Thursday, May 30, 2013

UKIFIKA MKOA WA RUVUMA USIKOSE KUTEMBELEA ZIWA NYASA....USISAHAU ULIKOZALIWA!!!!

 Hapa ni ziwa NYASA ebu angalia linavyomeremeta ....karibuni sana
Pia hutaindoka bila kula kama vile picha hii inavyotuonyesha ni DAGAA ambao huwezi kuwapata sehemu nyingine  na ndio maana wanaitwa DAGAA NYASA.......
Na samaki pia utapata ...Nakumbuka jina lake ni "MAGEGE"  kwa ugali wa muhogo weweeeee!!. TUONANE TENA WAKATI MWINGINE.Kapulya

13 comments:

MTU KWAO said...

Kimaamdhali ziwa ni pazuri sana na ukiangalia pale mbambaby na kule liuli utapenda sana na kiutalii bado serikali yetu hapaja boresha miundo mbinu ,utakuta bado njia ya kufika mahali kama huku yawezekana ni kama ile ya kwenda uwanja wa vita ,kama serikali ingitilia maanani umuhimu wa swala hasa la utalii pesa ingekuwa ni njenje na neno umasikini kwetu tz lingekuwa halipo ,ukweli sisi wananchi tunaumia tunapoona watu tunaoishi maeneo yenye utalii tunaishi maisha ya chini na duni .SERILIKALI IBADILIKE
iweke miundo mbinu na vitendea kazi viboreshwe ,na vilevile wawekezaji wadogowadogo hasa wavuvi wapewe zana zao na walimdwe soko lao.samaki wa nyasa ni watamu na hao MAGEGE ,MBELELE ,NA DAGAA , WAKE watamu kwa ugali ulee wa kulowekwa wa muhogo ni mtamu saaana kwa samaki
DADA SIKU NJEMA
CHe Jiah

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Che Jiah! Hakika Umenena....Tatizo ni barabara lakini ni kweli mkoa wetu wa RUVUMA una VIVUTIO VINGI SAN..Duh umenikumbusha Liuli..Ahsante kwa mchango wako mzuri.

Anonymous said...

Mashallah. Natamani ugali wa muhogo na samaki wa Nyasa! By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu. Basi inabidi ukaribie nyasa utakula hadi ile mbaya...

Anonymous said...

Jamani Dada Yasinta, mh mie sio mtu wa songea ila ni mTz. Songea nimefika kikazi, sasa kwenda huko Ziwa nyasa, jamani jamani Yansi´nta barabara inatisha sana sana, yani ukiangalia chini kulia na kushoto gari linavyopanda mlima likikosea tu ni kifo! Ila sijui kwa sasa kama wameishatengeneza au la? Je barabara bado iko vile vile? Mie nilifika huko 2004 hivi! Ila ukiishafika huko mh ziwa nyasa linavutia mno mno...ila mh kupanda barabara ilivyo nyembamba mie niliogopa sana. Kweli samaki huko hadi basi nk. Na hata songea hapo mjini nilikaa hostel ya dini nzuri mno tulikuwa tunapikiwa vyakula vitamu sana na juice ikabidi tuchukue mapishi hakukuwa na ujanja. Ila na mbinga kule kwenye mashamba ya chai kuna vutia sana, sasa kilichonishangaza huko mbinga ni kuwa kijijini ila watu wengi wana magari tena mazuri tu! tena magari binafsi wakulima wa chai..na wamejenga nyumba nzuri tu nilishangaa sana kuona landrover za wakulima...Kumbe chai inalipa ikikubali! Jamani songea pana uzuri wake, nimalizie na Peramiho jamani jamani kuna sausages kubwa hizooo halafu ni tamuuu sana kwa masista ila hizo zilikuwa zinapatikana huko tu sio za madukani kwingineko! Kuna na vyakula vingine vizuri, kwa hayo naikumbuka songea sana au niseme mkoa wa Ruvuma.

Anonymous said...

Nilisahau zile sausages za peramiho zina taste nzuri sana na nilikula kama hizo wakati nipo ujerumani! Nikaja kuzikuta huko Peramiho kwa masista..ila sio sausages zinazouzwa mitaani au madukani kwingine hapana. Za peramiho lahda yake ni tofauti na ni sawa na za ujerumani kabisa au wanatoa ulaya ila sijui! Sausages hizo sijawahi kuziona Dar es salaam na kwingineko ni peramiho tu. Sijui nirudi huko tena kwa ajili ya sausages? Au dada yasinta ukija enda nikuagizie uniletee nini!

Yasinta Ngonyani said...

Oh! Basi usiogope ...binasfi nilienda nyasa nilikozaliwa 2005 na barabara ililuwa safi kabisa
Ma mwska jana ilikuwa safi zaidi na sass kugiksa peramiho ni rami tupu. Kwa hiyo karibu ndugu wangu

MTU KWAO said...

Dada Yasinta huyu ndygu asiye na china alifuata kula kule kwetu kwani ukweli anasifia maamkuli na sehemu zote alizopita mambo yalikuwa sawa ila mimi nakumbuka nilipokuwa nasoma kule vyakula vyote vilikuwa vinapikwa kwa mafuta ya mbuzi katoliki siku hizi almaarufu KITIMOTO hivyo najuwa SOSEJI za masista wanatengeneza kwa huyo mbuzi katoliki na nilazima atasikia Utamu kupita zile wapikazo mitaani kwani Pale meja seminari pana mbuzi katoliki hao kazi yake kuchuja mafuta na nyama yake ni kutengeneza hizo soseji
muwe na siku njema na ingefaa dada tukumbushe ule wimbo wa chioda wa meli yetu mbeya AU KUNA ULE WIMBO UPO KWENYE HISTORIA YA KITABUcha darasa la sita MKISI CROSS LIKE NYASA MIMI MNAUKUMBUKA MWALIMU WANGU ALITOKA KULEE LITEMBO Alikuwa anaujua sana
1.mkisimmoja kavuka nyasa x2
kaenda ng'ambo mpaka nyasaland
akanunua muhogox2
2.akaparaza kitumbwi chake x2
salama akafikaka katikati
dhoruba iikaanzax2

CHE Jiah

Yasinta Ngonyani said...

Kakangu Che Jiah! hakika umeifanya Ijumaaa yangu ianze vizuri sana bahati mabaya huo wimbo sijawahi kuusikia ila nimeupenda sana Ahsante kaka...Na pia kuhusu mafuta ya mbuzi na soseji nimefurahi kujua...

MTU KWAO said...

ASANTE SANA SIJAIONA LEO MAADA KWANI KWANGU INACHELEWA KUINGIA NI MPAKA JIONI NDO NAIONA ,NASHUKURU KUONA LEO UPEPITIA MAPEMA
KULE KWETU KUNA VITU VINGI NA HASA CHAKULA INABIDI HUYU MTU APEWE URAIA KULE SONGEA ILI ALE MBUZI KATOLIKI KILA SIKU NAJUWA WATU WENGI WANAIPENDA RUVUMA KWA HALI YA HEWA NA MAMDHALI YAKE NA WATU WAKARIMU SANA
SIKU NJEMA
MTU KWAO
CHE JIAH

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Che Jiah...hata mimi huko mtu kwao sijapita nami nataka hivyo vitamu ni vipi kufika?..mada ya leo ishawekwa uwanjani pitia utaona---Ruvuma inavuma bwana:-)

Anonymous said...

Ruvuma ni kuzuri sana na hali ya hewa ni nzuri pia. Sikuetgemea kuwa patakuwa hivyo nilipofika nilipapenda mno. Ntakaribia tena wakati mwingine nikipata safari ka kikazi.

Yasinta Ngonyani said...

Basi usikose kuja kwetu ruhuwiko..KARIBU SANA TENA SANA