Thursday, March 17, 2011

MAISHA: NAZIPENDA SKAFU/SHALI ZANGU!!!

SKAFU ZANGU
Katika maisha sisi binadamu tupo tofauti kwa kila namna. Tukianzia tabia, sura, mwili, kupenda nk. Leo napenda kuzungumzia neno KUPENDA/TAMAA. Lakini si kule kupenda kwa kimapenzi hapana ni kupenda kwa kupenda vitu au kupenda kununua vitu hata kama anavyo vya kutosha:- Yaani utakuta mtu anapenda kikombe chake cha chai kweli kiasi kwamba mwingine akikigusa ni balaa. Mwingine anapenda kweli shati moja tu ambalo anaweza kulivaa kila siku utazani hana lingine. Mwingine akawa anapenda sweta kiasi kwamba hata kulifua anasahau. Halafu kuna hawa wanaonununua viatu, utakuta mtu ana pea za viatu chumba kizima huwa nashangaa sana je atavivaa lini? lakini hii yote ni basi tu yaani tamaa . Kwa hiyoleo nataka kuwaambia mimi ni MDHAIFU SANA wa SKAFU/SHALI. Hapo juu ni zaidi ya ishirini na bado natamani zaidi kwani nataka niwenazo rangi zote. NAPENDA SANA SKAFU.....Swali je wewe ni mpenzi/mkusanyaji wa nini?

10 comments:

Unknown said...

Dooh kwa kweli sijawahi kukutana na mtu mwenye skafu za kutosha kiasi icho ww ndo wa kwanza,hongera kwa hilo,kwa kweli ulichosema ni ukweliii kabisa mimi mwenyewe ni muhusika,kwa harakaharaka mm napenda kurundika magazine,yani ktk pitapita zangu kila siku siwezi kurudi bila magazine mkononi,ninazocountless.

Simon Kitururu said...

Mie nakusanya vitabu sana na ni vingi navyo hata kwa miaka ambavyo bado sijavifungua na ni vipya kabisa kisa nafikiria siku moja ntavisoma na kuna kitu ntajifunza.


Tatizo ni kwamba kuna baadhi ya vitabu sasa nimestukia elimu yake imepitwa na niko edition kadhaa nyuma wakati hata kabla sijavisoma !:-(

emu-three said...

Kesho kesho yaumiza matumbao,...skafu nzuri sana, nakumbuka nikiwa skauti....!

Mija Shija Sayi said...

Kutokana na kubadili mazingira nimejikuta hata sijui nilicho na udhaifu nacho, ila zamani nilikuwa nakusanya sana mapambo yenye asili ya kiafrika..

chib said...

Mie mkusnayaji mzuri sana wa CD na DVD za masuala yanahusu macho!!!! Ila ninajikiuta nashindwa kuziangalia au kuzisoma kutokana na muda!!!

Mbele said...

Sawa na ndugu Kitururu, mimi pia ni mkusanyaji wa vitabu, tangu nilipokuwa mdogo. Nashindwa kujizuia kununua vitabu. Hata kama nina kiu ya ulabu, halafu nikaona kitabu kinachonivutia, niko radhi kukosa ulabu :-)

Hadi sasa nina vitabu yapata elfu tatu, ambavyo viko Tanzania na hapa Marekani. Bado vinaongezeka. Nami nazidi kuwa na wasi iwapo nitaweza kuvisoma vyote. Najua haitawezekana, na ninakosa raha.

Rachel Siwa said...

Mimi napenda sana mapambo ya Nyumbani,ukumbini, na sehemu yoyote ile,kuna wakati natamani hata kama ningeweza huu ukuta niuamishie hapa na huu usogee huku.
kupika/kuijifunza vitu nisivyovijua,Hata kwenye pitapita zangu magazeti,majarida,vitabu vyangu ninavyo kusanya au vipindi ninavyoangalia zaidi ni hivyo!!.

Anonymous said...

unajuwa kupenda ni ugonjwa.mimi ninapenda sana viatu nina viatu mpaka sasa jozi zisizo zidi 20 nasiyovyote ambavyo nimevivaa zaidi ya mara tatu mpa wakati mwingine hujishitukia,na kama siyo kuwa na familia nafikiri ingenguwa balaa.
kaka s

EDNA said...

Jamani msema ukweli ni mpenzi wa Mungu, mie napenda viatu yaani nikiona kiatu alafu nikawa sina hela ya kununulia roho huwa inauma kweli.

PASSION4FASHION.TZ said...

Yasinta leo umenipata,ila samahani mimi ninapenda sana viatu na handbag yaani mpaka naona hata aibu kusema nina pea ngapi najaribu sana kujizuwia kuendelea kununua,mimepunguza sana hata kupita kwenye maduka nayopenda kwenda kununua viatu na hand bag,ila nimejikuta ile kiu nimehamishia kwenye ma bed sheets cover,yaani imekuwa kila nikienda madukani najitahidi nisiende kwenye womens fashion department, najikuta naishia kwenda home and furniture na naondoka na bed sheets.