Tuesday, January 22, 2013

SIKU YA MWAKA MPYA 1/1/2013 ILIVYOKUWA HAPA KWETU SONGEA/RUHUWIKO NA MZEE UHAULA NDANI YA MAPISHI!!!

Hapa pilau likiandaliwa na mpishi maalumu, kwa jina anaitwa mzee Edward Uhaula ni mkazi wa Matetereka..tulikuwa tukiishi nashi enzi hizo. Kwa hiyo siku hii ya mwaka mpya 2013 alikuja kutusalimia na hakukosa kukumbushia enzi yaaani kupika. Maana si unajua ukiwa na familia kubwa..halafu tena ni sikukuu ya mwaka mpya inapendeza kukutana pamoja kula na kucheza/kuongea..kubadilishana mawazo. ilikuwa safi sana kwa kweli
Hapa ni nyama ya ngómbe ikiandaliwa ..muda si mrefu itatengenezwa kwa viungo na baadaye kuliwa....

6 comments:

Markus Mpangala said...

Makulaji hayo mweeeee mate tu hapa

Anonymous said...

Kwa kweli mlijichana sana, ilikuwa safi sana kwenu na mpaka mpishi maalumu! Je hakukuwa na ugali kwa dagaa/ samaki na mboga mboga?

Yasinta Ngonyani said...

heheheeee..mlongo wangu punguza mate karibu bado vipi:-)

Usiye na jina!! kukosekane ugaöi kwa dagaa/samaki tena na halafu mbogamboga vyote vilikuwepo hata magharage:-)

Ester Ulaya said...

mlifaidi mnooooooo....hheheheh mlimbania rafiki yangu maharage hapo, mbona sioni kama yametengwa....mate tu hapa

Yasinta Ngonyani said...

Dada Ester... kweli tulifaidi ..rafikiyo alipata maharage yake ingawa hajaonekana hapo..usitokwe na mate sana:-)

ray njau said...

Ama kweli mtu kwao ni kwao tu!!