Sunday, April 18, 2010

HUU NI UJUMBE WA JUMAPILI HII YA LEO!!!

Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo. NAWAPENDA NYOTE.

Tufurahia jumapili hii kwa wimbo huu SISI SOTE NI NDUGU ulioimbwa na Innocent Galinoma....karibuni sana!!

NA NI DOMINIKA YA 16 TANGU MWAKA HUU UANZE.!!!!!

12 comments:

Anonymous said...

umepatia!

EDNA said...

Jumapili njema kwako pia.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Haya, aksante kwa ujumbe murua.

Uwe na wakati mwema.

Koero Mkundi said...

NAKUNUKUU.......

"Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo"

Kumbe nami ni mmojawapo?

Fadhy Mtanga said...

Uwe na Jumapili njema da Yasinta.

Upepo Mwanana said...

Jumapili njema dada

Mzee wa Changamoto said...

Salaam kwenu nyote msomao hapa.
Kama hujawa na moyo uliotajwa hapa, haimaanishi kuwa umepewa moyo huo na Yasinta (kama anavyodhani Da Mdogo Koero) bali wahimizwa kuwa nawe waweza kuwa mmoja wao. Anza kuishi hivyo
Nawapenda, nawathamini na kuwaombea nyote. Kwa kuwa nanyi ni ndugu zangu. Yaani kama alivyomaliza Da Yasinta, SOTE NI NDUGU

chib said...

Nimeliwazika na ujumbe, na kujihisi moyo wangu ni almasi.
Jumapili njema

Unknown said...

Ahsante dada Yasinta. Nasi twakupenda pia. Jumapili njema!!

PASSION4FASHION.TZ said...

Nawe pia na familia kwa ujumla.

Jacob Malihoja said...

Sikubahatika kupata muda wa kutosha kuwa kwenye net Jumapili, kwakweli ujumbe wa Yasinta kwa siku ya jana ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa somo muhimu kwa maisha yake. Asante Yasinta kwa ujumbe huo!

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa kutochoka kupita hapa na kuacha kitu. Nimefurahishwa sana na maoni yenuu mazuri. Mwenyezi Mungu awe nanyi na awalinde na kuwaepusha na mabaya. Upendo Daima.