Thursday, July 16, 2009

NI MARA CHACHE SANA UTAKUTANA NA MWANAUME AKITOA MACHOZI YA UHAKIKA

Chozi
Wanawake kweli ni viumbe wa thamani ambao wakati mwingine hushangaza; hata hivyo yote ni kwa utukufu wa Mungu aliyetuumba tuwe tofauti ili kukamilishana.

Machozi ni moja ya vitu ambavyo mwanamke huhusika moja kwa moja hata katika malezi wazazi wetu walikuwa wanatuonya watoto wa kiume tusilie tukikutana na jambo kubwa au gumu kwani walisema kulia ni mwanamke na si mwanaume.

Mwanaumke huweza kutoa machozi akifurahi, akihuzunika, akikutana na rafiki au ndugu ambaye walioachana muda mrefu, hata wakati mwingine hutoa machozi ili kupata kitu na wakati mwingine hutoa machozi kwa kupoteza kitu katika miliki yake yaani moyo, na kwenye misiba basi huko usiseme maana ukichanganya na mila inakuwa shughuli nzito.
Kwa maelezo zaidi ya machozi na mwanamke soma hapa

Pia machozi ni moja ya silaha mwanamke hutumia hasa kujilinda kwani anaweza kujieleza kwamba tafadhari “Usiniambie mapungufu yangu la sivyo nitaaza kutoa machozi sasa hivi”
Hata hivyo kazi kubwa ya mwanaume ni kutofautisha machozi ya hisia, msongo wa mawazo na uchoyo, ni kweli mwanamke ni emotional creature ambaye mwanaume lazima uwe makini to handle with care.

Hata hivyo Watafiti wengi wanakubaliana kwamba mwanamke anayetoa machozi ni mzuri sana lipokuja suala la hisia katika maeneo yote ya maisha hii ina maana kwamba mwanamke mwenye kumwaga chozi mara kwa mara ni mtamu chumbani kwa sababu anaweza kujieleza katika lugha ya mapenzi (love making, act of marriage) Na mwanamke mwenye macho makavu maana yake ni mgumu kuji –express wakati wa kuwa mwili mmoja.

Wanawake wenye machozi ni mara chache sana kuwa baridi (frigid) wakati wa kuwa mwili mmoja kwani ukimwandaa ni rahisi kuwa connected kihisia.

picha na maandishi kutoka kwa kaka Lazarus Mbilinyi :- mbilinyi.blogspot.com

7 comments:

Simon Kitururu said...

Swali kwa akina dada:

Hivi ni kweli Mwanaume akililia ni rahisi kuhurumiwa akapewa chakula cha usiku?
Nauliza kwa sababu kunatetesi zinaelea kuwa kulilia ni bomba la mtongozo wenye mafanikio sana. Je ni kweli?

Tamaduni zetu zinafunza wanaume wawe ngangali.

Nakumbuka wakati mdogo nishawahi kuingizwa mkenge kula pilipili kichaa halafu naambiwa nikilia mie sio dume.

Basi wacha nihangaike na pilipili huku chozi linalenga na nalikatalia lisitoke kwa kujitahidi kuhakikishia umati mie dume!:-)Halafu kumbuka nilikuwa na miaka saba tu na tayari nilishaelewa kama wewe dume huhitaji kuonekana unalia .:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

swali, vipi yasinta, wewe wakati wa kugawa penzi huwa unatoa chozi?

(samahani sana usinichukulie vingine)

Fadhy Mtanga said...

Machozi!
Mi siyaamini hususani katika mapenzi.

Mzee wa Changamoto said...

Kuna jamaa yangu kamaliza kunywa dawaza kumpa machozi. Ndio nimesoma hapa kisha nikamwangalia (na wala hajui kwanini nimengalia maana hata Kikwetu hakielewi) lakini nikaishia kujiuliza.
Hivi machozi yananunuliwa??? Mmhhhh. Basi alivyosema Kaka Lazarius ni kweli kuwa twahitaji kutofautisha machozi na hisia maana kuna wakati machozi si hisia.
Sasa najiuliza tena.
Kwani mwenye HISIA bila machozi ataonekana sawa na mwenye chozi bila hisia?
Kwani ni kipi cha kuthamini na vipi utakijua?
Nawaza tuuuuu

John Mwaipopo said...

maswali mengine! du!

mumyhery said...

mhuu makubwa!!!

Christian Bwaya said...

Pengine jambo hili linahitaji utafiti. Lakini kwa sasa nijiavyo ni kwamba wanaume na wanawake wana hisia sawa sawa. Kinachotutofautisha si maumbile ila ni mazingira tunamokulia.

Machozi hisia yanatofautiana kwa sababu tu za kimazingira. Namna watoto wa kiume wanavyokuzwa huwafanya kujifunza kudhibiti machozi yao (hasa hadharani)hata kama moyoni wanabubujika machozi.

Machozi ya kihisia ni matokeo na si asili ya kihisia. Tunadhibiti machozi kulingana na makuzi. Mambo tuliyosikia wkati tunakua. Ndio maana wapo wnaawake wagumu kulia kuliko hata mwanaume.

Kama tukizungumzia kazi ya machozi kiutendaji wa mwili, tunafanana. Machozi kazi yake kusafisha jicho. Hili si tendo la hiari. Ndio maana napata shida kuamini maelezo ya Mkodo kwamba aliwekewa pilipili na akaweza kuligomea chozi lisitoke. Maana, kwa mukhtadha huo, chozi halitokani na amri yake (uamuzi). Kwa vyovyote, angelia labda iwepo hali isiyoya kawaida. kwa sababu hapo mwanaume na mwanamke wanafanana katika kutoa machozi.