Tuesday, April 13, 2010

UJUMBE WA LEO:- NI VYEMA KUIJUA SIRI HII!

Huu ndio ukweli, ukitaka kupata furaha ya maisha

1.Sema kweli
2.Furahia maisha na furahisha wengine, Penda kwa dhati bila unafiki na bila masharti
3.Jiamini
4.Chukia kusema uongo
5.Tetea unachokipenda na kukiamini
6.Ukiwa dhaifu wa kukumbwa na mawazo potofu usichukie kumbuka mawazo pototfu yameumbiwa Binadamu
7Jitahidi kufikiri na kuwaza vyema ili uzidi kujiamini, kujipenda na na kuwapenda wengine. Yote yanawezekana.

Kumbuka usemi huu “ukivuliwa nguo chutama. Ukikosea tubu haraka.
Wastara huwa haumbuki……………

17 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Duh!

laiti kama wengi wetu tungeijua siri hii basi yanayoonekana mitaani sasa yasingetukia!

Aksante Da Yasinta kwa ujumbe huu.
Ubarikiwe kwa sana tu!

Anonymous said...

ujumbe madhubuti. Asante Yasinta kwa ujumbe huu. Hii ndio siri ya kufurahia maisha.

Anonymous said...

Nimefurahia ujumbe huu dada yangu mpendwa Yasinta,siku zote najifunza mengi nikiipitia blog yako.
Ranatus Kiluvia.

Christian Bwaya said...

Yasinta umegonga ikulu

Unknown said...

Swaadakta dada Yas, Nimekupata vizuri. Ukweli ni kwamba kama siri nyingi zingekuwa wazi basi mambo mengi yasingekuwa matatizo kwetu...

mumyhery said...

shukran kwa usia mwema

MARKUS MPANGALA said...

>>>>>>Mmmhh>>>>>>

ERNEST B. MAKULILO said...

Asante Da Yasinta,

Umetoa ujumbe mzuri sana. Nimeipenda hiyo kwamba ukivuliwa nguo chutama, nikakumbuka ile kichaa akikimbia na nguo zako, nini ufanye.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
San Diego, CA

Koero Mkundi said...

Nimeipenda hii.....

"ukivuliwa nguo chutama"

Nahisi hapa kuna dalili ya kubakwa....LOL

Anonymous said...

Dada yasinta unaposema ukivuliwa nguo chutuma, nadhani huu ni mtizamo wa mvuliwa kwani hujui dhamira ya mvuaji .mengineyo nauunga mkono ,

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eti ehe

PASSION4FASHION.TZ said...

Asante kwa ujumbe mzuri.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

@Koero: kama ni kubakwa ni kwa hiari, ama?...lol

STEVIE said...

NAMBA MOJA NI SALA MENGINE YANAFUATA

Anonymous said...

Stevie sala kwa nani? Mungu wa wazungu au Mungu wa kwetu?

STEVIE said...

SALA KWA UNAEMUABUDU KUTOKA NA IMANI YAKO,KAMA MBUYU AU MLIMA CHA MHM NINI MATOKEO YA MAOMBI YAKO KWA KILE UAMINICHO/ABUDU KUTOKANA NA IMANI YAKO.

Simon said...

umesema kweli dada..
hayo ni mambo ya msingi sana yanayoweza kumfanya mtu aishi vyema na afurahie maisha yake