Tuesday, March 12, 2013

NAPENDA NGUO NDEFU MWENZENU..NA HII NI KAZI YA DADA SUBIRA WAHURE...

 Hili gauni limenivutia mpaka basi ..yaani ningependa nilimiliki kabisaaaa..ebu angalia lipo rahisi rahisi kweli lakini ni bonge la kitu ...mavazi ya heshima hayaa ...
Na hapa hii sketi imenimaliza kabisa ndefu, pana, rangi zake zinavutia yaani kama nipenzavyo...Nakutakia kazi njema sana dada Subira ...kwa kuona kazi zake nyingine inga hapa. NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA SANA WOTE.

6 comments:

sam mbogo said...

Yawezekana ukawa sahihi kwa ukipendacho hasa nguo kamaulivyo sema,wapenda nguo ndefu. swali je unapenda kwa ajili ya kupendeza au mradi umeipenda na umeivaa? mi nimependa hiyo sketi hasa rangi za kitambaa. kaka s

Interestedtips said...

kwakweli nguo nyingi za Subira huwa ni nzuri sana na za heshima, namkubali kwakweli

Shalo said...

Yani nguo nzuri sana nimezipenda sn

ray njau said...

Urembo Usioharibika
=======================
Kujiamini na kuridhika maishani hakutegemei kuwa na sura nzuri tu. “Furaha ya kweli hutoka moyoni,” aandika Judy Sargent, aliyekuwa akijinyima chakula awali. “Haitokani na uzito wa mwili.” Biblia inatoa mashauri zaidi. “Kujipamba kwenu,” asema Petro, “kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.”—1 Petro 3:4, Union Version.

Urembo usioharibika ambao Petro anazungumzia hupita sura yenye kuvutia kwa sababu unadumu na ni wenye thamani machoni pa Mungu. Karne nyingi zilizopita mfalme mwenye hekima alisema hivi: “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.”—Mithali 31:30.

Ijapokuwa sura nzuri inaweza kuvutia zaidi leo, bado watu wengi humheshimu mtu mwenye sifa za Kikristo. Mtume Paulo aliwahimiza Wakristo: “Mjivike wenyewe utu mpya, . . . shauku nyororo za huruma, fadhili, hali ya akili ya kujishusha chini, upole, na ustahimilivu.”—Wakolosai 3:10, 12.

Kwa kawaida mitindo haidumu. Hata tuioneje, twaweza kutumia mitindo ya kisasa kwa muda mfupi tu. Sifa yoyote nzuri tunayopata kwa sababu ya sura yetu inaweza kuharibika ikiwa hatuna utu mzuri. Kumbuka kwamba, “matunda ya roho”—kutia ndani sifa ya upendo, shangwe, amani, ustahimilivu, wema, na kujidhibiti—hayachakai kamwe.—Wagalatia 5:22, 23; 1 Timotheo 2:9, 10.

Hata hivyo, ni kweli kwamba, tunapaswa kuzingatia mavazi yetu. Aline, kutoka Ufaransa, akiri kwamba haikuwa rahisi kuwa na usawaziko kuhusu jambo hilo. “Nilipokuwa tineja,” asema, “nilipendezwa sana na mavazi. Nilitaka kufuatia mitindo ya kisasa kwa sababu ilinifanya nijiamini. Na ikiwa ningeweza kununua mavazi yenye jina la mbuni maarufu, nilifurahi hata zaidi.

“Lakini nilipokuwa mtu mzima,” Aline aendelea kusema, “nililazimika kujifunza kujitegemea kifedha, pia nikaanza kutumia wakati mwingi katika huduma ya Kikristo. Nilitambua kwamba ikiwa nilitaka kuishi kulingana na mapato yangu, singeweza kuendelea kuwa mtumwa wa mitindo. Nilianza kununua nguo zangu bei ziliposhuka na pia kwenye maduka ya bei rahisi. Niligundua kwamba bado ningeweza kuvalia vizuri—lakini kwa robo ya bei. Siri ni kununua mavazi yanayokufaa, mazuri, yanayopatana vizuri na mavazi uliyo nayo tayari, na ambayo hayatapitwa na wakati upesi. Badala ya kuruhusu mitindo iniamulie ninachopaswa kununua, sasa mimi hujaribu kuamua kinachonifaa. Sisemi kwamba sijali mavazi ninayovalia. Lakini utu wangu hautegemei tu sura yangu.”

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! napenda nguo ndefu kwa vile nimelelewa hivyo fupi napenda ila zipite magoti...

Ester ! ni kweli kabisa maana kila ukiingia unakutana na jipya na ni kazi nzuri sana nampongeza.

Shalo! ni kweli zinapendeza mno.

Kaka Ray! ni kweli urembo usioharibikia ...ahsante kwa neno.

Subira Wahure said...

asante sana dada esther ulaya...big support kwangu.mungu akubariki