Monday, April 5, 2010

NIMEZISHITUKIA OFA ZA WANAUME!!!!!!!

Tumezishitukia ofa zao

Kwa huku kwetu ni wanaume wachache sana wanaomsaidia mwanamke bila lengo la kumpata mwanamke huyo, na akimtaka, mwanamke anaweza kujisikia vibaya wakati mwingine kwa kudhani kwamba misaada hiyo itakoma haraka kwa sababu hakuna jambo lenye kuwashika, yaani tendo la ndoa, hivyo hulazimika kukubali kutoa tendo la ndoa ili misaada isikome.


Hata hivyo sio wanawake wengi wanaokubali kulipa fadhila kwa njia hiyo, lakini wanaume wengi hutumia misaada au ofa kama chambo cha kuwanasia wanawake.

Kwa wanawake kusaidiwa ni kusaidiwa tu huwa hakufungwi na kutakiwa kimapenzi, lakini kwa wanaume kusaidia huwa kunafungwa pamoja na mapenzi.

Je sababu ni nini?

Wanaume wamelelewa na kufanywa kuamini kwamba wanatakiwa kuonesha sifa fulani kwa wanawake kabla hawajawatongoza.

Kwa hiyo mwanaume kabla hajatongoza huanza kujisifu kwanza, ili mwanamke amuone kama mtu anayeweza, hivyo mwanaume anapotoa msaada kwa mwanamke kuna mawili kama sio matatu, ama anataka kusifiwa au anamtaka mwanamke huyo, au vyote.

Lakini pia wanaume wengi huamini kwamba kwa kutoa ofa, mwanamke atajua kwamba anamtaka, hivyo kwa wanaume hao ofa ndio kutongoza kwenyewe. Kwa hiyo mwanume kama huyu anapotoa msaada kwa mwanamke anatarajia kumpata kimapenzi mwanamke huyo.

Kwa mijini kwa mfano mwanamke anayepewa lifti ni yule mzuri kwa sura na umbo, ukweli nikwamba hakuna msaada hapo bali mwanaume anaanza kununua penzi ambalo hajalipata.
Mwanaume akimpa lifti mwanamke na kumtongoza, na mwanamke huyo akakataa, basi huo msaada unafutwa mara moja.

Kwenye baa, mwanaume anaweza kumtuma mhudumu ampe pombe mwanamke fulani. Hajui mwanamke huyo kaja hapo baa na nani na anafanya kitu gani. hiyo ofa sio ya urafiki bali ni ombi la mwili wa mwanamke huyo, kwani hiyo ni hatua ya awali ya kuwa karibu nae.

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hujitolea kuwasomesha, kuwapa au kuwatafutia ajira wanawake, lakini nyuma ya kujitolea huko, kuna agenda ya kuutaka mwili wa huyo mwanamke.
Mara nyingi mwanamke anakuwa hajui kwamba misaada mingi ya wanaume imefungwa pamoja na mapenzi. Ni wanaume wachache sana waliolelewa tofauti wasiofanya hivyo.

Ukweli ni kwamba wanawake wengi wamekuwa wahanga wa misaada .
Utakuta mwanaume anamsaidia mwanamke, mwanamke anapokea misaada hiyo akijua ni ya kibinadamu, kumbe akilini mwa mwanaume ni kwamba amewekeza. kwa hiyo anapokuja kumtongoza mwanamke huyo akakataa basi vita huanza.

Mwanaume anaweza kukumbushia misaada aliyotoa. na katika hali ya kushangaza mwanamke huyo hushikwa na butwaa. kwani hakujua kwamba alikuwa anapewa misaada ili atoe mwili wake.

Kuna wanaume wengi tu ambao wanaweza kumpa mwanamke soda kama taarifa kwamba amempenda, na mwanamke anaweza kupokea soda hiyo akijua kwamba ni ofa ya kawaida, lakini baadae hushangaa akija kutongozwa, na akikataa, anadaiwa soda aliyokunywa.

Nawasihi wanawake wenzangu wawe makini na ofa za wanaume kwani nyingi zimejaa utata mkubwa.



Habari ndiyo hiyo.......
Mada hii nimeichukua kutoka kwenye kibaraza cha VUKANI, cha dada Koero, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha.

8 comments:

watila said...

Dada Yasinta maneno msumali
lakini tujilize kuna pahala siku hizi kuna free lunch sijuwi tusikie kwa wengine wanasemaje

watila said...

au nipe nikupe two way traffic

Anonymous said...

sina hakika kama hii habari ni kweli sana. Binafsi naona ni kinyume chake, kwamba mwanamke akisaidiwa huwa anaona shukrani ya pekee ni mwili wake. Naongea kwa uzoefu wangu, wasichana wengi niliowasaidia waliishia kunitega na walipoona sisemi waliamua kusema wao wenyewe kwamba wangehitaji kutoa shukrani ya aina gani. Kama sio mimi kutopenda aina hiyo ya shukrani basi ningewatembelea wengi mno.

MARKUS MPANGALA said...

Hizi ni kati ya mada za utani kupindukia. Ni mzaha.

Nakumbuka niliona mada hii, lakini pengine kwa wakati ule sikuweza sana kuisoma vema. ASANTE kwa kuiweka hapa.
ukiniambia nini unafurahi katika maissha yangu niakwambia NASHUKURU KUZALIWA MWANAUME.
Ziko sababu, na sitaki kujua ningezaliwa mwanamke ningekuwaje.

Ndiyo maana nathubutu kusema WANAWAKE NI VICHAA HURIA/VICHAA HURU ********** samahani kwa mcharazo huo*****************.

Ziko sababu, kwanza ukipendapenda ofa utapew ofa kwakuwa wanajua unapenda ofa, na watakuchungulia uvunguni halafu si utalaumu au la! wakati mwingine huwa najiuliza, baadhi yetu tumesadia watu wametia timu London,Ontario na miji kadhaa ya ughaibuni lakini hatujawahi kuomba uvungu.

Ukiwaza hivi ni lazima uangalie mazingira ya wanaokuzunguka, endapo unapenda ofa utazipata sana si wanajua WEWE LIMAMA DEZODEZO a.k. MPENDA KULA KUKU WAKUNYONGWA? yaani wakuacha acha wakutimbange na wakufirigise ha ha ha ha ha ha ha ha!!!! Lol

Ni kweli hali hii inafanywa na wanaume tu? Jamani wanawake wna matatizo, mara zote wanaamini kuwa wakikirimiwa basi hawana cha kutoa wanadhani zawadi kubwa ya mrejesho wa ofa ni kuachia uvungu uchunguliwe n.k? haya ni mawazo gani?????????????

NIMEACHA TOPIKI YA MZAHA.

Numuunga anony aliyepita kwamba watu tukiamua kutafuna na kutimbanga itakuwa taabu.

Na tatizo ni kwamba wanawake wanadhani endapo mwanaume amekutendeajambo fulani lenye ishara ya JEMA eti anakutaka, haya mawazo ya ajabu kabisa, hivi utawataka wangapi? Kwani ukitendewa jema kisha unajiuliza imekuwajeeeee huyu kunikirimu hiviii. Utaona wanaanza siyo bureeee ananitaka.

Ujinga mtupu! nani akutake na sauti ya kauzu hiloooooo Lol......................... ha ha ha ha ha ha mnaloooooo leo limewaganda mnafikiria eti mkikirimiwa lazima mtoe uvungu ha ha ha ha ha

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

iwe kweli ama kinyume chake ukweli unabaki kuwa hayo ni matokeo ya jamii kuwafanya wanawake waamini kuwa ukipewa OFA utatakiwa kurudisha kwa kuutoa MWILI wako UTAKASWE na mbaba alotoa OFA :-(

Hata hivo pia inatokana na 'mentality' ya wababa/wakaka kutaka kitu kingine ilihali wakiema kuwa wanazimia kitu kingine!

Utamsikia mbaba/mkaka anasema anazimikia ,titiz, guu la bia, sauti, wowowo a.k.a kibinda-nkoi cha mdada/mmama kumbe anataka UVUNGU :-(

Halafu sijui ni kwa makusudi ama kwa kutojua wababa/wakaka wanakuja na kaulimbiu ya KUPENDA wakati anataka KITU ingine. Kwa ujumla hakuna UPENDO bali kutamaniana tu kwa kuwa ktk upendo hakuna kutaka kitu chochote kile.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

msinyimane

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote na karibuni tena! Na natumaini wote mmekuwa na pasaka njema.

Koero Mkundi said...

Duh, nimechelewa kutoa maoni.
Lakini nimefurahi kuw aujumbe umefika kwa amara ya pili.

HABARI NDIO HIYO!!!!!