Tuesday, January 26, 2010

Kukatwa mshahara wakati ukiwa mgonjwa!!!!

Wiki iliyopita nilikuwa mgonjwa na kabla sijapona sawasawa nilikwenda kazini tena. Na wakati naumwa kulikuwa na baadhi ya marafiki kutoka nyumbani TZ, walikuwa wananitaka hali kila siku pia marafiki wengine waliojua kuwa naumwa.

Nachotaka kusema hapo ni kwamba:


Hapa Sweden kuna sheria ya kwamba ukiwa unaumwa ile siku ya kwanza ukishatoa ripoti kazini kuwa ni mgonjwa unakatwa mshahara wote wa siku ile. Siku ya pili 80% na siku ya tatu hivyo hivyo na kuendelea inategemea kama bado unaendelea kuwa mgonjwa. Kama unapata laki tatu kkwa mwezi siku ya kwanza wanakata elfu kumi na siku ya ifuatato elfu nane. Kama nilivyosema hapo juu kama utaendelea kuugua utakatwa kila siku elfu nane.


Hii ndiyo sababu nilikwanda kazini bila kupona sawasawa.

10 comments:

John Mwaipopo said...

hakika duniani sheria, haki mbinguni.

ubepari ukiwa umekolea hapo. Pole.

Bennet said...

Sheria ya kazi hapa Bongo ukiumwa siku ya kwanza ndiyo unalipwa na hizi zinazofuata hautalipwa, hii ni kwa wale wanaolipwa kwa masaa

Kwa wale wenye kuajiriwa kwa miaka mitatu (3) unaruhusiwa kuwa na siku za kuumwa 36 kwa maana ya siku moja kila mwezi, kama siku zina zidi 36 na miaka mitatu haijaisha unaanza kukatwa likizo zako, yaani kila ukitoka kuumwa unajaza fomu ya likizo

Siku za likizo nazo zikiisha basi kila siku unayoumwa unakuwa unakwatwa kwenye mshahara wako kama unapata 300,000 basi unakatwa 10,000 kila siku

chib said...

Mimi sina habari na sheria hizo. Siku ninapokuwa sipo kazini basi ujue ni likizo, off au safari ya kikazi!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ndiyo maana wameendelea hawa. Hakuna lelemama ati!

Anonymous said...

Huko Sweden basi ni wakatili hata kama ni maendeleo basi yanatafutwa pasipo kuwatendea haki wanaoleta hayo maendeleo. Anyways nchi zinatofautiana ukija North America kama umeajiriwa una haki ya siku 5-8 kwa mwaka zinaitwa sick days unalipwa kama kawaida ukimaliza siku zako basi wanaanza kukukata siku zako za likizo kama kawa unless uwe ni kibarua kwamba unalipwa kwa masaa ndio benefits kama hizo huna.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Pole sana Da Yasinta. habari ndo hiyo lakini pengine kuna mantiki

John Mwaipopo said...

kumbe hata kwetu yapo kivyengine. bennet!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante Bennet kama uko sahihi, mimi sikujua ujinga huu wa kisheria (samahani kwa neno ujinga)

ila Yasinta utakuwa unapenda sana hela kuliko afya yako!!!!!!!!!!

Anonymous said...

poleni wa2 wa sweden,hapa uk unalipwa full mshahara aslong as uwe na doctors note kusema,kuwa kweli ulikuwa mgonjwa km ni ugonjwa utakaokuweka home kwa siku zaidi ya 5,lkn siku1 au 2,unapiga cm na mshahara wako utalipwa,labda uwe kibarua.

malkiory said...

Pole sana, basi nyie majirani zetu ni wanoko. Kusema ukweli hapa Finland wanajali sana suala la ugonjwa. Kikubwa ni daktari tu akuandikie ED( Excuse from Duty) haijalishi ni siku ngapi na mshahara utalipwa kama kawaida.