Sunday, July 20, 2014

EBU LEO TUANGALIA VITU VYA MSINGI VYA KUTINGATIA KATIKA MAISHA YAKO!!

Katika pitapita kutoa salamu hapa na pele nikakutana na hii  nimeipenda sana na nikaona niiweke na hapa  Maisha na Mafanikio. Nimeipata baada ya kupita hapa. Haya karibuni!!
1. Kuwa karibu na wazazi wako na familia yako pia.
2. Kuwa makini na kila kitu katika maisha yako.
3. Kuwa na kiu ya kuipenda afya yako, kufanya kazi kwa bidii, kula na kuvaaa vyema.
4. Usijihusishe na mambo yasiyo na faida katika maisha yako.
5. Jali thamani yako machoni mwa watu hata kama unapitia katika nyakati ngumu maishani mwako.
6. Usiuabudu umbea.
7. Kuwa makini na marafiki unaowachagua kuwa nao maishani.
8. Usicheze na muda kwa kuamini kesho ipo.
9. Kuwa halisi wakati wa kupanga plan zako na hakikisha kila mara unazipitia kuona kama uko sahihi.
10. Kuwa mwerevu kwa kuishi vyema na jamii inayokuzunguka.
11. Andaa mipango inayoendana na wakati uliopo.
12. Maliza kazi zako kwa muda muafaka.
13. Usilale kwa kuchelewa ukijitetea kuwa unamalizia kazi, panga muda wako kwa kufanya kila jambo kwa wakati wake.
14. Hakikisha unatatua kwa busara, hekima na uvumilivu mkubwa kila tatizo linalokukabili katika maisha yako.
15. Usiwe mtu wa lawama kila mara kwa wakuzungukao.
16. Jitahidi kuwa mtu wa kuyakubali makosa yako na sio kumrushia mwenzako.
17. Heshimu kila anayekuzunguka pamoja na changamoto zao.

Imeletwa kwenu na Fred Kihwele.

5 comments:

sam mbogo said...

Ni mawazo/ushauri mzuri hasa kwetu sisi binaadamu.kuna mambo mengi pia tuna shauriwa kuya fuata ama kuto ya fuata ili tuwe wakamilifu katika maisha yetu ya kila siku,na hi nikwa ajilri ya kujiepusha na kutumbukia katika matatizo miongoni mwetu sisi kama binaadamu.kitu nilicho jifunza hapa ni kwamba binaadamu nikiumbe wa ajabusana,hasa katika maamuzi.kaka s

Ester Ulaya said...

ni kweli kabisa dada ila tu ubinaadamu huwa unatupitia tunashindwa kuyafuata yote hayo

sam mbogo said...

mama KATUTU-Ester hivi bodo mnaendelea na chama lenu la KITAMBI NOMA mimi nitakuwa huka wiki moja kuanzia sasa ningependa kujumuika nanyi katika chamalenu ilinipunguze kitambi .wapi mnakutana na line muda mawasiliano nikifika. wewe nielekeze eneo nitatafuta. asante
kaka s

Ester Ulaya said...

Hehehehe kaka Sam...chama letu bado lipo linasonga mbele hasa...Kataa Unene Family...ukija we nisake tu at any time T... utasaidiwa na kitambi kitayeyukaa hocho

Christian Bwaya said...

Kuyeyusha kitambi? Ha ha ha!