Wednesday, May 29, 2013

WATU 8 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 11 MAJERUHI AJALI YA GARI - NAMTUMBO !!!!

 

Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga

Watu nane wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiriaKwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma DeusdeditNsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe 26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku katika kijiji cha Hanga eneo la bombambili mkoa wa Ruvuma,chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa.Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA,Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.Kamanda wa Polisi amesema gari hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8) na majeruhi kumi na moja (11) ambaowote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Kutokana na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria. Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja ambapo. CHANZO:- DEMASHO

10 comments:

issack che Jiah said...

Poleni kwa wausika .tatizo hili aliwezi kwisha kwa mikoa kama ruvuma na mtwara,hasa wakati huu wa mavuno watu wanasafiri sana na malori na kukiwa na mizigo ,ukweli linapotokea tatizo kama hili lazima watu wapate matatizo hasa kufa na majeruhi ,hii inatokana na miundo mbinu kuwa mibovu inapelekea wenye mabasi kushindwa kupeleka mabasi vijijini, Miaka na hiyo kulikuwa na mabasi ya vijiji nakumbuka kule kwetu songea kulikuwa na basi la kijiji cha muyao ,matetereka ,Ndongosi nk mbali na yale ya Akina komba na mtumweni narudia pole sana Ndugu zango wa kule hanga ,namabengo ,ntyangimbole na namtumbo
na kwingineko
Che jiah

ray njau said...

Pole sana kwa ndugu,jamaa na wote waliopata madhara kwa njia moja au nyingine kutokana na mkasa huo wa barabarani.

MTU KWAO said...

Kwa hili serikali liitazame kwa makini sana hasa muda huu wa msimu wa mazao
MTU KWAO

issack che Jiah said...

mbana dada hujatupa majumuisho na wengi leo hawajakuunga mkono na kukupa pole kwani hawajuwi kama hili ni janga wamo akina ngonyani
che jiah

Yasinta Ngonyani said...

Kaka isaack! Umenikumbusha wakati naishi kijiji cha Kingole. Basi bwana kila kitu kilikuwa ni i kimoja tu ...gari la kijiji lilikuwa likisafiri kwa mwezi mara moja au zaidi. Kska majumuisho ya nini? Huwezi kumlazimisha mtu akuunge mkono au lukupa pole. Nimefurahi ww umeungana nami pia kaka Ray.


Kaka Ray...ahsante kwa niaba, pamoja daima.

Mtu kwako...nimependa jina lako

Rachel Siwa said...

Poleni sana wajameni!

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI! ! Ahsante alo...ni mimi KADALA/KAPULYA

ISSACK JIAH said...

MTU KWAO NI KAKA AKO CHE JIAH
KWA JINA LA BLOG YANGU

Emmanuel Mhagama said...

Pole nyingi ziwaendee wote waliopata majeraha katika ajali na wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na rafiki zao katika tukio. Mungu awape subira na uvumilivu katika majonzi haya makubwa.

emuthree said...

Ajali, ajali ajali...kila siku masikio hayakosi kusikia kauli hii, ...je ni kweli ajali haina kinga? Mbona kila kukitokea ajali hakukosi kuwa na sababu, ina maana hizi sababu zipo juu ya uwezo wetu? najiuliza bila majibu.
Poleni, tupoleni kwa matukio hayo ya kuskitisha, dada wangu Yasinta.