Friday, July 10, 2009

KWA NINI WANAUME/AKINA BABA WENGI WANAFIKIRI WAO NDIO WAAMUZI/WAFALME WA NYUMBA?

Suala hili limekuwa likinikera sana akilini mwangu kwa miaka mingi. Ya kwamba akina baba/wanaume wao wanafikiri kazi yao kubwa katika nyumba ni kuwa MUME/BABA basi. Mara nyingi utasikia wanasema mimi ndio mkubwa wa nyumba. Na kama wanafanya kazi za ofisini basi ndo itakuwa kero mno. Kwani hapa atataka anaporudi toka kazini akute chakula mezani, maji ya kuoga bafuni tena ya moto, nguo zimepigwa pasi n.k. Na kinyume kama hana kazi basi atakuwa anashinda kilabuni(UGIMBI) na akirudi toka huko basi ni kelele tu, hakuna amani wala maelewano

Bado naendelea, kuna wengine wanaona kupika, kulea watoto, kutafuta chakula ni kazi ya wanawake. Yaani hawawezi hata kujipikia chai kwa vile wao ni wanaume au hata kumbadili mtoto nepi, Mtoto amabaye ni wake. Kikubwa wanachofanya ni kukaa kitini/sofani na kuletewa kile wanachotaka. Wanasahau kabisha jambo la USAWA.

Bado wanaishi dunia ya mababu, mababu na mababuzi. Tuache UBINAFSI tuishi kwa kushirikiana/kusaidiana kwani wote ni SAWA. Nasema tena tuishi kwa kusaidiana hapo wote tutafurahia maisha. Tuache mambo ya UTUMWA.

7 comments:

chib said...

Da Yasinta. Ukweli ni kwamba hakuna mahali popote penye usawa. Wanaume na wanawake wameumbwa tofauti kinasaba. Hakuna usawa(equal) ila upo uwiano(fairness). Kwa njia ya kawaida mwanaume hawezi kubeba mimba au kutoa maziwa ya mtoto kunyonya, na pia mwanamama kuna mengi ambayo mwanamama hawezi kuyafanya. Kwa sasa mtu akiondoa ubongo wako wa mbele(FRONTAL LOBE) utaendelea kuishi lakini hutakuwa na hisia ya aibu, utatukana bila kujua, sababu control ya aibu itakuwa imetolewa.
Nafikiri upigie debe uwiano kuliko usawa, kwani hakuna hata siku moja kutakuwa na usawa kati ya wanaume na wanawake iwapo kila mmoja ataendelea kuwa na genes za sasa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kama mumeo yuko hivyo ni yeye pekee wengine hatuko hivyo!!!!!!

(samahani kama ukweli unakuuma, nihurumie labda nimelewa badala ya kumsaidia mke wangu!) duh wanaume wengine bwana!

Anonymous said...

sidhani kama kutakuwa na kitu kama hicho hata siku moja. muulize Mungu labda anajua kwanini alituumba tofauti hivyo. na mkidai dai sana ipo siku mtaanza kutaka wanaume wabebe mimba pia, si ndio usawa wenyewe huo maana mtasema mmechoka kubeba mimba peke yenu!!

Anonymous said...

haya mambo mnayoyaita utumwa ni adhabu toka kwa Mungu na aliyesababisha ni mwanamke mwenzenu Eva, yeye kwa uzembe wake akakubali na kumshawishi mwenzake, sasa wanaume tumekuwa wajanja, hatukubali kila kitu mnachotaka ninyi jinsia ke, maana mlishatuingiza mkenge

Bennet said...

Huu unaitwa mfumo dume na umeenea sana Afrika na kwingineko na hii inatokana na jinsi tulivyoumbwa wanawake hamuhimili hali za shuruba kali na mfumo huu upo kwa karne nyingi
Hapa kinachotakiwa ni kudai haki za mwanamke na sio usawa, kwetu sisi tumezoea kazi ngumu kama za kuwinda, kuchunga na kuchanja kuni ni za wanaume na wanawake wanafanya kazi kama za kuchota maji, kupika na matunzo ya familia. Kazi nyingine ni za wote mfano kulima, kukamua n.k

Nicky Mwangoka said...

KUPUNGUA KWA USAWA HUO KUNATOKANA NA MILA POTOFU KATIKA BAADHI YA MAKABILA, NA PENGINE TU KUTOKUELIMIKA.

Albert Kissima said...

Mimi nadhani swala la usawa na uwiano yawekwe kando kabisa.Pamoja na kwamba ktk familia kuna majukumu ya baba na mama kwa jinsi tulivyozoea, lakini pia kuna majukumu ambayo yaweza kufanywa na yeyote,tatizo huwa linakuja , nitaonekanaje?
Baba anaweza kumbadilisha mtoto nepi, anaweza kumwandalia mke wake maji ya kuoga na hata kumtengea mke chakula mezani, mke vilevile anaweza kuchanja kuni ,anaweza kutoa taratibu fulani au majukumu, anaweza kwenda kununua mahitaji muhimu ya familia n.k na mambo mengine ambayo yanadhaniwa kuwa ni ya kina baba lakini yako ndani ya uwezo wa kina mama.
Haya yanawezekana kama tu kuna upendo wa kweli na wawili hawa wataishi bila kuogopa macho na hata maneno ya watu.

Wanandoa wanaogopa kuambiwa kuwa fulani bwana kawekwa kiganjani kisa mme kaonwa akiteka maji, mme kaonwa akifua nguo zake mwenyewe,
mke ananyanyaswa, kila kitu yeye kazi za ndani hata mpaka kwenda kununua mahitaji ya familia.
Ni hayo tu.