Wednesday, January 14, 2015

HII NI KAZI YA MIKONO YETU WENYEWE....UTAKULA ULICHOPANDA.....NYUMBANI SONGEA/RUHUWIKO!!!!

 Tumekuta ndizi tulizopanda zimekomaa na tumezila  hapa ni baadhi tu.....
 ...tuliendelea na mihogo pia nanasi/mananasi.. kazi ya mikono ya kapulya------hatukuishgia hapo
 ....tukayala na maembe maana huu mti upo ndani ya eneo letu yaani tunaumiliki:-)......
----bado tukaendelea na matunda ya  ambayo pia ni kazi ya mikono yetu.."passion"....tutaendelea na picha zaidi...zinakuja:-)

11 comments:

Mbele said...

Safi sana. Umenikumbusha Ruhuwiko, ambapo ni njiani kuelekea kwetu Mbinga, na ambapo miaka mitatu hivi iliyopita nilimtembelea dada yangu anayeishi hapo.

Yasinta Ngonyani said...

Pro.Mbele...nafurahi kama unakumbuka Ruhuwiko. Utakspoenda teba usikose kupitia hapa kwetu.

Rachel Siwa said...

Hongera sana Kadala

Kelkaf said...

Imekaa frex ....

emu-three said...

Hongera sana, kweli utavuna ulichopanda na utakula ulichovuna, vipi likizo inakwendaje Tupo pamoja

Penina Simon said...

duh hadi raha!

Yasinta Ngonyani said...

"Kadala" Rachel! Ahsante sana!

Kelkaf! Ahsante,,
emu-three! Ndugu wa mimi Ahsante kwa ulichosema na kuandika, Pamoja daima.

Mama Wane said...

Hongera dada kwa juhudi zako yaani hadi raha.Wanetu walifurahi sana naona.

Yasinta Ngonyani said...

Mama Wane!! Ahsante sana kwa pongezi.Yaani kama ulikuwepo walifurahi sana sana.

Unknown said...

Nilikuwa sijapitia ukurasa wako muda mrefu na leo namshukuru Mungu nimepata nafasi ya kupitia makala hadi za nyuma. Ndio maana unaona nakomenti kwenye makala za Januari lakini, yote hii ni kwa upendo tu na ufuatilizi.

Kiukweli, Yasinta, uko wa kipekee. Umeanikwa ( got exposure) lakini bado uko mnyenyekevu na unakumbuka na kupapenda nyumbani kama sijui kitu gani.

Namshukuru Mungu kukuweka kati yetu, na amini, najifunza mengi kutoka kwako na nathamini na kutamani ( sijui kama ni tafsiri sahihi ya admire) attitude yako in life.
Ubarikiwe.

KIPAPLI

Yasinta Ngonyani said...

Unknown au Kipapli! Ahsante kwa yote na karibu sana tena na tena!