Monday, March 7, 2011

KUADIMIKA KWANGU NI KWASABABU HII!!

Habari, Hej, Monili, Kamwene, mwaukabwanji, hallo,!hola! nakadhalika. Nilikuwa sipo hewani karibia wiki sasa napenda kuwaomba radhi wasomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kuadimika kihivyo. Ni kwamba hapo mkoni petu kulikuwa na likizo ya wiki moja (Sportlov) nami nikaona ni vema nami niwe na familia.
SASA NIMERUDI NIPO NANYI TENA. KUSEMA KWELI NIMEWAMISS SANA NDUGU ZANGUNI:-) OH! MIJA na EDNA AHSANTENI SANA KWA KUULIZA NA SASA NIPOOOOO!!!

14 comments:

John Mwaipopo said...

interpol nilishawapa kazi ya kukutafuta. ngoja niwapigie kuwa umejisalimisha.

ha!ha!ha! nadhani ulikuwa na wakati muruwa na familia yako. karibu 'teni'!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka John ni furaha kusikia kuwa ulikuwa mpaka unataka kunitangaza huko. Ni kweli nilikuwa na wakati muruwa kabisa na familia. Ahsante!

Simon Kitururu said...

Bonge la PICHA hilo Yasinta!

Na karibu tena!

Fita Lutonja said...

Waoo! asante kwa kupatika kwenye blogu nimefurahi sana, na karibu sana. Japo tulikuwa tunawasiliana kwa simu lakini nimefarijika kuona umerudi kwenye chakula chetu cha kila siku. Asante sana bila shaka kaka Mwaipopo atakuwa amefarijika sana kwani interpol atawaambia kusitisha kazi aliyowapa

emu-three said...

Karibu tena dada yetu, tulikumisi sana, na kurejea kwako ni faraja kwetu. Tunataraji mengi kuhusiana na likizo hiyo fupi, usitubanie, ...lol
TUPO PAMOJA, KARIBU SANA TUENDELEZE MISHA YENYE KULETA MAFANIKIO!

EDNA said...

Karibu tena tulikumisooo ile mbaya.

PASSION4FASHION.TZ said...

Nimeipenda sana hiyo picha.xx

Rachel Siwa said...

Kariribu nyumbani da Yasinta!!!najua utakuwa umekusanya mengi ya kutushirikisha!!!!!

Fadhy Mtanga said...

nami nilikumiss sana. shukrani kwa kurejea salama.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kuona ukipotea kidogo tu ndugu zangu wanakutafuta. Ahsanteni sana na karibuni sana hapa kibarazani tena na tena. Upendo Daima:-)

Mija Shija Sayi said...

Mmh! Wenzetu mna baridi! Tumefurahi umerudi tena katika familia yako ya upande wa pili.

Yasinta unakumbuka lile swali langu? Wakina kamila wamekuwa sasa jamani..hebu ona mlivyopwaya katika hiyo picha..lol!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Wala huitaji kuomba radhi. Maana yake sisi wenzako mtandanoni ni Nambari 1, lakini familia yako ni Nambari NUSU (kama ipo lakini).

Sisi tunakufurahia unaporudi.

Watoto wako ni wazuri. Ebu wasogeze kidogo siku nyingine (au unaogopa siku moja watakulaumu umeonyesha picha zao bila ruhusa? Hata hapo ni ukweli mtupu!)


KARIBU SANA!

Zaidi nawakaribisha watoto wako nawe pia (bila kuwasahau wanablogu wenzangu hasaa wale wanaochangia kwenye blogu yako) kujifunza Kizulu http://ndimiafrika.blogspot.com/ (baadaye nitatoa hata mafunzo ya lugha ya Kikaburu---Afrikaans).


Kizulu na Kikaburu (KiAfrikaans) ndizo lugha mbili za kienyeji zilizovuma Afrika Kusini. Ukiongea moja yake, huwezi kabisa ukachomwa moto bure na wale wenye ugonjwa wa XENOPHOBIA nchini mwetu!

Salehe Msanda said...

Poa
Kila la kheri
Tuko pamoja
Njombe,Ruvuma ni mvua kwa saana.

kazi njema.