Tuesday, July 1, 2014

BUSTANI YETU MWAKA HUU INASUA SUA ..ILA HAYA NDIYO MAENDELEO YAKE.....

 Hapa ni mboga ya maboga tena ni zile mbegu nyeusi kutoka njombe nilipewa na mama yangu wa hiari mama Mgaya.
 Na  hapa ni viazi mviringo na mahindi ..ila mmmhhh haya mahindi sijui kama nitakula....
 Kwa vile ni Kapulya nikaona ngoja nijaribu na parachichi na huu ndio mti wa parachichi ila na hapa nina wasiwasi kama nitakula....
Mnazi pia unapatikana ... MNAZI MMOJA:-)
KILA LA KHERI PANAPO MAJARIWA TUTAONANA....KAPULYA A.KA DADA MKUU.

6 comments:

Anonymous said...

Bustani ya dada Yasinta hiyooooooo. Kwa kweli unastahili pongezi sana mana hali ya hewa kama unavyosema inasababisha hivyo. Tutakula kitakachopatikana mana juhudi zako naziona, mana ungeweza kusema aah! silimi na kupanda mwaka huu mana hali ya hewa ila hapana umefanya sehemu yako, ama kweli jembe halimtupi mkulima. Siku njema.

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante sana kuwa nami na karibu kusadia kumwagilia-:)

Anonymous said...

Ntakuja kumwagilia uache tu mpira wa maji hapo nje ili nikija moja kwa moja naendelea na kazi, sigongi hodi kuingia ndani. Inabidi kweli kusaidia kazi kabla ya mavuno.

Anonymous said...

Msinisahau maboga yangu saa ya Kufuturu na mfungo wa Ramadhani. Hongera da Yasinta. By Salumu.

Mbele said...

Hizi picha zinanivutia sana. Hongera na asante.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina usihofu mpira upo huko nje ww njoo tu.
Kaka Salumu usikonde maboga yakikomaa yu utapata..
Nakutakua mfungo mwems wa RAMADHANI.
Pro Mbele......ahsante...ni kweli zavutia mno