Monday, October 1, 2012

NIMEUTAMANI KWELI MLO HUU UNGEKUWA MLO WANGU WA JIONI HII!!!

ila nitashindwa kwa vile kitu kikubwa zaidi ni kwamba sina unga ....mwisho nimebaki kumezea mate tu..hasa huyo samaki wewe acha tu...picha toka http://barakachibiriti.blogspot.se.
Nawatakieni kila la kheri au sijui jioni,mchana, asubuhi au usiku mwema.

6 comments:

ray njau said...

Hii picha ya thamaki ni pouwa thana kwa mutani wangu Kitururu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray unaweza kufafanua kwanini ni kwa mutani wako Kitururu?

ray njau said...

Watani zangu wapare wana uwezo wa kula ugali kwa picha ya samaki.

Yasinta Ngonyani said...

oh! kumbe hili ni jipya kwangu..basi tusibiri tuone atasema nini kama atatokea....

Anonymous said...

kumbe ulikuwa hujui maana hawa jamaa wa upareni ndivyo walivyo maana ni bahiri kupitiliza kuna mmoja hapa kazini bandari yeye ikifika saa ya kula anaenda kantini anaangalia vyakula vyote halafu anakunywa maji tu anaondoka anasema kaisha shiba.....mhhh

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina! Hakika sikujua kumbe ndivyo walivyo kaaaazi kwelikweli..Kisa na mkasa nini?