Saturday, April 17, 2010

Volkano yaendelea kukwamisha usafiri wa anga


Sehemu nyingi za bara Ulaya zitaendelea kukosa usafiri wa ndege mpaka alfajiri ya Jumamosi kutokana na anga kujaa majivu ya volkano yanayotimka kutoka Iceland, maafisa wameeleza.
Sehemu kubwa ya anga la safari za ndege maeneo mengi ya Ulaya kaskazini na magharibi limefungwa, huku pungufu ya nusu ya idadi za safari za ndege zikifanyika Ijumaa.

Maelfu ya abiria barani Ulaya na kote duniani wameathirika kutokana na athari za majivu hayo ambayo yanadaiwa yanaweza kuharibu injini za ndege zinapokuwa angani.

Wanasayansi wanasema volkano bado inatimka ingawa inatoa majivu kidogo ikilinganishwa na mwanzo.

Volkano ya Eyjafjallajokull ilianza kulipuka siku ya Jumatano kwa mara ya pili mwezi huu na kurusha majivu umbali wa kilometa 11 kwenda angani.

Habari hii nimeipata kutoka BBC nimeona ni vizuri wengi tujue.zaidi unaweza kusikilöiza hapa http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/04/100416_ndege_ulaya.shtml

4 comments:

Jacob Malihoja said...

Tuna pata woga na wasiwasi mkubwa Yasinta wetu na ndugu zetu wote walioko huko pamoja na wenyeji wenu wote tunawaonea huruma. hebu tuelezae athari nyingine zinazotishia usalama wenum kwa mapana. Bionafsi nakuombea Yasinta, wewe na familia yako, nawaombea pia watanzania wote walioko huko pamoja na wenyeji wenu pia muwe salama. msipatwe na madhara makubwa zaidi. na hali irudi kama kawaida.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Poleni sana banuku bapendwa mlioko huko maeneo!

Tuko pamoja nanyi

Anonymous said...

Kuwajibu wanaotaka kujua athari za huu mlipuko wa volcano ni kwamba kwa kawaida majivu ya volcano huwa yanakuwa na gesi ya karbon dayoksaidi (carbon dioxide), pia fluorine ambazo ni hatari katika mfumo wa kupumua wa binadamu. Hivyo kuvuta hewa inayobeba hizo maneno hapo juu ni hatari.
kwa namna ya pekee huu mlipuko wa Iceland umekuwa wa hatari japokuwa mlipuko wenyewe sio mkubwa sana ni kwa sababu unatokea sehemu ambayo ina barafu, hivyo ule uji wa moto unapotoka huko chini unayeyusha barafu na hivyo kusababisha mlipuko mkubwa na pia kusababisha mafuriko.
zaidi mnaweza kutembelea mitandao na kuona madhara zaidi.

chib said...

Wakati mgumu huu. Ombeeni upepo upulizie mbali hilo vumbi kwenda north pole, vinginevyo kuna siku watu watazuiwa kutoka hata majumbani. Pole kwenu