Friday, July 24, 2009

SALAAM KUTOKA SWEDEN KWENDA MAHENGE - SONGEA



Katika maisha kuna wengine maisha yao yote wameishi na baba na mama. Lakini kuna wengine wameishi na watu tofauti tofauti. Kati ya hawa watu walioishi na watu tofauti tafauti ni mimi. Kuanzia mwaka 1989 mpaka 1991 nilikuwa naishi na familia ya mzee Innocent Kapole Nyoni Mahenge Songea.
Kipindi hicho nilikuwa nasoma chuo cha typing pale Songea. Nilipotoka pale ndo nikaenda Sec.School Wilima kuanza kazi. Kwa hiyo huyu mzee ni mtu muhimu sana kwangu. Kwani yeye ndiye aliyenitafutia kazi ile. La sivyo leo nisingekuwa hapa ninablog na kufahamiana na watu wote niliofahamiana nao.
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa familia nzima. Kwani wao wamekuwa kama familia yangu kabisa. Mungu awe nanyi daima.

10 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Hakika una kila sababu ya kumshukuru na kumuombea yeye na familia yake. Kama kila awezaye kuwa msaada kwa (japo) mtu mmoja angefanya hivyo, ulimwengu huu ungekuwa mahala bora sana pa kuishi. Tungeendeleza upendo ambao tunaoneshwa na kuweka mbali visasi vinayotawala sasa.
Maisha yangekuwa na upendo kama tusingekimbilia kutaka makubwa na kama kila kidogo tulichonacho tungeweza kukishirikisha kwa UPENDO. Mother Theresa alisema "i can do no great things, ONLY SMALL ONES WITH GREAT LOVE." na pia nakumbuka Lucky Dube aliimba katika wimbo wake wa HERO kuwa "you don't think it's much, but to them it means a WORLD. They wake up in the morning and wish you were there, you don't have to lie to gain their trust..... YOU'RE A HERO."
Shukrani kwa familia kwa "kukuwezesha" kuwa ulivyo na kwako wewe kukumbuka kuwathamini na kuwaombea pia.
You're all HEROES

Simon Kitururu said...

Sina chakuongezea maana naona Mzee wa Changamoto kanikata tayari Kauli!


DUH lakini nashindwa kukwepa kuistukia hiyo chupa pichani!:-(

chib said...

Nami sina cha kuongeza, ila picha hiyo inanikumbusha Singida, niliwahi kuwakuta wazee wamegeuza chumba cha darasa kuwa baa siku ya jumapili. Darasa lenyewe limekaribia kufanana na hii picha!!

Christian Bwaya said...

Shukrani nyingi kwa mzee wetu. Ametulelea rafiki yetu vizuri na bila yeye, leo tusingekuwa tunajadiliana na wewe kwa nyenzo hii.

Dada Yasinta, mie nina maombi maalumu yafuatayo:

1. Tutajie mambo kumi tusiyoyajua kuhusu wewe. Uamuzi wa yapi unaweza kutuambia, unabaki kuwa wako.

2. Ni watu gani watano huwezi kuwasahau katika maisha yako?

3. Mambo yepi mawili yanatumia muda wako mwingi katika masaa ishirini na mane ya siku?


Naamini hutasita kufanya hivyo, na siku njema.

Faustine said...

Ni vyema kukumbuka tulikotoka na pia kuwakumbuka na kuwaenzi waliotuwezesha kufika hapa tulipo.
Unafanya vyema.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/

Albert Kissima said...

Ni jambo jema kabisa dada Yasinta kumkumbuka huyu mzee na familia yake kwa ujumla.Wajizolea baraka teleeeee na mafanikio zaidi kwa yote uyafanyayo

Unknown said...

Ni vizuri kuwakumbuka wale waliochangia japo hata kidogo katika kukua kwetu.
ahsante dada kwa kuonesha njia, ni vyema tukifuata nyayo zako.

Nicky Mwangoka said...

Ni kweli Shukuruni kwa kila jambo"
Umefanya vizuri sana kuwakumbuka watu hawa muhimu kwenye maisha.Mungu awabariki wote waliokusaidia na wanaoendelea kukusailia kwa namna yoyote.

Yasinta Ngonyani said...

Shukrani tena na tena kwa maoni yenu. Watu tumetoka mbali na tuna maisha ya ajabu ni hayo tu. Asante sana familia ya Mzee Kapole Nyoni kwa kila kitu mlichonitendea nadhani ndio sababu mpaka leo hii nipo hapa nilipo.

Anonymous said...

Dada kumbe umefanya kazi shule ya kunyumba kabisa(Wilima S.S) aisee nafurahi sana kusikia hilo,mimi ni wa kulekule Lilondo pale na Mzee wangu ameitumikia sana hiyo Wilima,nitakutafuta privately tulonge zaidi.
All the best.