Friday, January 29, 2010

Napenda kuwatakia mwema wa juma hili pia ijumaa ya mwisho ya mwezi huu wa kwanza!!

Kunywa lakini kumbuka pombe si maji (na kumbuka kama utaendesha usinywe ugimbi mwingi)

Wazee na vijana wa kijiji cha kibaa wakicheza bao kama sehemu ya kupoteza muda baada ya kumaliza kazi.
Au ngoja tumsikilize Dada Saida Karoli ili wenye kuselebuka

Muwe na wakati mzuri wote

15 comments:

Faith S Hilary said...

Eh...vile ni ijumaa ya mwisho wa mwezi...yaani siku zinaenda kama upepo!! hata huzioni!!! hehe

Asante kwa nyimbo hiyo..naweza kuisikiliza kila mara na wala siuchoki kabisa.

Simon Kitururu said...

Kwako pia Dada Mpendwa!

Simon Kitururu said...

Samahani! unauhakika gani hao wazee katika picha ya pili walienda kazini?

Yasinta Ngonyani said...

Candy1! Ni kweli siku zimepepea kama nini juzi tu nilitimiza miaka leo mwezi tayari ushaisha... Candy1! huu wimbo mwenzangu ninavyoupenda leo hii ninamaumivu ya kicha lakini we acha tu nimecheza...mpaka kijasho.

Simon mt. Asante kakangu!
Simon! nina uhakika kwani kazi ni kazi hata kuwa kirabuni ni moja ya kazi au hata kushinda hapo na kucheza hiyo bao hapo kutwa yote ni moja ya kazi sio lazima kuwa ofisini au?

malkiory said...

UMKOMBOTHI HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

Unknown said...

Dada You have made my day

EDNA said...

Weekend njema kwako pia.....Huyo mzee anakunywa ulanzi au Komoni?

John Mwaipopo said...

yasinta mambo ya kutukumbusha komoni jamani. ngoja leo niende kilabuni nikagonge japo lita moja hivi. hii picha inantoa udenda ati!!

chib said...

Huyo Mzee anafanana na wachagga, na hiyo chubuku na kofia. I bet ni mchagga.
Weekend njema dada

mumyhery said...

shukran na kwako pia

Anonymous said...

Unanikumbusha mbali mpaka vilabu Matetereka na Madaba.

Anonymous said...

Sasa nakumbuka vilabu Matetereka na Madaba.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Mt. Simon: hiyo kazi wanayoifanya hao wazee nayo ni muhimu ati :-(

Nimependa huyo mzee hicho anachochangamkia...imenikumbusha Shirimatunda enzi hizo tunatoroka shule pale Moshi Technical - Karanga kwenda kupata 'kitochi' kimoja :-)

PASSION4FASHION.TZ said...

Dada ana sauti nzuri sana huyu,ila huo uchezaji wa wenzetu inabidi uwe umekula matoke ya nguvu,maana inahitaji uwe mkakamavu.

Anonymous said...

weee dada Yasinta, mwenu inywa kindi, komoni, ulai au myakaya? Akimaliza hiyo ataanza kuimba: a teresia wiganda, wiganda gani mbona wilya, unakula maganda ndizi bado za wenyewe.
Blog yako huwa inanikumbusha kweli ungoni... MAKI