Sunday, July 26, 2009

MAJIBU KWA KAKA BWAYA KUHUSU MIMI "YASINTA"

Hapa ni maombi maalau kutoka kwa kaka Bwaya. Anasema:-Dada Yasinta, mie nina maombi maalumu yafuatayo:

1. Tutajie mambo kumi tusiyoyajua kuhusu wewe. Uamuzi wa yapi unaweza kutuambia, unabaki kuwa wako.

2. Ni watu gani watano huwezi kuwasahau katika maisha yako?

3. Mambo yepi mawili yanatumia muda wako mwingi katika masaa ishirini na mane ya siku?

Nami nimejitahidi kujibu kama ifuatavyo:-

1. Tutajie mambo kumi tusiyoyajua kuhusu wewe. Uamuzi wa yapi unaweza kutuambia, unabaki kuwa wako.

=Mpole kiasi
=Mcheshi
=Mwenye upendo kwa watu wote bila kujali rangi, dini, kabila na itikadi
=Anayejali familia
=Anayependa kujitolea kuisaidia jamii, kwa njia mbali mbali
=Asiyependa majungu
=Mdadisi na anayependa kujifunza mamabo mapya
=Anayependa kuwafundisha wengine yale anayoyafahamu
=Anayependa kusikiliza muziki wa aina mbali mbali
=asiyependa kuona jinsia ya kike ikidhalilishwa kwa sababu ya mfumo dume



2. Ni watu gani watano huwezi kuwasahau katika maisha yako?
=mama yangu na baba yangu
=Mzee aliyenilea nilipokuwa masomoni chuo cha kupiga chapa
=Rafiki yangu aliyenipeleka hospitali nilipokuwa naumwa na mguu baada ya kuchomwa na mwiba wa samaki
=Mume wangu
=watoto wangu

3. Mambo yepi mawili yanatumia muda wako mwingi katika masaa ishirini na mane ya siku?


=Familia na kublog
=Kazi

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

11 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Kama ni kampeni binafsi basi ungeshinda maana umejipigia upatu mkubwa saaana. Sema kwenye swali la pili, mtu wa nne na watano ndio wanaweza kuweka kauzibe kwa wakware (Lol)
Bwaya ana maswali magumu jamani. Nadhani ningepata wakati mgumu kuyajibu haya. Lakini nafurahi umeweza na nashukuru kuwa nimejifunza kitu.,
Amani kwako, kwa Bwaya na kwa FAMILIA YAKO PENDWA.
Bless

Fadhy Mtanga said...

Duh kaka Bwaya mgomvi. Lakini kaka yangu Mubelwa hicho cha tano, watoto siyo tatizo, tatizo ni hiyo namba nne.

Halafu mbona da Yasinta amejieleza sana? Ama ndo mazoezi ya twenty ten?

Ila kujieleza unajua.

Faith S Hilary said...

Hapo wala sibishi chochote because you seem like a very nice person

Albert Kissima said...

Ewaaaa! Sasa nimemfahamu dada Yasinta kwa uzuri zaidi. Dada Yasinta umesema wewe ni mpole kiasi, ina maana ni mkali wastani au?(hahahaaaaaaa!)

Nicky Mwangoka said...

100% zamani tukiwa UPE ulikuwa unaanikiwa mia ya mia, halau wanazungushia duara na nje ya duara mwl anaandika Vizuri sana.Ndicho ulichopata Yasinta.You are Brilliant!

Unknown said...

MPOLE KIASI!!!!???? DUH!!!!!

Simon Kitururu said...

Unauhakika wewe sio Malaika?:-(

Fadhy Mtanga said...

Atakuwa ni malaika tu! Maana duh!

www.tanzaniasports.com said...

Du Pole sana kwa huo Mwiba wa SAMAKI!Miiba mingi ya samaki ina maumivu sana,Bahati ulikochoma mguuni,Ingekuwa kooni ungeumia sana Yasinta!.Pole

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni sana.Maoni mazuri WOTE MNAPENDWA.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bora ukawaulize woote wakuchukiao na kuwauliza sababu za chuki na uziandike kuwa ndio wewe!!!!! nnnnooooot