Friday, July 31, 2009

NGOJA TUFUNGE MWEZI HUU NA PICHA HII:-JE? WEWE UNAONA NINI HAPA?

Nikiangalia mtu huu naona kama sahani kubwa ya kupakulia ugali. Yaani mpaka raha.

6 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Naona UKUU wa uumbaji wake Muumba. Ama kweli na abaki kuwa yeye kwa namna alivyo nasi tuendelee kukubali UKUU wake.
Ameeen

Nicky Mwangoka said...

Mmmh na wewe Yasinta kwa Ugali husahau tu?Ilakusema kweli hapando unaona acha mungu aitwe mungu.

Fadhy Mtanga said...

Mi naona kitanda kizuri cha kupumzikia. No, naona sinia kubwa la kuwekea mihogo iliyochemshwa. Ile mihogo ya Songea.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mti unafanana na sahani au sahani inafanana na mti?

mtanga hiyo ni ndoto ya kweli kwani mti huo waweza kugeuzwa kuwa kitanda.

chib said...

Mimi ninamuona mjusi kwenye mti katulia chini ya kivuli cha majani

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa Changamoto! Ni kweli uumbaji ni wake muumba.

Kaka Nicky kusahau ugali sitaweza hata siku moja.

Mtani Fadhy umekosea ni sinia la kupakulia magimbi bwana.

Kamala nawe umenena kakangu.

Chib:-)