Friday, October 12, 2012

IJUMAA YA LEO NGOJA TUWATEMBELEE NDUGU ZETU WACHAGGA NA NGOMA YAO HII YA JADI/ASILI!!!


Ni ngoma ya kabila la Wachagga kutoka katika Wilaya ya Arusha wakicheza ngoma ya Jadi/asili.....IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWA WOTE!!!!!!

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nimeipenda ngoma hii ingawa sielewi wanasema nini kwangu hiyo midundo na jinsi ya kucheza ni raha mno...uasili ni mtamu.Wachagga oooyyeeee!!

ray njau said...

Wachagga ndiyo sisi!

ray njau said...

UNAPOTAJA JINA KILIMANJARO KWA HAKIKA UNATAJA TANZANIA KUTOKANA NA UMAARUFU WA MLIMA KILIMANJARO AMBAO NI MAARUFU KULIKO YOTE AFRIKA.NGOMA KUBWA YA ASILI YA WACHAGGA NI IRINGI.IRINGI HUCHEZWA KATIKA MDUARA HUKU WATU WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO IKIWA NI ALAMA YA UPENDO NA MSHIKAMANO WA KIFAMILIA.UPO UTANI KUWA ZAMANI NGOMA HIYO ILICHEZWA BILA KUSHIKAMANA MIKONO LAKINI BAADAE WATU WALIJIKUTA MIFUKO YAO MITUPU.WAZEE WA KIMILA WAKAAMUA KUONDOA UTATA KWA KUWEKA AMRI YA KUSHIKANA MIKONO WA KUCHEZA NGOMA HIYO.WACHAGGA WANAISHI KWENYE WILAYA NNE ZA MKOA WA KILIMANJARO AMBAZO NI SIHA;HAI;MOSHI NA ROMBO KWA MPANGILIO UFUATAO:

-----------------------------------

1.WASIHA

2.WAMACHAME [ WILAYA YA SIHA NA HAI]

3.WAMASAMA

-----------------------------------

4.WAKINDI

5.WAKIBOSHO

6.WAURU

7.WAOLDMOSHI

8.WAMBOKOMU [ WILAYA YA MOSHI ]

9.WAKIRUA

10.WAKILEMA

11.WAMARANGU

12.WAMAMBA

13.WAMWIKA

-----------------------------------

14.WAKENI

15.WAMKUU

16.WAMASHATI [ WILAYA YA ROMBO ]

17.WASSERI

18.WANGASA

Naitwa Kombe said...

Nimeona hii juhudi ya kutafuta ngoma ya Wachagga inapaswa kupongezwa sana.
Lakoni sisi Wachagga tunatokea Kilimanjaro Walaya za Rombo,Moshi Vijijini,Siha, Hai na Moshi Mjini kwa kiasi.Watani zetu ni Wapare wanapatikana kwa wingi Wilaya ya Same na Mwanga.Ni kuweka historia/kumbukumbu vizuri.

Unknown said...

Smhn ngoma ya wachaga inaitwaje

Unknown said...

Ngoma ya Wachaga"Iringi"Asante sana kiongozi.

Unknown said...

Safi kabisa