Monday, March 28, 2011

Marafiki waliokuja kutufariji siku ya ijumaa!!

Hapa ni marafiki wawaili waliokuja kutufariji siku ya ijumaa wote manjua mimi ni hapo katikati na kulia kwangu ni Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo na kuchoto kwangu ni Dada Asta kutoka Ivory Coast. Hapo walinilazimisha kunywa chai na unywaji wangu wote wa chai hapo nilikuwa hoi kabisa. Wote tunawashukuru kwa kutufariji maana wanaonywsha ushirikiana mzuri. Na jana Jumapili alikuaja Dada mmoja yeye anatokea Njombe ila samahani nilitingwa kuchukua picha yake. Na picha hii hapo juu mpigaji si mwingine tena ni Erik..... nitarudi mtandaoni hivi karibuni nitengamae kwanza. MNAPENDWA WOTE...

17 comments:

Unknown said...

Mungu azidi kuwafariji.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Pamoja sana Da Yasinta!

Mungu akupe uvumilivu!

Anonymous said...

Huyo katikati ndo,watu walikuta manyoya tu kukumwenyewe kishaliwa! doh(cheka kiduchi bas!) .pole sana,mshukuru mungu unawatu hata wakuku ambia kunywa chai.mungu mkubwa.
kaka s.

Mija Shija Sayi said...

@Kaka S, msanii ni msanii tu huachi visa? ninaamini hata da Yasinta pamoja na majonzi amecheka kidogo..

Yasinta mungu azidi kuwa nanyi, na hao kina dada wabarikiwe sana.

Pamoja daima.

Baraka Chibiriti said...

Tunawashukuru sana kwa kuja kukufariji katika wakati huu mgumu, hata sisi ingelikuwa karibu tungekuja kwa wingi sana, ila kama unavyojua umbali pia majukumu ya watu, huku Ulaya hawakupi ruhusa kama unavyojua.

Pole zangu sana tena kwako Dada Yasinta.

Rachel Siwa said...

Mungu azidi kukupa nguvu!wabarikiwe wageni wetu pia nasi tupo pamoja nawe!

Anonymous said...

Da mija,una juwa kwenye misiba huwa kunautani wa kimakabila/kikabila.sasa kwa yeye mpendwa mtukufu ,ndugu, kingunge Yasinta inakuwa ngumu kuwapata watu kama sisi watanizake.inasaidia sana kupunguza machungu,natamani ningekuwapo nyumbani kwake ningefanya shughuli zote kama mtani ,ila ungo wangu na kikombe kutoka kwa babu wa loliondo vina matatizo kidogo hivyo siwezi kuruka mpaka huko uliko Yasinta,na nguvu ya kikombe nayo muhimu niko kwenye foleni nikinywa tu nakamata ungo,utaniona sebuleni.kaka s.

Mwanasosholojia said...

Inapendeza marafiki kufarijiana.Tunawashukuru kwa kutuwakilisha physically...siku zote tupo nanyi mentally!

Upepo Mwanana said...

Pole sana Dada Yasinta kwa msiba mkubwa.
Naungana nawe katika majonzi na kukuombea kwa rehma za mwenyezi Mungu akupe nguvu na kuweza kushinda vita hii ya masikitiko.

MissPosh said...

pole sana dada yasinta may the comfort of god be with you.

emu-three said...

Mungu akujaze ujasiri wa subira, kwani yote ni mapenzi ya muumba

Anonymous said...

Ok! most welcome.there's time of sorrowful and time of joyful", we welcome them once more the time of joyful!but their presence is a challenge to us. Africa is One.

Kind regards Yasinta( Mtani)

Flora Wanna said...

pole dada! msiba ukikukuta mbali huwa unauma sana. pole mungu akutie nguvu.

Penina Simon said...

Mungu awabariki hao wadada kwa moyo wa upendo na umoja.

Yasinta Ngonyani said...

Kuwa ugenini; inapokuja dhida kama hii hapo ndipo utapaotamani uwe na mabawa na uruke. Lakini dada zangu hao Mariana na Asta ni kweli akina dada wa kweli tunashirikiana sana kwa raha na shida. Nawashukuru nao pia wanawashukuruni ninyi wote kwa kuwa nasi. Mbaribiwe sana.

Anonymous said...

Blog yako dada nzuri hongera sana.
Nami pia ni mwanablog kama wewe,ombi langu kwako naomba link hapo globuni kwako blog yangu hii: http://allyshams.blogspot.com/
Natumaini utafanya hivyo.Nakutakia kila la heri.Mungu akubariki,
asante.
Ally

emuthree said...

Tunawapa pole wafiwa, na tunamuombe mwenyezimungu aiweke mahali pema peponi roho ya mpendwa wetu huyo. Na Pole sana ndugu wangu,...yote ni mapenzi ya Mungu!