Thursday, February 19, 2015
Wednesday, February 18, 2015
Kitabu Kipya cha NYUMA YA PAZIA KIMETOKA!
Thursday 12 February 2015, author(s)-editor(s) Nkwazi Nkuzi Mhango
Nyuma Ya Pazia inazungumzia ubadhirifu unaomhusisha rais na mawaziri wake katika nchi ya Mafuriko au Abracadabra. Rais akishirikiana na waziri mkuu walileta kampuni ya kigeni ya kuua wadudu ya Richmen kuwekeza kwenye kuzalisha umeme nchini Mafurikony; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Kupitia rushwa na ushawishi wa wakubwa hawa Richmen ilipata tenda na kutumika kama mrija wa kuibia mabilioni ya fedha za umma toka Benki Kuu. Wananchi walipogundua jinai hii waliiangusha serikali na kuwaaadhibu watawala wao kwa kuwafunga maisha na wengine kuhukumiwa vifo. Kitabu kinaupiga kijembe tawala fisadi barani Afrika.
Nyuma Ya Pazia or Behind the Curtain is about corruption involving the president, and his ministers who rob the country of Mafuriko or Abracadabra. President in conjunction with his Premier brought fake foreign insecticide company; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Through logrolling Richmen lands a very lucrative tender used as a conduit of stealing millions from the Central Bank. Richmen is used to syphon billions of dollars from the treasury. When people get wind of this theft, force the government to crumble thereby rulers are punished by being jailed or other being sentenced to death. The book satirizes African kleptocratic regimes.
ISBN 9789956792184 | 254 pages | 203 x 127mm | 2015 | Langaa RPCIG, Cameroon | Paperback
Tuesday, February 17, 2015
HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA WIKI!!!
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU HII YA JUMANNE IWE NJEMA NA PIA TUWE WAANGALIFU JINSI YA KUTUMIA MANENO KWA WATOTO WETU!!
Saturday, February 14, 2015
NAPENDA KUWATAKIENI HII SIKU YA WAPENDANAO IWE NJEMA NA YENYE AMANI.
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU HII YA WAPENDANAO IWE YENYE AMANI.
HUU ULIKUWA MLO WANGU WA JANA JIONI PILAU, KACHUMBALI HAKUKOSA...JUMAMOSI NJEMA.
HUU ULIKUWA MLO WANGU WA JANA JIONI PILAU, KACHUMBALI HAKUKOSA...JUMAMOSI NJEMA.
Friday, February 13, 2015
SWALI LETU LA IJUMAA YA LEO!!!
Swali letu la lau ni kama lifuatavyo:- Kwa nini wanawake wanaishi maisha mazuri, marefu na yenye amani ukilinganisha na wanauma?
NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA/MWISHO MWISHO MWEMA WA JUMA!!
NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA/MWISHO MWISHO MWEMA WA JUMA!!
Wednesday, February 11, 2015
TUDUMISHE UASILI WETU/UTAMADUNI WETU!!!
Mdada akichunja pombe ya asili, na hivyo ndivyo walivyofanya hapo kale na pia kuna baadhi ya sehemu Afrika bado inafanyika hivyo
Na hapa ni nyumba ya asili huko Afrika ya kusini/ hasa kwa kabila la kizulu. Ambao inasemekana ni wanaukoo na wangoni.
Na hapa ni nyumba ya asili huko Afrika ya kusini/ hasa kwa kabila la kizulu. Ambao inasemekana ni wanaukoo na wangoni.
Na hapa ni nyumba ya asili ya wangoni iliyopo Songea pale Makumbusho ya Mashujua
Tuesday, February 10, 2015
TUWE MAKINI TUTUMIAPO VINYWAJI MAANA KUNA WENGI WANAPENDA!!!
Hii inanikumbusha siku moja tulikuwa na sherehe na katika shamrashamra basi kaka mmoja akawa amechukua bia yake na kunywa kumbe mende walikuwa wamemwahi. Na pia mwingine aliingingiliwa na nyuki akamuuma mdomoni na kuvimba vibaya mno. Kwa hiyo ndugu zangu tuwe makini. Tutaonana tena panapo majaliwa...Kapulya!!
Friday, February 6, 2015
IJUMAA YA LEO TURUDI TENA ZANZIBAR !!!
Nilimwuuliza aliyetuongoza (guide) kama ningeweza kutumbukia humo shimoni na kupigwa picha. Lakini alisema hairuhusiwi. Hakika ndugu zetu waliteswa sana halafu mbaya zaidi hawakuwa wanaume tu hata wanawake pia watoto. Niwachekeshe kitu huyu guide weyu alikuwa na vichekesho mno akaniambia nami nilionekamna kama mmoja wao:-) IJUMAA NJEMA!
Thursday, February 5, 2015
SOMO LA ALHAMIS HII:- TUSISAHAU USAFI WA KUCHA ZETU
Kucha ni kitu cha msingi sana na kutakiwa kuwa safi wakati wote sababu mikono yetu hutumika mara nyingi mfano mapishi, kufua, kuosha vyombo n.k. Usafi wa kucha zetu ni muhimu kwetu wanawake lakini tujue tuna jukumu la kuhakikisha waume zetu, wapenzi zetu na hata watoto wetu wawe wasafi kwa kucha zao (Mikono na Miguu)
------------------------------------------------------------------------------
Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.
Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.
Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele.
Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.
Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.
Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.
Usitoe ovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.
Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa.
Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, badala ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembe au kitu chenye makali.

Tuesday, February 3, 2015
JUMANNE YA LEO TUANZE NA:- HADITHI YA WAPENDANAO!!!
Katika pitapita zangu nikakutana na hadithi hii na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa ili wengi tupata faida...karibu
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mdada mmoja alitaka kujua anapendwa kiasi gani na mumewe. Hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha. Mwanamke akaamua kuandika barua inayosema"Samahani mume wangu nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali na wewe. Barua akaiweka juu ya meza iliyochumbani .Baadae jioni, muda wa mumewe kurudi akajificha chini ya uvungu wa kitanda chumbani. Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma kisha akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga miluzi na akiwa anavua nguo. Akapiga simu na akasikika akisema"Mpenzi nina furaha sana leo ..yule mwanamke nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na kutuachia uwanja, jiandae nakuja "Muda huohuo akaondoka. Mwanamke alipotoka uvunguni alikuwa amenyong'onyea na ameloa mashavu kwa machozi, akasogea pale ilipo barua na kutaka kujua mumewe kaandika nini. Akakuta maneno haya. "Nimeona miguu yako uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. NAKUPENDA SANA MKE WANGU".......

Monday, February 2, 2015
BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUMPONGEZA KAKA SAMWEL MBOGO "SAM" KWA KUFANYA GRADUATION
Sunday, February 1, 2015
NI JUMAPILI NYINGINE TENA YA MWEZI MPYA...DAWA YA KUSAMEHE NI UPENDO!!
JUMAPILI NJEMA! UJUMBE TOKA KWA KAPULYA:- TUDUMISHE UPENDO NA TUWE WEPESI KUSAMEHEANA!
Thursday, January 29, 2015
TUSISAHAU METHELI ZETU:
1. Njaa ni adui, hata mchawi yaua.
2. Haki ya nyani kuona fahari kwa mkia wake
3. Heri yao wazee kujifunga kwa mshipi tumboni.
4. Yu mcheshi machoni moyoni kuna mengine.
5. Binadamu ujikaze, Mungu atakusaidia.
6. Ee mtoto utakutana na watu katili.
7. Yakiteguka mapaja choo hutoka ovyo.
8. Mtoto wa simba sharti naye awe simba.
9. Yu ndugu machoni
10. Fuata maji yanakokwenda.
Methali hizi nimezipata katika kitabu cha SIASA HAPO KALE ni methali katika hadithi za kingoni. Ambazo zimetafsiriwa kwa kiswahili. Na kwa kingoni nimeweka kwenye blog ya vangoni.blogspot.com.

Tuesday, January 27, 2015
JINSI KAPULYA ALIVYOINASA TASWIRA YA LILONDO....AKINA MAMA WAJASILIAMALI....
Hapa ni Lilondo, huwezi kupita hapa bila kusimama ni kijiji chenye ndizi nyingi sana kama unavyoona akina mama wajasiliamali wanavyochangamka wakati basi la Super Feo liliposimama. Kwa hiyo upitapo Lilondo usikose kusimama kununu ndizi... maana kuan kila aina uwezo wako tu..karanga pia. PAMOJA DAIMA!!
Monday, January 26, 2015
TUANZA JUMATATU/WIKI HII NA MSEMO HUU!!!
Kama binadamu, huwezi kamwe kuona aibu kwa kutokubali kosa. Kwa maneno mengine hii inaweza ikasemwa ya kwamba mtu ana akili leo kuliko jana.
NI MATUMAINI YANGU WIKI IMEANZA VIZURI KWA WOTE! MWANZO MWEMA WA WIKI.
NI MATUMAINI YANGU WIKI IMEANZA VIZURI KWA WOTE! MWANZO MWEMA WA WIKI.
Saturday, January 24, 2015
JUMAMOSI NJEMA...NIPO NA KAKA ZANGU KATIKA UPANDAJI WA MITI RUHUWIKO/SONGEA 2015 JANUARI
Nipo na kaka zangu tunapanda miti, huu mti niliosimama nao karibu niliupanda mwaka 2013 na sasa umenipita urefu kazi kwelikweli. Kata miti na pia panda miti kwani ndio uhai. Huu ndio ujumbe wangu wa leo!JUMAMOSI NA MWISHO WA JUMA MWEMA!! KAPULYA.
Thursday, January 22, 2015
HOSPITAL YA MBEYA YATEULIWA KUPIMA EBOLA!!
Mbeya. Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), imeteuliwa rasmi kuwa na maabara maalumu ya kuwapima watu watakaohisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa ebola.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Mpoki Ulisubisya alisema hayo jana jioni alipozungumza mambo mbalimbali kuhusu changamoto zinazoikabili hospitali yake.
"Ni kweli Serikali imeiteua maabara yetu ya hospitali kuwa maabara maalumu ya kupima virusi vya ebola nchini na kwa sasa maandalizi yote yanakamilishwa na tutaanza kazi mwishoni mwa mwezi huu au mapema Februari’’ alisema.
Kwa kipindi cha miaka mitano sasa, Maabara ya Hospitali ya Rufaa Mbeya ni maabara ambayo imethibitishwa kimataifa kwa ubora na kwamba vipimo vikitolewa kwenye maabara hiyo vinakubalika hata nchi za Marekani na Uingereza.
Akizungumzia uboreshaji wa utendaji kazi amesema wafanyakazi kupitia kwa viongozi wao kwa sasa wameimarisha utendaji kazi.
Kuhusu chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali hiyo, Ulisubisya amesema Serikali imempata mtu atakayejenga jengo kubwa la kuhifadhi maiti na kuliboresha ili kuendeshwa kwa ubia katika hali ya usafi na kisasa zaidi.
‘’Bila shaka unakumbuka , mfanyakazi wa chumba cha maiti aliwahi kumweleza Waziri kwamba ukifariki dunia ukiwa Mbeya maiti yako italazwa chini. Sasa Serikali imeamua kuchukua hatua ili kuboresha nyumba hizo ingawa wahusika watatakiwa kutoa mchango kidogo’’alisema.
Mapema mwaka jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid wakati huo akiwa Naibu Waziri alitembelea hospitali hiyo ambapo mfanyakazi wa Chumba cha maiti, Vuruga P Vuruga alimweleza kiongozi huyo kwamba maiti zinalazwa mbili mbili kwenye chumba chenye uwezo wa kuhifadhi watu sita.
Vuruga amesema kutokana na kasi ya kufa, hivi sasa maiti zinalazwa chini na kwamba hata Naibu Waziri angefariki akiwa Mbeya ajue maiti yake ingelazwa chini.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
Tuesday, January 20, 2015
NA ZANZIBA PIA TULIFIKA!!
PAJE BY KITE ZANZIBAR
Kama kawaida ukifika Zanzibar ni vigumu kuacha kwenda kusuhudia jinsi ndugu zetu walivyoteswa kama watumwa.
Monday, January 19, 2015
Sunday, January 18, 2015
JUMAPILI HII YA TATU NAONA WIMBO HUU :- NAMSHUKURU MUNGU UNAFAA.
Nami nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote. Ahsante Mungu-
Wednesday, January 14, 2015
HII NI KAZI YA MIKONO YETU WENYEWE....UTAKULA ULICHOPANDA.....NYUMBANI SONGEA/RUHUWIKO!!!!
Tumekuta ndizi tulizopanda zimekomaa na tumezila hapa ni baadhi tu.....
...tuliendelea na mihogo pia nanasi/mananasi.. kazi ya mikono ya kapulya------hatukuishgia hapo....tukayala na maembe maana huu mti upo ndani ya eneo letu yaani tunaumiliki:-)......
----bado tukaendelea na matunda ya ambayo pia ni kazi ya mikono yetu.."passion"....tutaendelea na picha zaidi...zinakuja:-)
Tuesday, January 13, 2015
TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO
Ni muda mrefu sijafungua barua pepe yangu, kwa vile nilikuwa safarini. Nimefungua nimekuta hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio, nimeona si vibaya kugawana elimu....karibu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.

Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.
Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”
Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!
Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.
Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu:“Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu” Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu.
“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.
Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.
“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.
Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”
HEKIMA:1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.
2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILA YA KUJALI HALI ULIYONAYO.
Monday, January 12, 2015
HODI..HODIII....NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU NIMESAFIRI SALAMA NA NIMERUDI TENA SALAMA
KAPULYA KIZIZINI PERAMIHO 2/1/2015
Nachukua nafasi hii kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda katika safari yetu na pia sasa tumerudi salama tena. Pia ahsanteni kwa sala zenu. Nilikuwa natamani kula nyama ya ngómbe nikaona ngoja nitembelea kizizini Peramiho kwa wale wanaotokea Songea wanajua ni wapi. Na wewe usiyejua ni njia ya kwenda Peramiho upande wa kushoto kama unatokea Songea.TUPO PAMOJA ....
Monday, January 5, 2015
KAPULYA ANATIMIZA MIAKA LEO... NI TAREHE NILIYOZALIWA LEO:-)
Leo ni tarehe/siku ambayo familia ya Mzee Ngonyani ilikuwa na furaha kumpati binti yao ambaye alizaliwa siku hii ya leo. Na leo ameongoza mwaka tena na kuzidi kuzeeka. Lakini hata hivyo anapenda kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki kwa siku hii ili tumsaidie kusherekea. Na wote manakaribishwa..sana. NAWATAKIENI SIKU NA WAKATI MWEMA. WOTE MNAPENDWA SANA ...KAPULYA Nachukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama .
Thursday, January 1, 2015
SALAMU KUTOKA SONGEA/RUHUWIKO ...KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2015!!!
MDADA YUPO KATIKA MAOMBI
Habari zenu jamani!!Leo ni siku ya kuusheherekea mwaka mpya 2015. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2015 UWE WENYE MAFANIKIO. NAMSHURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA YOTE.. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!! HERI SANA YA MWAKA MPYA 2015!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)