelewana. Jitahidi kuwa na maoni yenye usawaziko kuelekea matendo unayoona kuwa si ya fadhili, na uwe tayari kusamehe kwa upendo. Utakuwa mwenye furaha zaidi ukisamehe.—Soma 1 Petro 4:8
=================================

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu Ahsante ..na karibu sana tena na tena

Kaka Ray ! Nawe ahsante kwa mwongozo huu..ni kweli kusamehe ni jambo nzuri ila si wengi tunaweza kufanya hivyo...

ray njau said...

Asante sana dada Yasinta;
=========================
"Jitahidi kuwa na maoni yenye usawaziko kuelekea matendo unayoona kuwa si ya fadhili, na uwe tayari kusamehe kwa upendo. Utakuwa mwenye furaha zaidi ukisamehe".—Soma 1 Petro 4:8