Tuesday, July 29, 2014

MTU UNAISHI MARA MOJA TU DUNIANI HAPA KWA HIYO UNAPASWA KUJIPA RAHA PALE UPATAPO WASAA NA WALE/YULE UMPENDAYE!!

 Wakati mwingine mtu unapaswa kupumzika kupika ..kwa hiyo mimi na kijana wangu tulitoka nje na hiki chakula nilikula mimi au tusema tuliagiza tofauti na tukawa tunaonja  kipi ni kitamu zaidi
Kama muonavyo nikawa naonja cha kijana"Pizza" huwa sipendi sana  ila nilionja kwa vile naye alionja changu ambacho ni mshikaki  wa nyama ngómbe, viazi na bonge la saladi  bila kusahau cha kuteremshia mimi maji na kijana cocacola. Hapo sijui ni utamu au pozi??? Siku njema

12 comments:

Mija Shija Sayi said...

Kabisa tena Yasinta! Kijana naona hataki tena mambo ya kuwekwa bloguni au?...amekuwa jamani..

Yasinta Ngonyani said...

Yaani Mija kama ulikuwepo hapendi kabisa na ndiye yeye alipiga hizo picha

Christian Bwaya said...

Na njaa niliyonayo, macho yote kwenye mishikaki.

NN Mhango said...

Da Yacinta hilo sosi bomba ila punguza size. Utazamisha lote hilo bila kunenepa dada yangu? Karibu tule basi japo jasho la mtu haliliwi. Hiyo ni mishkaki au finyango?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Bwana umenifanya nitabasamu...ahsante kuacha lako lilikuwa moyoni.

Yasinta Ngonyani said...

Heeeehh, kaka yangu Mhango..ndo maana nimesema tuligawana nusu chake akachukua nami nikachukua nusu yake hata hivyo sikuweza....ni mishikaki kaka:-)

ray njau said...

Raha ya raha ni kwako na wenzio utapata karahaaaaaa tu.Hiyo kakakola imechakachua menyu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray kwa nini kakakola imechakachua menyu?

ray njau said...

Haina viini lishe!

Ester Ulaya said...

nimetamaniiiiiiiiiiiiiiiii

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! nimekuelewa.

Mama Alvin!...kilikuwa kitamu kwa kweli....

obat cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur