Monday, January 25, 2010

Wazungu bora kuliko waafrika!?

Makala hii nimeikuta Jamii Forum nimeipenda na nimeona niiweka hapa kwangu ili tusaidiane kwa mapana swala hili.


Baba yangu mzungu, mchanganyiko Irish/dutch
Mama yangu msambaa lakini nilishangaa jana kukuta hii post kule JIACHIE.
JE NI KWELI KUWA WANAUME WAKIBONGO HAWANA MPANGO? Sunday, January, 17, 2010
Salama jamani huko?? Kuna huyu dada mmoja wakiTanzania, yeye baada yakuolewa na mzungu anaona kuwa manamume wakibongo hawana mpango. Hebu soma hii blog yake.... Ni kweli wajomba zangu wakiswahili ni wayeyushaji?

Im not a great writer, that is evident. Sijui kupangilia sentensi zangu…..so bear with me Sasa leo nataka tuweka wazi swala zima la wasichana wa kitanzania kuolewa au kuwa na maboyfriend wa kizungu.

Mimi binafsi nime-notice kwamba wasichana wengi wa kitanzania wamekuwa wakiona kwamba kuwa na boyfriend ama mume ambae ni mzungu is actually an achievement in life. Na wengi wamekuwa hawataki kabisa hata kuwa na ma-boyfriend ambao ni waa-africa especially watanzania.

Na kuna wasichana ambao nawajua ambao wako kwenye relationships na mwanaume wa kitanzania lakini anaeleza wazi wazi kwamba anatamani apate mwanaume wa kizungu. Mdau wewe unanaoje swala hili? Je hawa wasichana ni kwamba they are shallow and stupid? Or are they very smart???

Really kabla huja-judge na kutuma comment za kuwatukana lifikirie hili swala vizuri… Mimi personally naona kuna 2 sides to this issue.kuna wale ambao watanaka kuwa na wazungu na hawataki ku-date watanzania wenzao kwasababu za kijinga na zisizo na msingi, 1st side…

Kwa mfano kuna wengi facebook unaona mtu akipata boyfriend wa kizungu basi anamwaga picha zake na mzungu facebook, sasa hizo comments za marafiki nayeye mwenye mchumba ndio zinazotuharibia wengine wote..nashindwa kuelewa kabisa ni kwanini mtu akiweka picha yake na mzungu facebook basi kila mtu anamwandiki comment ‘UKO JUU’, ‘UMEOPOA MAMA UKO JUU’ , ‘KWELI MUNGU MKUBWA’ , ‘RISKI ZIMEFUNGUKA MWAKA HUU’, KWELI MUNGU AMEKUKUMBUKA’ , comment kama hizi na zingine za disini hii zinanisikitisha mno…jamani hivi kweli kuwa na mwanaume mwenye ngozi nyeupe ni kitu cha maana kiasi hiki? alafu hivi kweli tumejishusha utu wetu kiasi cha kwamba tunafurahia in public? Kwanini msiweke comment kama ‘u look happy’ ,’hongera kwa kupata mchumba and so forth’ …kuwa na mzungu sidhani kama inamaanisha uko juu or whatever. (kama moja ya comment nilizoandika hapo zipo kwenye picha yako ,please usijisikie vibaya, niliitumia tu kama mfano ili kuwapa wasomaji wangu picha kamili,its really not about you) hivi kweli hawa wazungu wenyewe wangekuwa wanajua kusoma Kiswahili humo facebook ingekuwaje??

Wanawake wenzangu wa kitanzania, tuache kujiabisha na hili swala zima la mzungu mzungu mzungu, especially kwenye facebook, mtu akikuwekea comment ya kishamba kama hizo hapo juu usiishadadie sana, ikiwezekana i-delete akuwekee comment ya maana, … Kama wewe ni mwanamke ambae kupata mzungu is an achievement basi , I am sorry to say ,you are without a doubt a loser,

Wazungu wanamatizo mengi tu, na hata ukiangalia the highest divorce rates in the world zipo western countries na sio kwetu.

na kwa wale wenzetu wanaodhani wazungu wote wanapesa na kwamba atakuhonga basi unajidanganya kabisa, mzungu sio muhongaji , kama unataka kuhongwa bora mapedeshee ya kibongo litakununulia hata gari baada ya kukujua kwa siku chache tu.hahahahha…. Wazungu wanachukua muda wao kumsoma mtu na tabia zake, na kama kuna chochote atakachokufanyia ni baada ya muda mrefu na kwamba umeshakuwa mke wake au labda anahisi utaishia kuwa mke wake.

Na pia ndugu zetu wa kibongo wanaweza kuishi na mwanamke asie na income yoyote, na asiejishughulisha la lolote, asilimia kubwa ya wazungu hawawezi kabisa hii tabia. So kabla hujarukia na kugeza watu, angalia usije kuchanika msamba…lol….

2nd side… Kuna wale wasichana wa kibongo wanaotaka kuolewa na wazungu for the right reasons. Hao ndio ninaowalewa mimi…

Ukweli lazma tuuseme leo… Asilimia kubwa ya wanaume wa kibongo ni miyeyusho mitupu , tuseme labda 80%....sasa wewe utakuwa na bahati gani mpaka upate mmoja wa hiyo 20% ambao ni wastaarabu. Ukweli ni kwamba, nikiangalia rafiki zangu walioolewa na wanaume watanzania na walioolewa na wanaume wazungu, walioolewa na wazungu, are way more content in their marriages, ofcourse kuna exception za rafiki zangu wachache waliiolewa na wabongo na wana-enjoy ndoa zao na ndoa zao haziwapi homa kila siku…

Mie nafikiri,wanawake wengi wa kitanzania wameamua kuwa na wazungu kwasabu wanatafuta pumziko la roho…ukweli ni kwamba wanaume wengi wa kitanzania wanasumbua mno tena kupita kiasi.

Mwanaume wa kitanzania amelelewa akiona baba yake ana wake wawili na nyumba ndogo kama tatu, je unadhani yeye atakuja kuwa mume wa aina gani???? Mwanaume wa kitanzania anajiona ni mwanaume kamili zaidi kama anawanawake wengi, na kitu ambacho yupo proud nacho kiasi ya kwamba anaweza kukaa na rafiki zake bar akaadisia jinsi gani anawanawake wengi na wenzio wakamuona ‘YUKO JUU’….

Mwanaume wa kizungu, hajakulia kwenye mazingira haya and automatically ipo kichwani mwake kwamba anatakiwa kuwa faithfull kwa mke wake na kumtreat as an equal.hata ikitoea akawa macho juu akapata kidosho nje, atajificha, hutojua lolote na ni jambo la aibu sana kwake kiasi cha kwamba hawezi kuongelea hadharani. Umeona tofauti hapo?

Huwa nasikitika sana, nikienda disco, unaona kabisa janamme lina mke na watoto, lipo disco na totos nyingine na anajua unamjua mke wake na labda utamueleza lakini haogopi kabisa, Hivi kweli hapo unaweza kumlaumu mtoto wa kitanzania akianza kutafuta mzungu??? Anakuwa ni kwamba ameamua hataki kuumizwa roho yake wala akili yake ana anataka kuishi maisha yake in peace.

Sio kwamba wazungu hawacheat au na wao sio washenzi wakati mwingine, tofauti ni kwamba hiki sio kitu cha kawaida kwao na hata akiwa mshenzi basi huu ni samaki mmoja mmbovu,inabidi tu awekwe kwenye kapu la pekee…lol…

Mwanaume wa kitanzania, kama hajatembea na rafiki zako,au mtu ambae unamjua basi haoni raha kabisa,

And whats worse, wanaume wa kitanzania haachi mke wake hata siku moja, atamtesa mke wake miaka kibao lakini hamuachi..yani mmbongo atakufanyia vituko weeeee mpaka utaondoka mwenyewe utarudi kwenu, but mzungu akipata mtu nje, atakuja kukwambia on your face, i don’t love you anymore,I love somebody else. Ofcourse inauma sana but atleast utakuwa umeachwa with respect, lakini kaka zetu atamake sure amekutoa all your dignity, kakuabisha mji mzima, amekutoa confidence yote ndio anakuacha…lol…

Na wasichana wengine wameniambia pia wanachukia tabia za kaka zetu za kufanya nao ngono alafu wanakaa bar na kuanza kuhadithia rafiki zao, Yule demu yuko hivi yuko vile, huu mji ni mdogo sana, unaingia sehemu unadhani umevaa nguo kumbe watu wanakujua ulivyo ukiwa uchi…

Basi siku hizi utawasikia wanaume wa kitanzania wanatukana hawa wanawake wetu wanatamaa sana, sijui wanawafatia nini wazungu,kila mtu mzungu,kila mtu mzungu. Kaka zetu you are the best, lakini badilisheni tabia zenu….

Kuwa na wanawake wengi sio haki yako.sana sana ni kujitafutia magonjwa na kumpelekea mkeo asie na hatia.

Tunawapenda sana, lakini anzeni kutu-treat with respect ,love and humanity. Ni hayo tu wadau kwa leo ambayo nimeweza kuyaelewa ndani yah ii issue nzima ya wanawake wa kitanzania na wazungu…….
wewe una yapi mdau?

16 comments:

Anonymous said...

labda wewe utuambie vizuri maaana una uzoefu mkubwa na pia wewe unaonekana mkweli unaweza ukasema bila kupendelea upande wowote

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bagueni rangi lakini kila mtu binafsi na tabia yake au njia yake ya kufanya atakacho kwa hiyo kuangalia rangi sio sahihi sana

harafu mimi sikuwahi kuwa na kimdhungu kwahiyo no uzoefu

Anonymous said...

Dada Yasinta waiting to hear from you na Mchungaji Kitururu uko da same boat /Train na wewe huwaga na wathungu tuambie dada zetu wa kibongo vipi?

lee cushman said...

Mmmmh!No comment.

Bennet said...

Haya wenye experience tuambieni

Anonymous said...

wewe umeolewa na mzungu una uzoefu haya tuambie.

Anonymous said...

Hakuna lolote kuna baadhi mmeamua kuolewa na wazungu kwa sababu ya umasikini ili muende ughaibuni mpate kusaidia wazazi/ndugu zenu.

Anonymous said...

kuna wa2 wazuri na wabaya kwenye rangi zote hapa duniani,pili wanaume na wanawake wengi 2najumuishwa,yani m2 anasema wanaume wote waongo au wanawake wote waongo,ila ukweli ni kwamba wapo wanawake na wanaume ambao sio waongo,sasa nikirudi kwenye swala la wazungu,hakuna 100% kua ni bora kuliko sisi wenye rangi za kahawa,na wala sisi wenye rangi za kahawa c bora zaidi yao,narudi palepale wapo wazuri na wabaya popote,pia hata sisi 2likua huku ughaibuni kuna kipindi kinaitwa cheaters hapa US,wengi wanaokamatwa ni wangoswe sasa uzuri wao uko wapi,kwa kifupi inategemea na m2,ila km ishu ni financial kweli wenzetu wamepiga ha2a kidogo,so km ishu ni hyo sawa,ila km ni uaminifu kwenye mapenzi au ndoa,ngoma droo.

Mija Shija Sayi said...

Anony wa 'January 25, 2010 9:42 PM' amesema kweli.

Yasinta Ngonyani said...

haya jamani ukweli ni kwamba wazungu, waafrika,wachina, wajapan nk. kwa mtazamo wangu naona ni sawa tu kwani mwanamume ni mwanamume na mwanamke ni mwanamke hata akiwa na rangi ya aina gani. Nimeipenda mada hii kwani kuna wengi wameniambia binafsi kuwa nina BAHATI kuolewa na mzungu. Na nimekuwa najiuliza siku zote ni bahati gani niliyo nayo ingawa sijawahi kuolewa na mwafrika mwenzangu lakini nategeme hakuna tofauti.

Kuna wanaoona kama mmoja ameolewa/oa mzungu basi wanaona kama alivyo andika mwenye mada kuwa "UPO JUU" nimekuwa nikijiuliza watu wanaosema hivi wana maana gani? Ndio maana naweza nikapinga na kusema hakuna aliye bora kati ya mzungu na mwafrika.

Simon Kitururu said...

Wazungu kama Waafrika wanatofautiana.

Kwa mfano kwangu: Wanawake wa Kirusi, Kiistonia , Kilatvia huwa nawafananisha sana tabia na baadhi ya wasichana wengi tu wa Kitanzania.

Na Wanawake wa Kispanisha na Kiitaliano huwa nawaona ni kama kinyume kabisa na Wanawake wengi wa Kifini, Kiswidi , kinorwei au tu ni seme Kiscandinavia. Wanawake Wakiscandinavia kuna mambo nawaona wako huru zaidi na maisha yao na maamuzi yao ni yakibinafsi zaidi.


Ukienda Marekani pia utastukia tu waitwao ni Maredneck ni wakinanani kwa tabia .

Nachojaribu kusema ni kwamba ukiongelea Wazungu , KIJUMLA JUMLA kwa KUWALUNDIKA KATIKA MAKUNDI jua kuna tofauti zao hata kijiografia .

Na ukiingia kwa undani nakubaliana na Komandoo Kamala kuwa kila mtu ni binafsi na tabia binafsi za mtu hazifuati rangi wala kusababishwa na rangi. Kwa hiyo kuanzia matapeli, viruka njia,wazuri kitandani, wabaya kwenye teremka tukaze, wafanyakazi bora, wavivu wa kwenda kazini, wenye akili darasani, wajinga, kama tu katika jamii yoyote wanapatikana katika Wazungu kama tu wapatikanavyo kwa Wabongo.

Na kwa kulundika watu katika makundi , sijui kwanini mademu wa Kikikuyu waliowahikunisaidia kunituliza moyo kitabia wanafanana sana na Wakichaga bongo. Na wasichana wakutoka Peru kadhaa nawafananisha sana kitabia na wakutoka Thailand.



Ila kila mtu ana sababu zake za kufikia hitimisho ni wakinanani ni bora.

1. Nani ni bora kwa CHUNA BUZI.

Kama ni kipesa watu wengi kutoka nchi magharibi wanapesa zaidi ya watokao Bongo kiwastani. Kwa hiyo kama nia ni kubahatisha mwenye pesa katika bahati nasibu hiyo mtu anaweza bahatisha chuma bizi kirhisi kwa kuwalenga watokeao nchi za magharibi kuliko sie kama mimi nitokaye Morogoro. [Hapa siwaingizi katika asilimia Wazungu watoka nchi za ulaya mashariki.)

2.Matatizo ya Kila siku Chai na KITUMBUA TU!

Kuna wahusuduo vitu tofauti na adimu kitu kilicho fanya mpaka baadhi ya mawe kama almasi kuonekana kiboko kwa kuwa ni machache tu.

Kutokana na hilo wakati nasoma Mfaranyaki Songea, wajanja walikuwa wananyemelea watoto wa kihindi kwa kuwa walikuwa wachache shuleni kwa hiyo hata mbaya ukipinga naye urafiki wewe waonekana mjanja. Halafu kumbuka enzi hizo za utoto kumbuka hata mchezo wa baba na mama ulikuwa ni kinguonguo.:-(

Na kwa wazungu sehemu kama Ulaya ya kusini kama ya Spain , Uingereza kwa kuwa wanashortage ya Mablondi , mablondi huwa yanadaka sana akili za wahusuduo mionekano kwa sababu hiyo hiyo.


3.Sababu kubwa iko katika tafsiri ya UBORA ni nini.

Kwa hiyo jinsi utafsirivyo ubora wa kitu ndio waweza kujipatia mwenyewe ni nini ni bora. Na kama kiimani ndio upatavyo ubora. Bora maishani kwako ni mcha Mungu na kumbuka mcha Mungu hana rangi.


Na kumbuka pia kuna mambo mengi yapo katika hili swala ikiwamo la baadhi ya jamii kuchagulia watu wachumba, wengine kulazimika tu kuwa mchumba ,kwa sababu za kiuchumi, kimila, kiumri kitu ambacho kinaweza zua kuwa limtu ulilokuwa nalo wala hulipendi sana na ulihusudulo halilipi.

Swali:
Si unakumbuka moja ya siri ya mafanikio ya uhusiano wa watu wawili ni TIMING?

Malengo yenu watu wawili na muda kama haviendani hatatu kwa kuwa utakaye kumjaza mimba sasa hivi yeye anafikiria kuongezea digirii mwaweza kujikuta mnanyimana ubora wa wa kukua pamoja kiuhusiano kisa tu vichwa vyenu vinalenga magoli tofauti.

NIMEACHA ila nahamu kweli nipate demu la Kibongo halafu zuriii, haliniringii mimi ila wengine lina wapa tabu kweli kwa maringo . Likilia linalia mswano, halafu linasauti nzuri kweli ya kulalamika, na likiwa na huzuni lina macho mazuri ya kuhudhunika.:-(

Umestukia ni kwanini napata tabu kupata mtu?:-)

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Mt. Simon: duh! Nina hamu kusikia umempata huyo ulonaye HAMU :-(

Sina uzoefu wa kotekote kwani WANGU wa kibongo amenipa MAUMIVU (yawezekana ni laana ya kuukimbia UKUHANI kama Mt Simon) ila duh, nahitaji kupata demu wa kizungu ili niwe na kauzoefu kengine :-(

Yasinta Ngonyani said...

nimenukuu Mt. Simon anasema"NIMEACHA ila nahamu kweli nipate demu la Kibongo halafu zuriii, haliniringii mimi ila wengine lina wapa tabu kweli kwa maringo . Likilia linalia mswano, halafu linasauti nzuri kweli ya kulalamika, na likiwa na huzuni lina macho mazuri ya kuhudhunika.:-("Mwisho wa kunukuu:- Sifa hizi, Nakutakia kila la heri. Maana naona umefia kweli hapo

Chacha wambura anasema:- Nanukuu "Sina uzoefu wa kotekote kwani WANGU wa kibongo amenipa MAUMIVU (yawezekana ni laana ya kuukimbia UKUHANI kama Mt Simon) ila duh, nahitaji kupata demu wa kizungu ili niwe na kauzoefu kengine :-(" mwisho wa kunukuu:- Mie mwananke ni mwananke:-)

MARKUS MPANGALA said...

Ambier Mtakatifu Kitururu...... na tatizo la kupata mtu lazima atataka kukulingia wewe ili ujue anachoringishia kipo sawasawa na cha liel demu la Kanada lenye likajizoa nyasa halafu likabanjuliwa lisijue hata maouno ya NDOMBOLO tatizo la tofauti ya kijiografia hata kwetu bongo ni hilohilo, sina uhakika lakini ninao na labda wahay wanaweza MITINDO HURU na pengine kushinda hata waringiacho wengine kwamba kina sumaku na biliani!

hata ukiwashwa na upup unajikuta huwezi kuparamia harage la mbeya kwakuwa halina tofauti na harage la mbalizi, cha ajabu yote mbeya.

SASA.....
ni hapo mtakatifu unapokuta tofauti za kuringishia kitabia au mengineyo za waspaniola,waswidi na wandengereko!
tatizo la kuringishiwa ni kujiona kuna mgodi wa dhaabu wakati ni tumbaku la songea halafu akiweka na fangasi za bandia a.k. nywele wanaona wamenawiri na kupendezesha mibanjuko.

ushaona wengine wanachokochoko za kinyamkera na hatua za kutongozea ilmradi wasiwe kama wazungu wengine hawa waingereza watembeao kama wanajeshi wa Lugalo. na ukikuta linyasa linakuhadhia habari za midemu ya kanada pengine ni mmoja basi anakupa stori za nchi nzima, kumbe lile gogo la kitandani ni jiwe la fatuma liliopo mbagala au TPDC.

mazingira ni tofauti na kile kitwacho tabia, lakini vinashabihiana sana.

sidhani kucha za bandia na lipustiki zinamtofautisha mzungu na mwafrika lakini makuzi ni yale ya kichoyo na umimi wa kujitosheleza bila kumtosheleza....
kalagabahooooooo

yanmaneee said...

golden goose outlet
jordan shoes
air max 270
jordan shoes
christian louboutin outlet
balenciaga speed
moncler jacket
nike air max 270
curry 5
nike shoes

Anonymous said...

bape sta
yeezy boost 380
russell westbrook shoes
yeezy 350
yeezy
a bathing ape
hermes bag outlet
air jordan shoes
giannis antetokounmpo shoes
kobe shoes