Tuesday, January 27, 2015

JINSI KAPULYA ALIVYOINASA TASWIRA YA LILONDO....AKINA MAMA WAJASILIAMALI....

Hapa ni Lilondo, huwezi kupita hapa bila kusimama ni kijiji chenye ndizi nyingi sana kama unavyoona akina mama wajasiliamali wanavyochangamka wakati  basi la Super Feo  liliposimama. Kwa hiyo upitapo Lilondo usikose kusimama kununu ndizi... maana kuan kila aina uwezo wako tu..karanga pia. PAMOJA DAIMA!!

6 comments:

Mbele said...

Picha nzuri. Je, Lilondo ni wapi?

Yasinta Ngonyani said...

Prof. Mbele ahsante. Lilonfo ni kijiji kimoja kati ya Madaba na wino. Nahisi unapoenda nyumbani Mbinga/Litembo ni lazima unapita hapo

Mbele said...

Shukrani, Dada Yasenta. Ni kweli nimepita njia hii mara nyingi sana, kuanzia mwaka 1971, nilipoenda kuanza masomo Mkwawa High School. Ajabu tu ni kwamba nilikuwa sijui jina la kijiji hiki. Madaba na Wino nazifahamu vizuri tangu enzi hizo. Au labda Lilondo imezuka hivi karibuni?

Yasinta Ngonyani said...

Prof. Mbela ...hapana hiki ni kijiji cha zamani tu kwa jinsi nikumbukavyo na nijuavyo mimi yaani hapa mabasi hayakosi kusimama ni LAZIMA.

Mbele said...

Nashukuru kwa taarifa.

Unknown said...

Napapenda na tuna mradi wetu katika Kijiji hicho . Mradi wa kuwawezesha wazee na najisikia fahari (japo kwa unyenyekevu) kuhusiana na Kijiji na maeneo hayo kwa namna hiyo.