Friday, March 11, 2011

MAISHA/MILA,UTAMADUNI NA DESTURI:- SIKU YANGU ILIVYAKUWA LEO....MAZISHI!!!

Sijui nianzia wapi??
Ok ni hivi:- Jana Alhamisi nilikuwa kazini, na baada ya kazi kama kawaida ya watu wote huwa wana hangaika na mihangaiko au kuridi nyumbani na kupumzika. Kwa hiyo nami nilifanya hivyo jana nilikuwa na mihangaiko yangu na baadaye nikarudi nyumbani. Ile kuingia tu ndani nikakumbana na mlio wa simu, kuangalia sioni jina yaani limefichwa, hata hivyo sikusita nikapokea.

Oh! Kumbe wewe Mariana, ndiyo mimi Yasinta, hali yako? Salama tu......tukaendelea maneno mawili matatu...Oh, nilisahau Mariana ni rafiki yangu anatoka Angola. Basi pale tukawa tunapeana habari za hapa na pale na mara akaniambia kuwa rafiki yetu mwingine kutoka Serbien kafiwa na mamamkwe wake na mazishi ni kesho yaani leo.

Hapo nikawa hoi, ingwa huyo mama mkwe wa rafiki yetu Saida sijawahi kumwona hata siku moja. Nikashikwa na uchungu sana. Kwa hiyo nikakata shauri kwenda kwenye mazishi yake ambayo yalikuwa leo. Mamamkwe wa Saida anaitwa Maria amefariki akiwa na miaka 82.

Tulikuwa na misa na baadaye tukaunganika na kumsindikiza mamamkwe Maria kwa safari yake ya mwisho. Kulikuwa na watu 23 na Padre 24. Nasikitika sana kuwa sijaweza kupiga picha nilisahau kamera yangu nyumbani. Mamamkwe Maria na Ustarehe kwa Amani Peponi Amina!!

6 comments:

Simon Kitururu said...

Kwa Sweden mlikuwa wengi maana watu 24 si mchezo kwenye nchi hizi kuwapata hata kutoka kwa ndugu kutokana na staili ya maisha waishio!


R.I.P Marehemu tutakutana hapo baadaye Mungu akipenda!

John Mwaipopo said...

je waliofanikiwa kudondosha machozi walikuwa wangapi? huku unyakyusani watu huporomosha mchozi hata kama uhusiano ni wa kuunga-unga kwa gundi. ukiwauliza eti marehemu amemkumbusha marehemu wake aliyetangualia miaka kibao nyuma.

chib said...

Makwetu wakija watu 24, basi ujue kuna jambo, wazushi watasema nyie ni wachawi tu, maana hata wauaji huzikwa na watu wengi japo huwa hawaombewi ibada.

Mija Shija Sayi said...

RIP Maria.

Yasinta Ngonyani said...

Simon! Ni kweli kabisa

Kusema kweli kaka Mwaipopo wote kwani tulikuwa wahamiaji tu unajua:-(

Najua Chib! lakini hapo kwanza hao walikuwa wengi sana tena mno.

Mija ni kweli mama Maria apumzike kwa amani peponi. Amina . Ahsanteni wote jamni.

Sara Chitunda said...

Pole kwa msiba wa mamamkwe wa rafiki yako Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi "Bwana alitoa na Bwana ametwaa" jina la Bwana libalikiwe amina.