Saturday, April 3, 2010

Heri ya Pasaka kwa watu wote/Glad Påsk alla!!!

Påskgubbe
Påskkäringar

Haya wasomaji naona sasa pasaka inakaribia. Nimeamua niwaeleze kidogo mila na desturi wakati/kipindi hiki cha pasaka huku ninakoishi ni tofauti sana na nyumbani TZ. Ngoja nianze kuwaeleza kuliko kuanza kuwachosha. Ni hivi alhamisi kuu ni kama kawaida au nimesahau sijui yaani watu wanakwenda kazini kama kawaida. Ijumaa kuu baadhi ya watu hawafanyi kazi na JUMAMOSI KUU hapa ndio sikuuu kubwa sio kama nyumbani TZ sikukuu ni jumapili.

Haya sikiliza sasa siku ile ya jumamosi watu wote ni lazima kula mayai kadiri unavyopenda bila mayai basi si pasaka tena. Wana mila hii ya kula mayai kwa sababu hapo zamani kuku waliacha kutaga mayai. Na ghafla walianza tena kutaga na siku ile ya waliyoanza kutaga ilikuwa JUMAMOSI KUU. Hii ndio sababu siku hii ni lazima kuwe na mayai mazani.

Halafu kitu kingine siku hii ya JUMAMOSI KUU watoto wadogo wanavaa kama mababu na mabibi hapo zamani. Pia wanajichora usoni na kalamu za rangi .Na pia wanakuwa na barua ambazo wameziandika/chora wenyewe kwenye vikapu. Na wanapita kila nyumba na kubadilishana na pipi. Ni mila yaani ni kama jambo la kutakiana pasaka njema. Kwa hiyo kipindi kama hiki kila kaya inabidi iwe na pipi au matunda kama huna hivyo viwili basi uwe na hela. mwanzoni nilishangaa lakini sasa nimezoea. HERI KWA PASAKA WOTE!! GLAD PÅSK ALLA!!

7 comments:

Koero Mkundi said...

PASAKA NJEMA WEWE NA FAMILIA YAKO....

MARKUS MPANGALA said...

aaaaaaaaaaah JAMANI KARIBUNI NIMEANDAA BONGE LA PIKINIKI YA KUSOMA VITABU VITANO VIPYA.

kwahiyo chaguo langu la kwanza ni ERICK a.k.a RASTA

Anonymous said...

Ha ha ha ha!
Ni taratibu ngeni kabisa masikioni mwangu,anyway tunashukuru kwa kutuhabarisha taratibu za huko.
Mimi nakutakia wewe pamoja na familia yako "GLAD PASK ALLA"....(utanisamehe hizo dot zenu za juu ya herufi nimeshindwa kuzipata kwenye keyboard yangu)

chib said...

Pasaka njema nawe

EDNA said...

Glad påsk Da Yasinta.

John Mwaipopo said...

du mayai kadri uwezavyo! ilikuwaje kuku woote wastop kutaga mayai au walikuwa katika mgomo kama ule tunaotaka kuuanzisha tanzania. ha! ha! ha! pasaka yangu ilisindikizwa na kondoo na mapochopocho mengine na.......ndio, you have guessed correctly.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote nami nawatakieni wote na ninaamini mmekuwa na pasaka njema wote. Upendo Daima!!