Thursday, January 1, 2015

SALAMU KUTOKA SONGEA/RUHUWIKO ...KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2015!!!

MDADA YUPO KATIKA MAOMBI 
Habari zenu jamani!!
Leo ni siku ya kuusheherekea mwaka mpya 2015. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tulioonyeshana.
Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2015 UWE WENYE MAFANIKIO. NAMSHURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA YOTE.. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!  HERI SANA YA MWAKA MPYA 2015!!!

5 comments:

Anonymous said...

Nakutakia mafanikio makubwa kwako na familia yako na blog ya Maisha na Mafanikio mafanikio makubwa katika mwaka 2015.By Salumu.

Mbele said...

Kila la heri kwa Mwaka Mpya hapa Ruhuwiko.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu Ahsante sana na namini hata wewe umeuanza mwaka kikakamavu...
Pro.Mbele. Hakika mwaka tumeupokea vizuri sana Ruhuwiko. Nawe naamini umeupokea vizuri.

johari abby said...

kila la heri

Yasinta Ngonyani said...

Johari Abby! Ahsante ..kheri nawe!