Saturday, July 4, 2009

TUFANYEJE ILI TURIDHISHANE KIMAPENZI?

Ilibainishwa humu hivi karibuni kuwa utafiti ulionyesha kuwa baadhi ya wanaume wana haraka ya kufanyamapenzi (sex). Habari ile bado inawafanya baadhi yenu kuendelea kunitumia mails zenye michango ya hoja na maswali pia.
Miye si mwalimu katika hili bali nimerejea dondoo za utafiti uliofanywa na wengine. Maana tunajifunza kutokana na uzoefu wetu na uzoefu wa wengine.
Hapa kuna swali; “Tufanyeje ili turidhishane kimapenzi?
Hatuhitaji watafiti ili kufahamu kuwa cha msingi na kikubwa kabisa ni MAWASILIANO kati ya wawili wapendano. Tumeona kuwa kufanya sex si kazi rahisi. Inahitaji muda, mwanamme anaweza akajisikia kuwa haridhiki na partner wake kwa vile partner hawi wa kwanza katika kuonyesha anataka na mengineyo.
Mwananme anaweza akahisi partner wake hampendi. Kama tulivyoona, mwanamke anahitaji muda zaidi ili awe tayari. Kushikana na mabusu yana umuhimu wake, lakini hata kumsaidia partner wako na kazi za nyumbani kunaongeza hamu ya mapenzi kwa patner wako.
Kama ni mwanamme, jaribu siku moja moja kushiriki kazi za nyumbani. Ni wajibu wako pia na inamsaidia mpenzio hata inapofikia wakati wa shughuli yenyewe. Hata kama ni baba nyumbani jitahidi basi kufagia, kuzoa takataka za nyumbani na kwenda kuzitupa pipani, it’s sexy too!
Ikumbukwe, kuridhishana ni kuridhiana. Na kikubwa ni MAWASILIANO. HABARI HII INATOKA http://www.kwanzajamii.com/ Asante kwa habari hii.

5 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Kumbe kuna haja ya kurejesha "jando na unyago" maana yaonesha namba ya wasioridhishana ni kubwa. Hivi zamani ilikuwa hivi ama hawakuwa na ujasiri wa kusema kuwa hawaridhishwi? Ama kwa kuwa "wazee" walikuwa wakishiriki kazi za nyumbani ndio maana ilikuwa inasaidia (kama ulivyosema kuwa kushiriki kunasaidia)? Labda mfumo wa maisha wa sasa hauwapi wanaume wengi muda wa kushiriki mambo mengi ambayo babu zetu walifanya na hivyo "kuwasaidia" mabibi zetu kuridhika.
Sina hakika kama ni mitazamo, ama mfumo wa maisha ama mabadiliko ya "kimaumbile" yanayosababisha haya, lakini naamini zama zimebadilika na mambo mengi yanaambatana nazo.
Nami si mtaalamu pia. Lol

Bennet said...

Ukimuachia mkeo mikazi mingi basi ukifika muda wa kufanya mapenzi anakuwa amechoka sana kwa hiyo hata kuamsha hisia zake za mapenzi inakuwa ngumu
mwanaume unatakiwa ufanye zile kazi ngumg ngumu na kumuachia mwenza wako zile rahisi rahisi kwa sababu hisia za mwanaume kwenye mapenzi ni sekunde chache tu yaanio hata akiona tu anasisimka

Simon Kitururu said...

Mimi somo hili limenishinda na LILINISHINDA ZAMANI ndio maana katika WALI nashindia UBWABWA halafu mpaka naanza kuhisi UBWABWA ni mtamu kama PILAU:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuna wakati hata mwanaume anachoka huku mama akidai msuguo!

harafu yasinta neno kufanyamapenzi sio kiingereza cha sex bali ku-make love, inamaana hakuna neno Sex kwa kiswahili au ni matusi? hamkawii kutukanwa nyie!

Yasinta Ngonyani said...

Asanteni sana wote kwa maoni yenu na kwa kuwa na moyo wa kunitembelea daima.

Kamala Asante kwa kunisahihisha.