Sunday, April 4, 2010

PASAKA NJEMA !!

Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye alitoa uhai wake kwa ajili yetu, imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ua hao ndugu. Yoh. 3:16-
Pasaka njema na jumapili njema sana yaani jumapili ya kwanza ya mwezi wa nne na ya 14 ya mwaka!!!

10 comments:

Koero Mkundi said...

AMEEN, AMEEN, DADA
Wakati tunaposherehekea siku kuu hii ya Pasaka ni vyema tukawaangalia watoto wa mitaani na mayatima.

Kama sehemu ndogo tu ya wale miongoni mwetu ambao tumebahatika kuwa na uwezo kidogo tungeamua kutumia sehemu ndogo ya ziada katika mapato yetu na sehemu kidogo ya muda wetu kuwasaidia watoto hawa, tungekuwa tumewaokoa wengi kati yao ambao kwa kawaida huishia mahali pabaya bila hiyari zao.

Hata kama msaada au vitendo vyetu kwa watoto hawa vitakuwa vinaonekana vidogo sana kwetu au kwa wengine kama ilivyo kwa matendo mengine yoyote ya upendo, juhudi hizo zingekuwa hazijapotea bure.

Kwa kadiri ambavyo misaada yetu hiyo ingeonekana midogo, bado ingekuwa ni mikubwa sana kwa kuchanganya na ya wengine.
Hebu jaribu na jitahidi sana kutoa msaada hata mdogo sana pale ambapo unaona wazi kabisa kwamba kuna mtoto mwenye mateso, ambaye una uhakika atafikia umri kama wako akiwa hajui maana ya upendo.

Fita Lutonja said...

Asant dd yangu Yasinta kwa kututakia pasaka njema Asante and have be blessed pia ktk post yako ya Sungura yaani imenifanya nicheke mpaka nikasahau kuwa jumatatu nina test ya EL 205 English Adv Phonology

mumyhery said...

shukran mamie na wewe pia na familia kwa ujumla

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana da Yasinta. Hakika nimekuwa na wakati mzuri Pasaka hapa jijini Mbeya. Ndugu, jamaa na marafiki wamenipa sababu nyingine ya kufurahi.

Nami nakutakia Pasaka njema wewe na familia yako.

Unknown said...

Pasaka njema nawe , Mungu akubariki sana na awabariki bloggers wote, na karibuni mara kwa mara kwenye kibaraza changu.

Unknown said...

Dada Yasinta ninashukuru tena kwa salamu za pasaka, ila tuna wakati mgumu sana hapa kwetu Tanzania kwa sababu kuna juhudi na nguvu kubwa sana za kupotosha ukweli huu tunaousheherekea na ilikwisha tabiriwa kuwa kutakuwa na upotoshaji. 2 Petro 3:15-17.

Simon Kitururu said...

Nakutakia PASAKA iliyonawili bila kujichubua Mdada!

MARKUS MPANGALA said...

@koero; MAYATIMA ni kitu gani?

heri ya pasaka wafuasi wa mambabu wa mashariki ya kati, ambao siyo wafuasi wa Kinjeketile Ngwale,Mirambo,Isike,Mkwawa,Ibin Batuta n.k

Mzee wa Taratibu said...

Pasaka njema kwenu woote hapa.

Yasinta Ngonyani said...

Shukrani kujua wote mmekuwa na pasaka njema. Kwani nami pianimefurahia pasaka kama ipasavyo.....