Saturday, July 19, 2014

BUSTANI YETU INAVYOENDELE...

 Ni mboga ya maboga na mahindi, ila hasa mboga maboga. Hii imekubali sana na nimeanza kula lakini mchicha na figiri mwaka huu vimekataa kabisa. Hata sijui kwa nini...
 Na hapa ni viazi mviringo na mahidi ...Mahindi nilijaribu tu  yanakaribia kuchanua ila sijui kama nitavuna muhindi. Ila viazi karibu nitavuna kwani sasa vinachanua kwa hiyo mwezi ujao tutakula.
Mwaka huu tutakula na ZABIBU  kama mnavyoona hapa:-)
JUMAMOSI NJEMA BINAFSI NIPO LIKIZO KWA HIVYO MKIONA SIPATIKANI  MJUE  MAJUKUMU. ILA SITAPOTEA SANA MAANA SISI NI NDUGU LAZIMA KUTAKIANA HALI.

5 comments:

Mbele said...

Hizo picha za mimea ya viazi, mahindi, na maboga zimenikumbusha maisha yangu ya utotoni kule kijijini kwangu Lituru, Umatengo. Yaani mno, siwezi hata kuelezea. Nilikuwa nashiriki katika kupanda na kupalilia mazao hayo, na mengine, wakati mwingine huku mvua ikinyesha na udongo kuwa tope.

Ningeweza kuandika insha au hadithi ya kubuni, lakini yenye uhalisi huo. Picha zimenikumbusha mbali. Nitazichungulia mara kwa mara, kwa vile niko huku ughaibuni, angalau nijisikie niko kwetu. Asante sana.

Yasinta Ngonyani said...

Prof. Ni kweli kabisa sio peke yako hata mimi huwa nikiangalia nakumbuka sana nyumbani ingawa nilikuwa mvivu kidogo wakati ule. Na hii ndio sababu kubwa kuwa na bustani ili kukumbuka mazingira ya nyumbani. Ahsante sana kwa kuliona hili.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Da Yacinta bustani inapendeza. Natamani kungekuwa na uwezekano lau wa kututumia mboga mboga ufanye hivyo, Huwa tunapenda kuwa na bustani lakini muda wetu hauruhusu. Ukiwa unakula matunda tafadhali tukumbuke nasi hata kama hatuna uwezo wa kujiunga kwenye makulaji.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango.....usikonde nitumie add. Na uone wala mie si mchoyo su karibuni hapa kwetu. Ahsante kupita hapa na kuacha lako ls moyoni

Interestedtips said...

dada naku salute bustani imependeza hadi rahaaaaa