Tuesday, March 22, 2011

MICHEZO YETU!!


Netiboli....
Leo nimeamka na mawazo yangu yamefika hadi Lundo pia Kingoli wakati nasoma shule ya msingi. Nilikuwa mchezaji mzuri sana wa netiboli tena nilikuwa mfungaji magoli yaani mchezo huu ni raha kweli. Najiuliza sijui bado unachezwa mashuleni bado au?

11 comments:

Mwanasosholojia said...

Da' Yasinta, bado inachezwa ingawa si kwa hamasa kama mliyokuwa nayo zamani!

Yasinta Ngonyani said...

Nafurahi kusikia hilo maana siku hizi naona kama hata mchakamchaka unaanza kufa. Halafu kaka M. Karibu tena maana ulipotea kidogo nilikuwa mbioni kupeleka tangazo sehemu inayohusika:-)

EDNA said...

Nafikiri bado wanacheza.

Simon Kitururu said...

Duh! Mchezo huu unanikumbusha ujana pale MOROGORO uwanja wa Jamhuri - kwa maana mie na washikaji tulikuwa tunamchezo wakwenda kuangalia ingawa madhumuni na kilichokuwa kinatupeleka ilikuwa ni wavaavyo wacheza netiboli kuliko mchezo wenyewe .

Nahisi unaweza kuhisi tulichokuwa tunafurahia kama wavulana tulio balehe tu ni nafasi ya kuona wadada wenye bomba za paja katika vimini wakiruka na kutusaidia kuona zaidi ya magoti .

Safari ya ukuaji ni ndefu kwa mtoto wa kiume jamani!:-(

Rachel Siwa said...

hahhaa @kaka Kitururu kweli ilikuwa ndefu,tunakuombea ufike salama au umeshafika salama,

nami sinauhakika kama inachezwa basi si ya ushindani kama zamani!.

Mwanasosholojia said...

Ni kweli da' Yasinta, siku hizi mchakamchaka umebaki zaidi kwa shule za jeshi, nashukuru kunikaribisha, upotevu wangu una mambo mengi lakini sasa nimeanza kuonekana pasi shaka

Anonymous said...

Sasa Yasinta hata habali ya watanzania wenzetu wanamziki wa taarab wakundi la five star waliopatwa na umauti!! huweki hapa kabisaaa wewe ni michezo tuuu Tanzania kwenu ni vilio vyawanamziki waliopoteza maisha dada,,hata rais vifo hivyo vimemgusa na ameshatoa salaam za rambirambi.Usikwazike ni mdau wa blog yako,pia hata mimi nimeguswa mnoo na ajali hii!!!!!

Simon Kitururu said...

@Rachel aka Swahili na Waswahili: Kwani unafikiri safari ya kukua inaisha basi?

Nahisi kwa yeypte aaminikaye kakua ukimsachi vizuri utakuta tu kuna mambo yake aliyokuwa nayo tokea utotoni ambayo kunaawezaye kuyaita YAKITOTO.:-(

Yasinta Ngonyani said...

Edna unaonaje tukianzisha timu yetu?...

Simon wewe bado hujatulia tulia kabisa:-)

Rachel itakuwa bahati mbaya kama umekufa...ngoja tuanzishe timu yetu au?

Kaka M! Nimesikitika kusikia mchakamchaka unafifia mashuleni ...
Usiye na jina! wakati ulikuwa bado..

Simon! nakubalina nawe ni kweli kukua hakuishi...Ila Simon umenichekesha kwenda kuangalia netiboli kumbe una yako..kaazi kwelikweliiii:-)

Simon Kitururu said...

@Yasinta:
Ukuaji hauishi na labda UKUAJI hauna kutulia kwakuwa kuna sababu za KIBAOLOJIA pia.:-(

Na kila umri una mambo yake na usishangae kuwa kuna umri ukubwani wauitao wa MIDLIFE CRISS ambao unaweza kukuta KUBWA zima hubadilika -na yasemekana katika kipindi hicho ndio dume kibao hutafuta dogo dogo saizi yao na kuachana na kitu cha zamani ambacho hakina ladha tena maishani.


Na kwa kuwa wewe una mtoto wa kiume ,...
... utastukia ni jinsi gani anabadilika kuanzia enzi za kutojali kucheza na wasichana,...
... enzi za kuchukia kucheza na wasichana na ambaye nafikiri kashafikia umri wakuanza kuwa na interest za watu wa jinsia nyingine.

- ukimchunguza utastukia .

Na una MME ambaye hata ukiangalia picha zake za zamani na kusikia aliyofanya zamani na mpaka ulivyokutananaye ,...na mpaka sasa hivi ,..
...utastukia kuna yaliyobadilika.

Kwa hiyo mambo hayatulii aisee!:-(


Kuhusu kwenda kuangalia NETIBOLI,..
... haki ya nani tulikuwa tunaondoka kiwanjani tunajua rangi ya bukta au chupi za wachezaji wote wasiovyaa tracksuit ,...
.... na ni kwa nadra sana tulijua ni timu gani imefungwa au nani mchezaji bora.


Kuna umri fulani katika ukuaji wewe acha tu! Halafu kila mtu muongoo ili kujifanya mbele ya vidume wengine tu kuwa ana mademu kibao wakati ukweli wenyewe ni bikira.

Yani wee acha tu!

Yasinta Ngonyani said...

Mtakatifu hapa umenitia wasiwasi ila najua nitamuda tu..."nanukuu Na kwa kuwa wewe una mtoto wa kiume ,...
... utastukia ni jinsi gani anabadilika kuanzia enzi za kutojali kucheza na wasichana,...
... enzi za kuchukia kucheza na wasichana na ambaye nafikiri kashafikia umri wakuanza kuwa na interest za watu wa jinsia nyingine.

- ukimchunguza utastukia ." mwisho wa kunukuu:- Mtakatifu hapa umenitia wasiwasi ila najua nitamuda tu.