Sunday, January 10, 2010

Aneth Mbilinyi: Mwanamke tajiri asiyejua kusoma wala kuandika

Aneth Mbilinyi
Asomesha watoto wake, na yeye aamua kuingia darasani
Habari hii nimeipata kutoka gazeti la Mwananchi. Na Tumaini Msowoya
Nimeipenda sana habari hii na nimeona ni vizuri niiweka hapa ili tujadali kwa pamoja.

UKITAKA kuwazungumzia wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, bila shaka hutaweza kuacha kumtaja Aneth Mbilinyi.
Mwanamke huyo ambaye ni msambazaji wa maji ya kunywa katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa, amejizolea sisa kutokana na uwezo wake wa kuendesha biashara kubwa.
Kuna msemo unaosema elimu ni ufunguo wa maisha, kwa mama huyu ni tofauti kidogo yeye hakupata elimu ya darasani lakini yeye anasema hajui kusoma wala kuandika, lakini amepata elimu ya maisha ambayo inamsaidia kuendesha shughuli zake za kila siku.
"Sijawahi kwenda shule hivyo kifupi sijui kusoma wala kuandika, lakini nina uwezo mkubwa wa kuendeleza biashara zangu. Mungu akipenda nitaanza darasa la kwanza wakati wowote,"anasema.
Anasema kabla ya kufikia mafanikio yake biashara, maisha yake yalikuwa magumu kwa sababu haikuwa rahisi kwake kupata ajira hakuwa na elimu ambayo ingemwezesha kufanya hivyo.
Aneth anasema ugumu wa maisha ulimpa changamoto hivyo akatafuta mtaji mdogo na kuanza bishara ya kukopesha vitenge ambayo aliiacha mapema kutokana na wengi kushindwa kumlipa madeni yake hivyo kuua mtaji.
Anasema baada ya kuachana na biashara hiyo alianza kusaga unga wa sembe ambapo alikuwa akiusafirisha jijini Dar es Salaam alikokuwa na wateja wengi.
Hata hivyo,biahsara ya sembe ilimshinda kwani nayo haikumpa mafanikio yoyote kitu kilichomkatisha tamaa na kuamua kuachana nayo.
Mwaka 2000 Aneth alianza kuuza maji ya kunywa ambayo alikuwa akiyafuata katika kijiji cha Kidamali kiwandani kisha kuyasambaza Iringa mjini.
"Uaminifu katika biashara ya maji uliwafanya wamiliki wa kiwanda kunipenda hivyo wakaniongezea mtaji na nikawa na uwezo wa kuyasambaza mkoa mzima, na hapo nikaanza kuona mafanikio makubwa," anasema.
Anasema kuna wakati alikuwa akipewa mzigo mkubwa wa maji unaozidi milioni 20 na kuusambaza bila hasara yoyote licha ya kuwa hawajahi kuhudhuria darasa lolote.
"Hakuna asiyejua kuhesabu hela, kamwe sijawahi kudhurumiwa kwa sababu nipo makini sana kwenye biashara zangu," anasema.
Anasema miezi sita baadaye alifanikiwa kununua gari aina ya Fuso ambalo lilimwezesha kusambaza maji kirahisi zaidi tofauti na awali alipokuwa akitumia magari ya kukodi au ya kiwanda hicho.
Kutokana na kuwa makini katika uendeshaji wa bishara zake biasharayake ilizidi kukua na akafanikiwa kushi mashas mazuri pamoja na kuwasomesha watoto wake katika shule nzuri ili wasiishi maisha ya kubahatisha kwa kukosa elimu.
"Nilijibana sana japo faida iliyokuwa ikipatikana kutokana na baishara yangu ilikuwa kubwa, malengo yalianza kutimia taratibu na mpaka sasa namshukuru Mungu kwani namimiliki mamilioni ya fedha bila kuingia darasani, anasema.
Baadaye alinunua malori mengine mawili aina ya scania kwa ajili ya kusiadia kusambazia bidhaa zake.
Mbali na mradi wa kuuza maji, Aneth anamiliki maduka ya vyombo na bidhaa nyingine huku akisema siri kubwa ya mafanikio yake ni Mungu na kujituma.
"Hakuna mafanikio yatakayokufuata mwanamke kama atakaa na kusubiri awezeshwe, lazima tukubali kufanya kazi kama watumwa ili siku moja tuishi maisha ya kifahari," anasema.
Anasema ingawa hajafikia malengo yake , lakini kwa hapo alipo anamshukuru Mungu kwani tayari amejenga nyumba za kisasa, gari kwa ajili ya usafiri na watoto wake wamesoma.
Bila elimu anawezaje?
"Nikubali nikatae, elimu ni kila kitu, napata shida kwenye kazi zangu kwani huwa nalazimika kukariri mambo kichwani ili nisikosee mahesabu, mfano mzuri ninapoenda benki," anasema.
Anasema kukariri namba na mambo mengine ya kibiashara vimekuwa vikimsaidia katika biashara zake.
Pamoja na mambo hayo, mwanamke huyo anasema amekuwa akishirikiana na mtoto wake wa kwanza ambaye amehitimu shahada ya Uchumi na bishara Chuo Kikuu cha Tumaini.
"Kwa sababu sikubahatika kusoma, wanangu nimejitahidi kuwasomesha hadi watakaposhindwa ili wasije kuishi maisha ya kubahatisha hasa wakati huu ambapo elimu inaonekana kuwa kila kitu," anasema.
Hata hivyo, anasema taasisi za fedha zinatakiwa kupunguza masharti ya mikopo ili kumwezesha mwanamke mjasiliamari kumudu kuchukua mikopo hiyo pamoja na kurejesha.
"Mara nyingi taasisi za fedha huhitaji mkopaji awe na mali isiyohamishika kama nyumba ama hati ya kiwanja, sharti hili ni gumu kwa wanawake walio wengi jambo ambalo huwakatisha tamaa wanawake kuchukua mikopo," anasema.
Anasema alifanikiwa katika biashara yake kwa sababu kiwanda kilimuamini na kuanza kumpa bidhaa kwa kumkopesha, lakini kama isingekuwa hivyo hali ingekuwa tofauti kutokana na ugumu wa mashari ya mikopo.
Anaongeza kuwa taasisi za fedha zina wajibu wa kutoa elimu kwa wanawake wajasiliamari ili kuwawezesha wanawake hao kutambua faida na hasara ya biashara zao.

16 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

kwa taarifa yenu: si lazima uwe umesoma ndo uwe tajiri. In fact ukitaka kuwa tajiri (bila shortcuts) unaweza na ukitaka kuendelea kuwa hohehahe a.k.a masikini utakuwa tu...uamuzi ni wako dugu...:-(

kuna tajiri mmoja hapo mjini mwanza ambaye alianza kwa kuuza karanga na sasa anamiliki biashara ambayo imesambaa mpaka zimbabwe! na hana shule uelewe...so?

The verdict is yours.

chib said...

Da Mija huwa hawa ndio anawaita akina mama wa shoka

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

na anapaswa kuingia katika list yake!

EDNA said...

Everybody is good at something, Mungu hakunyimi vyote bwana!!Ugumu wa maisha tunaopitia ni shule tosha na inatufanya kuwa wabunifu.Kwa maaisha ya sasa tumekuwa na tafsiri ya kwamba ili ufanikiwe unahitaji elimu kwanza,Swali je ni wangapi wanadegree na wapo mitaani wakihangaika kupata ajira? Yote kwa yote ELIMU MUHIMU nenda kasome angalau ujue hata kusoma.

Bennet said...

Huyu Mama kilichomsaidia ni moyo wa kujituma na uaminifu kwenye biashara, pia nafikiri ana kitu kinaitwa customer care skills ambazo pia hakufundisha popote darasani bali ni malezi aliyopata toka kwa wazazi na walezi wake

Mija Shija Sayi said...

Mama Janeth ni kiboko yetu, hiyo tukubali tusikubali. Wadau hivi mmeshagundua kwamba watu wanaojua sana mambo a.k.a wasomi huwa ni ngumu sana kufanya mambo makubwa tofauti na wasio wasomi, hii ni kwa sababu msomi anapoteza muda wake mwingi kutafakari jinsi ya kulifanya jambo wakati asiye msomi akipata wazo tu, hapotezi muda analifanyia kazi. Matokeo yake muda unazidi kupita huku mwenzake anaendelea kuzalisha. Ndiyo ya huyu mama.

Mfano mzuri angalia wasanii wanaotamba Bongo, wengi wao hawana hata mafunzo ya sanaa lakini wameamua kupambana mbele kwa mbele, sasa akina siye wenye hadi stashahada za sanaa kazi ni kukosoa tuuu, hapo hakutakiwa kufanya hivi.. vile.., muda unakwenda kina kanumba wanazidi kupeta.

All in all, humu mama nimeshamuingiza kwenye list yangu kanitia moyo sana.

@Chacha Ng'anambiti point uliyoongea hata Dolly Parton kaiimba kwenye wimbo wake wa Coat of many colours... anasema.."But they didn't understand it
And I tried to make them see
That one is only poor
Only if they choose to be"...

Haya kazi kwetu wadau maisha ni kujituma.

Yasinta Ngonyani said...

Ngoja niulize shwari moja kwa hiyo kusoma sana ni kupoteza muda bure?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Yasinta: nadhani haimaanishi kuwa yeyote anayesoma sana anapoteza muda bali malengo. Inategemea unataka kuwa nani katika maisha.

Mara nyingi tunawalea wanetu wawe kama sisi; madaktari, manesi, mainjinia, wahasibu nk. Na kinachouma zaidi ni kuweka mbele maslahi a.k.a hela mbele zaidi ya utu kwa maana kuwa tunawachagulia watoto taaluma ambayo inalipa kwa muda mfupi kama uwakili, uhasibu nk.

na wakati mwingine tunadharau taaluma nyingine...mtoto akifeli fom fooo utamsikia mzazi anadai 'yaani hata ualimu umishindwa?' kana kwamba ualimu ni taaluma ama kazi ya waloshindwa :-(

Cha muhimu ni ntoto anasoma ili awe nani....! Yaa ni achague kile akipendacho yeye mwenyewe

Yasinta Ngonyani said...

Chacha Wambura una uhakika kwamba kuna wazazi wangapi wanaacha watoto wao wachugua nani wanataka kuwa? Kwani mara nyingi nimeona wazazi wanataka watoto wao wawe kama wao na akibidi zaidi. Nina mfano mmoja kuma wazazi hapa wanawafanyisha watoto wao mazoezi ya mpira nk kwa vile yeye alitaka kuwa na hii ndoto na ameshindwa kwa hiyo sasa anataka mtoto awe kama yeye alivyokuwa ameota alivyokuwa mdogo. Je hii ni haki kweli katika maisha?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Yasinta et al: ukweli nadhani umeshaupata. pengine hata huyo mbaba unayemsema naye alifuata ndoto za kuwa mwanasoka kwa kuwa mzazi wake naye alikuwa anam-encourage kuwa mwanasoka.

yawezekana nawe unataka aidha wanao wawe watawa ama wawe hiyo kazi unayofanya..lol

Yasinta Ngonyani said...

Kuna watu wengi hawataki kujaribu kuufanya kama huyu dada/mama wanasahau kuwa, wakati mwingine hata kusoma haina maana sana kama huna juhudi ingawa ni kweli elimu muhimu. Kwani wanafikiri kufanikiwa ni lazima kusoma na kuwa na elimu ya ju. Ningekuwa na uwezo ningewuomba huye dada apite vijijini na kuwwelewesha wengine jinsi ya kufanikiwa sio lazima kujua kusoma na kuaandika na kuwa wasikate tamaa mapema.

Mija Shija Sayi said...

Kusoma + Juhudi + Kujaribu = Mafanikio.

Kusoma pekee bila juhudi na kujaribu ni ngumu kufanikiwa, hapa ninajibu swali la Yasinta juu ya kusoma sana ni kupoteza muda bure.

Tupo pamoja katika mjadala.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Da Mija: Yawezekana Kusoma + Juhudi + Kujaribu = Kufeli a.k.a kutofanikiwa :-(

Kuna ka msemo kanadai hivi: if you can dream it you can make it. Wangapi tuna ndoto fulani ambazo tunataka tuzitimize? Je kama tunazo do we cling unto them? au tukianguka tu tunachanganyikiwa?

tuna uwezo wa kuwa chochote hata Da Mija akitaka kuwa Rais wa nji yetu hii anaweza ;-)

Anonymous said...

Yasinta rudia kusoma comment zako, kuna comment moja umetukana hapo!! zisome tu utaikuta moja ina tusi kubwa linalokusu kwani umetaja kiungo kimoja du!!

Anonymous said...

Yasinta wakati mwingine upo sahihi maana hata tajiri aliyekuwa anashika nafasi ya kwanza kwa utajiri tanznia Salim Said bakharesa hakusoma aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanza kuuza urojo zanzibar , akaweka akiba baadae akafungua mgahawa , aliendelea kudunduliza mpk akafikia alipofikia naamin ni malengo ya kuwa na ndoto kubwa na juhudi.

Anonymous said...

Unyama sana