Thursday, October 25, 2012

UNATAKA KUNYWA SODA/VINYWAJI BARIDI? BASI JARIBU NA HII HAPA/AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE-UBUNIFU!!!

JIPATIE VINYWAJI BARIDI

Kuna namna nyingi ambazo sisi wanadamu tunaweza kujipatia huduma zetu tofauti na vile tulivyozoea. Ili kinywaji kiwa baridi tumezoea kukiweka kwenye jokofu/fridge ili kipate baridi, na hii hutumika zaisi maeneo yenye hali joto kama vile Dar Es salaam nakadhalika. Kwenye sehemu za baridi kwa Tanzania kama vile Njombe, Mufindi, Makambako n.k mara nyingi hawatumii majokofu, kwa kuwa vinywaji hivyo vinakuwa vya baridi tayari.
Sasa basi iwapo huna jokofu haimaanishi huwezi kujipatia kinywaji cha baridi. Ni hivi chukua soda na uziweka ndani ya maji yaliyomo ndani ya mtungi kwa usiku mzima, na asubuhi zinakuwa baridi  safi kabisa kwa kukata kiu yako.
Vyungu hivi hutengenezwa na sisi wenyewe waTanzania, na hutumika kwa matumizi ya kupikia, kuhifadhia na leo hii tunajifunza pia twaweza kufanya zoezi hili. Pia kuna aina nyingine ya ubunifu katka kutaka kinywaji kiwe baridi ni hivi:- Chukua soksi na uiweke chupa ndani ya soksi na halafu weka maji kwenye chombo chochote kile kama ndoo vile utaona matokeo yake itakuwa baridiiiiii..UJANJA eehh:-)

5 comments:

Emmanuel Mhagama said...

Hii imenikumbusha kijijini kwetu. Tunatumia hadi leo hii kwa ajili ya kuhifadhia maji ya kunywa. Kitu ninachokifurahia kwa habari ya maji ya mtungini ni kwamba ubaridi wake ni "standard", siyo ule wa kuumiza meno. Kwa hakika inafurahisha sana.

Yasinta Ngonyani said...

halafu sasa uwe na kata (ndeve kwa kingoni) hapo ndio utajua utamu wa maji ya kwenye mtungi...

Emmanuel Mhagama said...

Au kikombe cha bati, siyo glass.

ray njau said...

Hakika inapendeza kujua ya kale ni dhahabu!

EDNA said...

Ubunifu wa hali ya juu.