Wednesday, March 6, 2013

LEO EBU TUMSIKILIZE HUYU KAKA BINAFSI NIMEPENDA SANA MAZUNGUMZO YAKE ...NA DA SALAMA...EBU SIKILIZA UKIPATA MUDA

Nimependa sana mazungumzo haya ..nawatakieni wote JUMATANO NJEMA SANA....

10 comments:

Anonymous said...

Ni kweli Yasinta ameongea mambo mazuri. Anajiamini sana kwani wengi wakiishi nje kama ulaya nk. wanawafanya wazungu ni miungu watu. Mzungu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule. Au dada Yasinta unasemaje? Tunaomba nawe utupe uzoefu wako wa kuishi na wazungu huku sweden, na unapambana na changamoto zipi? sehemu mbalimbali iwe kazini, na kwingineko. Na pia kuishi na mume mzungu kuna changamoto zozote? Na wanao wanakuchukuliaje? Mana kuna sehemu nilisoma kuwa watoto wanaochanganyika na weusi huwa wanadharau mzazi amabye ni mweusi, je hiyo ni kweli? au ni jinsi utakavyomlea?

Yasinta Ngonyani said...

Kwa uzoefu wangu kwa kweli sijawahi kufikiria hata siku moja kama naishi na mzungu au au wanangu ni mchanganyiko na sidhani kama wao pia wanajiona kama ni mchanganyiko au wana mama ambaye ni mwafrika. Hata kazini kwangu hakuna anayeniona kama mimi ni tofauti na wao ...labda nina bahati sijui ...ila kama alivyosema Mad Ice mzungu ni mtu tu kama mimi ni rangi tu, halafu kitu kingine ambacho rafiki zangu wengi wanajua ni kwamba SIPENDI KABISA KUITWA MAMA MZUNGU au TU KUMWITA MTU MZUNGU SIPENDI KABISA KABISA....

Anonymous said...

Asante Yasinta kwa maelezo yako. Hiyo ni bahati yako, ingawaje najua kuna sehemu utakuwa lazima umekutana na vitu fulani labda hupendi kuongelea zaidi. Kwa mfano kwenye mabasi wazungu wengi hawapendi kukaa na mweusi, kama kaka alivyoongelea atajihimu asimame ili mradi asikae na mweusi hii nimeiona ujerumani pia. Hata hapa Sweden ila sio wote ingawaje hiyo kasumba ipo. Basi unajikalia kwenye basi kwenye siti mbili kwa raha zako. Labda Yasinta umeishi nao miaka mingi na sasa umazoea kila kitu ni sawa kwako mana nafahamu lazima ungetuelezea vitu fulani, siamini kama kila kitu kiko smooth kwako kama ulivyosema! mana wapo wasiopenda kuelezea hayo hata kama anayaona wazi wazi. Jioni njema.

Anonymous said...

Asante Yasinta kwa maelezo yako. Hiyo ni bahati yako, ingawaje najua kuna sehemu utakuwa lazima umekutana na vitu fulani labda hupendi kuongelea zaidi. Kwa mfano kwenye mabasi wazungu wengi hawapendi kukaa na mweusi, kama kaka alivyoongelea atajihimu asimame ili mradi asikae na mweusi hii nimeiona ujerumani pia. Hata hapa Sweden ila sio wote ingawaje hiyo kasumba ipo. Basi unajikalia kwenye basi kwenye siti mbili kwa raha zako. Labda Yasinta umeishi nao miaka mingi na sasa umazoea kila kitu ni sawa kwako mana nafahamu lazima ungetuelezea vitu fulani, siamini kama kila kitu kiko smooth kwako kama ulivyosema! mana wapo wasiopenda kuelezea hayo hata kama anayaona wazi wazi. Jioni njema.

sam mbogo said...

Dogo amesema kutokana na mtazamo wake ju ya jamii zetu zinavyo wachukulia au kusema ju ya WAZUNGU(samahani dada Yasinta). fikra ambazo sisi weusi/waafrika kwa mtazamo wa baadhi mtu anapo owa huwa anavitu vinavyo mvutia au vinavyo mpekea kuolewa au kuoa .yawezekana ika wa ni,sura nzuri ya kuvutia nahapa ni wote mwanamke/mwanaume.pia yawezekani ni kwa sababu ya mali,pia vivyo hivyo kwa mwanamume/mwanamke nk.ila kuna wengine hayo niliyo yasema kwao hayana tija. ndomaana ukija kwa upande wa swala la kuoa au kuolewa na MUZUNGU(Yasinta kumradhi/zi) kuna baadhi kweli wanakuwa na mitazamo ya kuchuma/kutafuta maisha,na wengine inakuwa nizaidi ya hiyo ni kumpata mwenza waweze kutengeneza familia kwa pamoja. ndiyo maana utakuta ndoa nyingi kati ya mswahili na mweupe/ulaya kama lengo la mmoja wapo ilikuwa ni kutafuta njia ya kutokea ,huwa hazikaai,na pia kwa shemeji zangu weupe walio owa dada zetu kama haja ilikuwa kuonja mswahili huwa ndowa hizo hazidumu.pia hata zile ndoa ambazo kwa hakika nikwa nia njema ya kujenga familia nazo zina mikikimikik yake.ila niseme kwamba ndoa mchanganyiko kama hizi mswahili na mweupe ni ngumu zinahitaji busara sana,kidogo naona za nyumbani zina afadhali!! kwa mtazamo wangu mimi kama mwana ume.kaka s

Anonymous said...

Kweli kaka Sam Mbogo umesema ukweli na kuweka wazi kabisa. Kwa kweli yote uliyoongelea ni kweli tupu. Ndoa za mchanganyiko na weusi nyingi mno ni utata na matatizo matupu. Wachache saana zinadumu na kuwa nzuri: Dada Yasinta ameamua kufumbia macho hilo, Hivi hata huyo kaka angeamua kusema uongo na kutotaja yanamkuta huko Finland ladba tungeweza amini hivyo ila kama umeishakaa nje kwa kweli hakuna cha siri kila kitu kinajulikana na labda kwa wale ambao hawajaishi nje au kutoka nje na kujionea maisha ya huku ni rahisi kumdanganya kuwa unajua hakuna tatizo lolote lile! La hasha sio kweli! hata mashuleni ni tabu tupu hata kwa watoto machotara wa waafrica na wazungu, kwani wazungu huwa wanawaona sio wazungu pure, na hivyo kuwanyanyapaa wakati mwingine! Hizi sio siri mie nimeona kwa macho yangu na sio simulizi na ni nchi nyingi tu! Hivyo hayo mambo yapo. Dada Yasinta anaona uzito kuelezea na wakati huo ameipenda mada ya salama na huyo kaka ila mwenzio ameelezea ukweli wote ulivyo. Swala sio kitwa mama Mzungu, na wala kumwita mumeo mzungu hapana, tunazungumzia changamoto, vikwazo na kubaguliwa wakati mwingine kama ilivyo ndani ya mabasi. Nakuuliza Yasinta tangu uje Sweden hujaya-experience ya kuachiwa kiti kwenye mabasi? Mana hii ukifika tu ulaya utaiona hata bila kuambiwa! Au wewe kwa kuwa umeolewa Sweden unaogopa kumuudhi shemeji yetu?

ray njau said...

KUJITAYARISHIA NDOA YENYE MAFANIKIO
==================================
Ikiwa unafikiria kwa uzito kufunga ndoa, unapaswa kujiuliza, ‘Niko tayari kweli?’ Jibu la swali hilo halitegemei tu maoni yako kuhusu upendo, ngono, kuwa na mwenzi, au kulea watoto. Badala yake, kuna miradi hususa ambayo kila mwanamume au mwanamke anayetaka kufunga ndoa anapaswa kufikiria.

Mwanamume anayetafuta mke anapaswa kufikiria kwa uzito kanuni hii: “Tayarisha kazi yako huko nje, uifanye tayari kwa ajili yako shambani. Kisha ujenge nyumba yako.” (Methali 24:27) Andiko hilo linamaanisha nini? Katika siku hizo, mwanamume alipotaka ‘kujenga nyumba yake’ au kuwa na familia kwa kufunga ndoa, alipaswa kujiuliza, ‘Ninaweza kumtunza na kumtegemeza mke na watoto wowote tunaoweza kuwapata baadaye?’ Kwanza alipaswa kufanya kazi, atunze mashamba au mazao yake. Kanuni hiyohiyo inatumika leo. Mwanamume anayetaka kuoa anapaswa kujitayarisha kwa ajili ya majukumu ya ndoa. Maadamu afya yake inamruhusu, ana wajibu wa kufanya kazi. Neno la Mungu linaonyesha kwamba mtu ambaye haandalii familia yake mahitaji ya kimwili, kihisia, na kiroho ni mbaya kuliko asiye na imani!—1 Timotheo 5:8.

Vivyo hivyo, mwanamke anayeamua kuolewa anakubali kuchukua majukumu mazito. Biblia inataja stadi na sifa ambazo mke anahitaji anapomsaidia mume wake na anapoitunza familia yake. (Methali 31:10-31) Wanaume na wanawake wanaokimbilia maisha ya ndoa bila kuwa tayari kwa ajili ya majukumu yanayohusika ni wenye ubinafsi, nao hawafikirii wanachoweza kuchangia katika ndoa. Zaidi ya yote, wale wanaofikiria kufunga ndoa wanahitaji kujitayarisha kiroho.
Kujitayarisha kwa ajili ya ndoa kunatia ndani kufikiria kwa uzito majukumu ambayo Mungu amempa mume na mke. Mwanamume anapaswa kujua maana ya kuwa kichwa katika familia ya Kikristo. Jukumu hilo si leseni ya kupiga ubwana. Badala yake, lazima amwige Yesu katika kuutumia ukichwa. (Waefeso 5:23) Vivyo hivyo, mwanamke Mkristo anapaswa kuelewa jukumu lake lenye heshima akiwa mke. Je, yuko tayari kujitiisha chini ya “sheria ya mume wake”? (Waroma 7:2) Tayari yuko chini ya sheria ya Yehova na ya Kristo. (Wagalatia 6:2) Mamlaka ya mume wake katika familia ni sheria nyingine. Je, anaweza kuunga mkono na kutii mamlaka ya mwanamume asiye mkamilifu? Ikiwa hayuko tayari kufanya hivyo, afadhali asiolewe.

Zaidi ya hilo, kila mmoja anapaswa kuwa tayari kutosheleza mahitaji ya pekee ya mwenzi wake wa ndoa. (Wafilipi 2:4) Paulo aliandika: “Kila mtu mmoja-mmoja kati yenu na ampende hivyo mke wake kama vile anavyojipenda mwenyewe; kwa upande mwingine, mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.” Akiongozwa na roho ya Mungu, Paulo alitambua kwamba mwanamume ana uhitaji wa pekee wa kuhisi kwamba mke wake anamheshimu sana. Naye mke ana uhitaji wa pekee wa kuhisi kwamba mume wake anampenda.—Waefeso 5:21-33.

Kwa hiyo basi, uchumba si kipindi cha kujifurahisha tu. Ni wakati wa mwanamume na mwanamke kujifunza kutendeana inavyofaa na kuona ikiwa wanafaana kwa ajili ya ndoa. Pia ni wakati wa kuonyesha sifa ya kujizuia! Kupita mipaka katika kuonyeshana mahaba kunaweza kuwa kishawishi chenye nguvu sana, kwa kuwa kila mmoja anavutiwa na mwenzake. Hata hivyo, wale wanaopendana kikweli wataepuka matendo yoyote yanayoweza kuharibu uhusiano wa mpendwa wao pamoja na Mungu. (1 Wathesalonike 4:6) Kwa hiyo, ikiwa una uchumba, onyesha sifa ya kujizuia; sifa hiyo inaweza kukusaidia katika maisha yako yote, iwe utafunga ndoa au hapana.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka sam! umesema ukweli kabisa ahsante kwa mchango wako...
Usiye na jina...ntakujibu swali lako ..kuachiwa siti kwenye basi imetokea mtu anaingia na kuona wewe umekaa na anachukua siti nyingine au anaamua kusimama sijui ndo kuogopa kuupata weusi?..Lakini hata mie imetokea wakati mwingine ila sio kusimama wakati siti zipo hapana ...kuhusu watoto kunyanyaswa hilo kwa kweli kwa hawa wetu sijawahi kusikia..sio kwamba nakataa halipo lipo ...nategemea umenielewa

Anonymous said...

Nashukuru sana yasinta. Unaonekana kuwa na malezi bora kwa wanao, na jinsi invyoonekana mume wako anakupenda sana sana na hivyo una familia nzuuri sana yenye furaha na amani. Au nimekosea? Samahani sijawahi kuishi na nawewe wala familia yako ila jinsi inavyoonesha hapa kwenye blog una-enjoy sana maisha yako hapo Sweden. Na kwa hivyo nazidi kukutakia maisha mazuri ya ndoa yako pamoja na familia yako kwa ujumla. Siri kubwa nimejifunza kwako unaonekana uko very strictly na pia ni mcheshi na hivyo umeweza kubalance vitu vingí. Mana pia tunafahamu malezi ya watoto nje ni magumu sana, ila nakuaminia sana Yasinta. Tunza huo ushuhuda. Mungu akubariki na familia yako.

Yasinta Ngonyani said...

Duh! usiye na jina wa 10.00pm ..naona niseme tu AHSANTE sana.nanukuu:- Siri kubwa nimejifunza kwako unaonekana uko very strictly na pia ni mcheshi na hivyo umeweza kubalance vitu vingí. Mana pia tunafahamu malezi ya watoto nje ni magumu sana, ila nakuaminia sana Yasinta. Tunza huo ushuhuda. Mungu akubariki na familia yako. mwisho wa kunukuu. maisha ni kujifunza ..