Wednesday, June 20, 2012

Chakula cha KIZUNGU ndio chakula gani hicho?-Chakula cha KIAFRIKA ndio chakula gani HICHO?


Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO na leo katika pitapita zangu nimekutana na hii  na nimeona si vibaya tukirudia. Na kama nisemavyo kurudia kitu/somo ndio kujifunza zaidi. Na nilikutembelea na kukutana na hii ni kwa Mtakatifu. KARIBUNI SANA...
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nimestukia kuna katabia ka WAAFRIKA kusifia MAJINA ya vyakula vya KIAFRIKA na kwa WAZUNGU visemekanavyo ni vya KIZUNGU,...
... bila kusahau WAARABU, Wahindi, Wachina ...nk....
....na hii ni bila kukumbuka kuwa labda CHAKULA sio MAJINA wala UTAMU wa CHAKULA,...
.... kama mahitaji ya MWILI ndio yalengwayo.
Swali:
  • Hivi tunakumbuka ni nini MWILI wa BINADAMU yeyote unahitaji -kitu ambacho chaweza kuwa ni zaidi ya kuhusianisha WATU wa ENEO fulani na VYAKULA vyao hata kama sio KIMAJINA hasa ukizingatia labda ni virutubisho tu fulani fulani ndivyo muhimu kwenye hivyo vyakula ndio MUHIMU kuliko lililobobea kimtazamo ambalo ni MAJINA tu na staili za MAPISHI ya kiitwacho ni CHAKULA?
  • Si yasemekana CHURA wakukaanga na UGALI -labda uhitajicho mwilini mwako ni CHURA kwa kuwa ushakunywa uji wa MTAMA asubuhi na wala sio UGALI?
  • Ndio,...
.... labda mambo mengine ni ladha na MAZOEA tu,....
.... kwa kuwa MTU ahitajicho zaidi ni MATEMBELE au tu MATE kipenzi litakalomfanya asile sana asivyohitaji MWILINI!:-(

PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO !!!!

3 comments:

ray njau said...

Kwa kawaida mazoea hujenga tabia.

Yasinta Ngonyani said...

kaka Ray umesema kweli...ila sijui kama mimi naona kuna tofauti...

ray njau said...

@yasinta;
Kila mtu kaumba kwa namna yake na kwa pekee ya kwa mapendezi ya pekee yake kwa maisha ya pekee yake na wewe utandaelea maisha ya pekee yako kwa namna ya kipekee!