Wednesday, December 21, 2011

SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!

Habari zenu jamani!!
Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2011 na kuingia katika mwaka mpya 2012. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tunaoonyeshana. Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2012 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA LISILOWEZEKANA/KISICHOWEZEKANA. NAONA TUTAENDELEA MWAKANI NA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO YA MADA, MATUKIO MBALIMBALI PIA PICHA.. bila ninyi kipengele hiki hakingeweza kuwa. MBARIKIWE WOTE MTAKAOPITA KATIKA BLOG HII NA NYINGINE ZOTE. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!

10 comments:

Rachel Siwa said...

Ahsante sana da'Yasinta,Mungu awe nawe na familia yako pia,Mungu azidi kukutumia,Baraka na Amani vitawale nyumbani mwako.

Unknown said...

Nawe pia dada yangu. Mungu akubariki na azidi kukuzidishia hekima na busara ili wasomaji wako tuzidi kuneemeka zaidi. Ahsante kwa yote..

Mija Shija Sayi said...

Yaani hapo unavyoonekana mtulivu...

Asante kwa ujumbe na ubarikiwe sana dada.

Issack che Jiah said...

Nasema asante kwa wema wako kwaana fadhili zakoo zidumu,milele na milele amina.
Tunakutakia nasi amanini na upendo utawale ndani ya nyumba yenu tunashukuru kwa kutubariki mwaka ujao mungu atujaze baraka na amani kwani bila amani upendo haupo na bila upendo hakuna amani tufikishie salamu kwa mlinzi mkuu wa nyumba yako si yule malaika bali yule aliyetendeka mwili mmoja nawewe Amina
Che Jiah

ray njau said...

Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Katika maisha ya mwandamu yapo mambo matatu muhimu sana katika harakati za maisha na mafanikio.
1.SALAMU
2.SAMAHANI
3.SUBIRA
4.SHUKRANI
Kupitia utulivu wake pichani amekuja na salamu pamoja na shukrani kwa wadau wake wote.Yeye ni binti na mama yake alipongezwa sana siku alipompamta binti huyu ambaye kwa sasa ni mama wa familia huko ughaibuni lakini utadhani yupo Ruhuwiko.Hapa nazipokea shukrani na salamu zake kwa moyo uliosheheni upendo kabisa.Kwa wadau wote nawaomba iwapo inawezekana kuwe na mabadiliko kidogo katika kuogopa kukosoana na kupeana mashauri pale inapowezekana.Hakuna binadamu mkamilifu asijikwaa katika makosa na kuomba msamaha.Siku zote tuwe hodari katika uchambuzi wa mada na tusiishie tu na pongezi.Daima tusiogopane bali tupendane.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana wote kwa michango yenu na kutochoka kupita hapa kila mara. Mija unadhani mie sio mtulivu?

Yasinta Ngonyani said...

Rachel ...tupo pamoja ndugu yangu.

Kaka Mrope!Ahsante sana Pamoja daima.

Mija! kwani mimi si mtulivu? Ahsante na wewe kwa kusoma ujumbe ubarikiwe nawe dadangu.

Kaka Che Jiah! Upendo huo utawala katika nyumba yako pia nami nashukuru kwa kutochoka kupita hapa.

Kaka Ray! Nawe ahsante na ujumbe wako wenye kubeba ujumbe murwa ahsante sana. nukuu "Siku zote tuwe hodari katika uchambuzi wa mada na tusiishie tu na pongezi.Daima tusiogopane bali tupendane" mwisho wa nukuu.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta ushaona wapi Kapulya akawa mtulivu?

nakutakia kila la heri na familia yako.

Yasinta Ngonyani said...

Oh! kumbe kuwakumbe si utulivu aisee.....Mija Ahsante sana kwa wasifu huu.

Wilbard said...

Hongera! Nafurahi kuona vijana tuna,mlengwa chanya wa maisha. Kwani vijana wengi wamebaki kulalamikia serikali zao. Tusaidiane kutoa ELIMU kupitia www.wilguy-jibebe.blogspot.com ili kuwa na jamii yenye utulivu