Saturday, March 26, 2011

MAZISHI RUHUWIKO: TUUNGANE PAMOJA KWA KUMSINDIKIZA MPENDWA WETU ASIFIWE NGONYANI KATIKA SAFARI YAKE YA MWISHO

Asifiwe Ngonyani
Kuzaliwa 26/11/1989
Kuiacha dunia 23/3/2011
Kuzikwa 26/3/2011

Asifiwe Ustarehe kwa amani peponi Amina

Habari nilizozipata leo kutoka nyumbani Ruhuwiko ni kwamba watu wengi SANA wamemiminika na wanazidi kumiminika.TWAMSHUKURU MUNGU KWA HILI.
Leo tarehe 26/3/2011 siku ya jumamosi saa tatu tukwenda kuchukua mwili wa Asifiwe katika sehemu ya kuhifadhi miili katika Hospitali ya mkoa Songea. Baada ya hapo mwili wa Asifiwe unapelekwa nyumbani Ruhuwiko kwa buruani ambayo itakuwa saa tano. Saa sita mchana maandamano kwenda kanisani Ruhuwiko. Saa saba nusu mchana misa inaanza katika Kanisa la Ruhuwiko. Na baada ya hapo wote tunaandamana ili kumsindikiza mpendwa wetu ASIFIWE NGONYANI KWA SAFARI YAKE YA MWISHO. MWENYEZI MUNGU TWAKUOMBA UIPOKEE ROHO YAKE PEPONI AMINA.

FAMILIA YA MZEE NGONYANI NA FAMILIA YA NGONYANI/KLESSON ITATOA SHUKURANI ZA DHATI KWA USHIRIKIANO WENU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU!!!!

17 comments:

Mija Shija Sayi said...

Asante kwa taarifa hii Yasinta. Ni wakati mgumu sana kwa familia yenu, lakini kumbuka Mungu yuko nanyi na wala hatawaacha hasa katika kipindi hiki kigumu.

Mungu azidi kuwatia nguvu.

Amen.

Simon Kitururu said...

Poleni sana!

Anonymous said...

pole sana ,kufiwa na ndugu yako ukiwa mbali na kwenu-tanzania ningumu sana jikaze,na mungu atakusimamia. kaka s

Mrs Haule. said...

Pole sana Yasinta, yaani sikumjua huyu dada lakini nimestukia nalia kama nilikuwa mtu wa wa karibu na huyu dada. Mungu akutie nguvu mpenzi.

Fadhy Mtanga said...

pole sana.
Tunamtakia Asifiwe kupumzika kwa amani.
Amina.

Unknown said...

Soo sad,Mungu awafariji.

Baraka Chibiriti said...

Pole sana Dada yasinta, kwa pigo hili kubwa. Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele na lenye raha tele mpendwa Asifiwe. Pia ninyi familia kwa ujumla ili mpate nguvu zaidi katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu mzito. Poleni sana!

Rik Kilasi said...

Pole sana dada Yasinta na ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huu, Mungu awape nguvu na Imani katika kipindi hiki kigumu.Mungu akaweke roho yake mahala pema peponi na Mwanga wa milele akamuangazie Asifiwe Ngonyani.
Amina!

Anonymous said...

"Waache watoto waje kwangu maana ufalme ni wao" Courage,prayer,hope and blessings.

I remain.

EDNA said...

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi..

Unknown said...

USIJALI DADA YASINYA. YOTE HAYO YALISHAPANGWA, HIVYO HAYANA BUDI KUTOKEA KAMA TUJUAVYO HISTORIA YA MWANADAMU NA KISA CHA SHIDA ZOTE HIZI, ILA IPO SIKU YATAKOMA.

http://mtayarishaji.blogspot.com/2011/03/je-unajua-yanayotokea.html

HATA HIVYO NIMEFANYA MUENDELEZO WA FARAJA KWA KUZUNGUMZIA JAMBO HILI KWA NAMNA INAYOTIA MOYO KWA JINSI NILIVYOGUSWA.

TUPO PAMOJA WOTE...PEACE.

Baraka Mfunguo said...

Sina cha kuongea wala kuongeza katika machungu. Inasikitisha sana lakini ndio kipindi cha kuenzi na kuendeleza yale mazuri aliyoyaacha. Nafsi na mwili wake vitamezwa ardhini lakini hakika roho yake itaendelea kuishi. RIP ASIFIWE.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

RIP Asifiwe!

Poleni sana Ngonyani/Klaesson family

Sara Chitunda said...

natoa pole kwa familia yake yote Bwana awafunike na kuwaondolea majonzi.

Penina Simon said...

Jamani was too young!!!!!!!!!!!!!.
Mwili wake na ulale salama.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika ni kipindi kigumu sana tena mno lakini namshukru Mungu ninyi ndugu zangu hampo nyuma, hamuachi kunitia/kututia moyo bila hivi nawaambieni leo hii ilibidi nilazwe kabisa. Lakini Sala zenu na zangu/zetu hakika zinasaidia. Ahsanteni kwa kushirikiana nasi katika safari ya kumsindikiaz ndugu yetu Asifiwe. Amina.

Christian Sikapundwa said...

Ama kweli nimekuwa mbali sana na blog kutokana na matatizo ya mitandao.Dada yasinta Pole sana kwa Msiba wa ndugu yetu mpendwa Asifiwe Ngonyani.Pole sana kwa ndugu na jamaa iliyo kutwa na msiba huo,Ni imani yetu Mungu amesha mpokea dada Asifiwe mahala pema peponi. Yasinta msiba huwa hauishi upesi utazidi kupokea pole nyingi sana kwa wanablogia wote wenye upendo.Kwa kawaida kazi ya Mungu haina makosa.

Pole sana uwe mpole sana katika kipindi hiki cha majonzi kwako.

Dada