Friday, April 5, 2013

NIMEKUMBUKA KWELI NYUMBANI LEO NIKAANZA KUSIKILIZA NGOMA ZETU ZA ASILI..HII NI NGOMA BETA YA WANGONI

NAWATAKIENI WOTE JIONI HII YA IJUMAA YA TAREHE 5/4 IWE NJEMA NA YENYE UPENDO,,,,

8 comments:

Mija Shija Sayi said...

Nimekumbuka kipindi cha Tumbuizo Asilia Redio Tanzania, sijui bado kipo au la?

Ijumaa njema kwa wote..

ray njau said...

Utamaduni asilia ni kioo cha jamii husika.

Yasinta Ngonyani said...

Ngoma hii ya beta inatokana ilianzia/asili yake ilikoanzia ni pale watu wanapotwanga hasa wawapo wawili michi inapotua kwenye kinu.....umewahi kuusikia wimbo huu wa beta kwa KINGONI..Wa mngwana veve,jana ubweli, lelu ubweli walikinda ndila, ubweli kunilola, ehe!...KISWAHILI ITAKUWA HIVI:- Mume wewe, jana ulikuja, leo tena unakuja umekuwa mtu wa njiani tu, umekuja kuniona, ehe!
Sasa hapo ndo weee utamu kweli...

Rachel Siwa said...

Pole KADALA...Kama nakuona hapo..baba aahh babahh..nikupenini..

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Umenikumbusha mganda. Pia nimemkumbaka Michael Katembo na tumbuizo lake asilia RTD wakati ule ikivuma kabla ya kupasuliwa na FM upuuzi zilizotamalaki. Laiti siku zingekuwa zinarudufiwa nadhani ningefanya hivyo. Najihisi kama niko nyumbani ingawa hapa niko ugenini.
By the way da Yacinta una habari zozote kuhusu Mwalimu Masangu wa Matondo mwana wa Nzuzulima? Maana naona ugani kwake kumejaa nyasi.
Otherwise nakutakia wikendi njema huku ukiburudika na vitu vya home.

Philipo Haule said...

Jamani nyumbani kwetu , jaman napamis Songea wapendwa wangu , Am so sad kwa kweli nawapenda wot mungu atulinde wapendwa , ndo naiona hii blog leo jaman......hebu nitajieni nyimbo zetu za asili kwanza