Saturday, January 5, 2013

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA ....MIAKA INAKWENDA JAMANI

Leo ni tarehe/siku ambayo familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa kumpati binti huyo ambaye alizaliwa siku hii ya leo. Na leo ameongoza mwaka tena na kuzidi kuzeeka. Lakini hata havyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...KAPULYA

14 comments:

ray njau said...

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika muungano na Bwana, kwa maana hilo ni jambo la uadilifu: “Mheshimu baba yako na mama yako”; ambayo ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi: “Ili mambo yakuendee vema nawe ukae muda mrefu duniani.” Nanyi, akina baba, msiwe mkiwakasirisha watoto wenu,bali endeleeni kuwalea+ katika nidhamu na mwongozo wa akilini wa Yehova_Waefeso 6:1-4

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana "Kadala" MUNGU azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo leo.....uwe na wakati mwema!!

Mija Shija Sayi said...

Hongera dada Yasinta, Mungu akuongezee miaka tele na yenye furaha..

Amen..

Anonymous said...

Happy birthday to you Dada Yasinta.

Mungu azidi kukupa afya njema na hekima katika kumjua yeye.

Anonymous said...

Baada ya kuangalia hiyo video yako ya leo, nimeipenda sana ni nzuri mno. Ombi, je unaweza kutuwekea ya matukio ya songea na siku ya leo ilivyokuwa kwako? Natumaini nasi tulio mbali na Tz tutakuwa tumefika kwa njia ya kukuona katika video. Huu nao ni ubunifu wa aina yake na huo wimbo umenogesha sana, kwani nimerudia kuangalia mara tatu. Haya uwe na wakati mzuri na familia yako.

John Mwaipopo said...

hongera kwa kuchana kalenda. wewe na familia yako muwe na wakati mujarabu mkirafakuri yaliyopita na yajayo.

sam mbogo said...

Hongera,da Yasinta . kaka s.

Baraka Chibiriti said...

HONGERA SANA KWA SIKU YAKO YA PEKEE....DADA YASINTA.

batamwa said...

hongera kwa kuzidi kuuendea uzee na hapo ndipo busara zinazidi kuongezeka si uzeetu ubarikiwe sana

Rafikio wa hiari said...

hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa rafiki yangu wa hiari Mungu akutimizie yale yote uliyoyapanga mwaka huu, akujalie afya njema, mafanikio na baraka tele!
Happy birthday Yasinta!

Markus Mpangala said...

Ubarikiwe kwa mengi mema. Mungu akulinde zaidi na zaidi pamoja na familia

Simba Deo said...

Hongera sana Kapulya ... ingawa salamu yangu imechelewa lakini nakutakia afya njema, mafanikio na maisha marefu ili mchango wako kwa jamii ya wanadamu upate kuendelea.

Asante sana.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana wote kwa kuwa nami katika siku hii maalumu kwangu maana ilikuwa ndiyo siku ya kwanza kuingia katika dunia hii. Na leo nipo nanyi na nimetimiza miaka ...au niseme makumi 4..naelekea kweli uzeeni ila napenda kwelikweli umri huu:-)

Justine Magotti said...

tunakutakia happy birth njema.