KAPULYA KIZIZINI PERAMIHO 2/1/2015
Nachukua nafasi hii kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda katika safari yetu na pia sasa tumerudi salama tena. Pia ahsanteni kwa sala zenu. Nilikuwa natamani kula nyama ya ngómbe nikaona ngoja nitembelea kizizini Peramiho kwa wale wanaotokea Songea wanajua ni wapi. Na wewe usiyejua ni njia ya kwenda Peramiho upande wa kushoto kama unatokea Songea.TUPO PAMOJA ....
5 comments:
Tunafurahi kukuona tena baaada ya kupotea zaidi ya siku saba. Usitusahau na sie nyama choma kwa kachumbari.By Salumu.
Nikuulize kitu Kadala, hivi uliondoka na picha gani na umerudi na picha gani kuhusu Peramiho? Nakuonea huruma Peramiho ya zamani sio ya sasa! Mengi yamebaki historia. Bustani na mashamba mazuri yote yamekufa, zizi linajikongoja tu, majengo waliyotuachia wamisionari yanaanguka, wale ma-father wa kizungu na mabruda wengi wameshakufa. Bila shaka ata Rafiki zako uliokuwa unacheza nao wapo sio kama ulivyowaacha. Maisha ni ajabu sana tunatamani enzi zetu zile zirudi tena!
Mdada ulivyomechisha vazi na mjengo sina hamu! Umefunika ile mbaya na karibu tena kwenye baridi baada ya kufaidi vinono vya nyumbani.
Nakupenda the ulivyo simple, hujikuzi, unajishusha hasa unapokuja huku nyumbani, Mungu akuzidishie huo moyo
Kaka Salum!Unajua kublog ni raha mimi sikuwa mtandaoni tangu tarehe 13/12 mwaka jana :-) ni ujanja tu...Ila usihofu nyama choma na kachumbali utapata.
Usiye na Jina! Kwa vile huwa sikai sana..lakini hata hivyo kuna mabadiliko yake...Ndiyo bustani na mashamba yamekufa na zizi linajikongoja. Ni mambo mengi kuhusu Peramiho yanapotea.
Mwalimu Mhango! haikuwa makusudi kumechisha:-) Ahsante nimerudi salama na baridi nimeipokea na mafuta yote yashakauka:-)
Dada P. Ahsante sana.
Post a Comment