Thursday, January 28, 2010

HATUA MUHIMU KATIKA MAKUZI YA MTOTO

Katika udadisi wangu nikawa nimepitia blog ya http://kaluse.blogspot.com/ na kukuta makala hii na nikashidwa kuiacha kwa vile najua wote katika hizi blog lengo letu ni moja kuelimisha jamii.

Hivi umeshawahi kujiuliza hata siku moja, kwa nini watu wengine ni walevi? Wengine waongeaji sana? Wengine wakimya sana? Wengine waongo sana? Wengine wana tamaa ya ngono kupita kiasi na kadhalika? Lakini pengine una maswali mengi ya namna hii ambayo yanaonyesha jinsi wanadamu wanavyotofautiana.

Kuna hatua 5 muhimu ambazo mtoto lazima afanye mambo ambayo yanastahili kufanyika katika hatua husika. Na iwapo hayatafanyika, hali hizo huhifadhiwa katika mawazo yake ya kina na hivyo kumsababishia matatizo makubwa ukubwani.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-

Hatua ya kwanza – oral stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia siku moja mpaka miaka miwili. Katika hatua hii ya kwanza, furaha na raha ya mtoto huwa imejificha mdomoni. Utakuta mtoto kila wakati anafurahia kunyonya maziwa ya mama yake, vidole au midoli. Mtoto anatakiwa atumie mdomo wake mpaka ile hamu yake yote iishe. Kama ni kunyonya basi aendelee kufanya hivyo mpaka pale utakapofika wakati mzuri wa kumwachisha ziwa. Kumnyanyasa mtoto wakati ananyonya au kumfanyia vitendo ambavyo si vya kiungwana ikiwa ni pamoja na kumwachisha ziwa mapema, husababisha hamu yake ya kuutumia mdomo ibaki na hivyo kuhifadhiwa kwenye mawazo yake ya kina. Anapokuwa mtu mkubwa hulipa kisasi bila kujua kwa kuutumia mdomo kwa kadri anavyoweza. Hivyo anapokuwa mtu mkubwa anaweza akawa muongo sana, mlevi kupindukia, mvuta sigara sana, muongeaji sana, au mmbeya sana. Kama kuna watu unawafahamu wenye tabia hizi, jaribu kupeleleza kama walinyonyeshwa bila kunyanyaswa au kama hamu yao ya kunyonya iliisha.

Hatua ya pili – anal stage: Hatua hii humhusu mtoto wa miaka miwili au mitatu. Matumizi ya mdomo huwa yamekwisha na raha huhamia sehemu za haja. Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia au jinsi ya kutumia choo. Kinyume na hivyo ni kumfanya mtoto awe na tabia ya kujifanyisha na hivyo kuwa na hali mbaya ukubwani. Mtoto aliyenyimwa huduma hii akiwa katika hatua hiyo hubakiwa na deni, anapokuwa mkubwa anaweza kupata matatizo ya kiakili. Watoto waliokosa huduma hiyo wanapokuwa wakubwa, mara nyingi huwa mashoga, na wengine huwa waoga kufanya mapenzi, lakini mbaya zaidi ni kukosa kabisa hamu ya mapenzi, wengine huwa wazembe na huwa na tabia fulani fulani ambazo zinahitaji msaada mkubwa wa wengine.

Hatua ya tatu – phallic stage: Hatua hii huwahusu watoto wenye umri wa miaka minne. Ni katika hatua hii ambapo mtoto huanza kutambua jinsia yake na hivyo kuwa karibu na mama yake au baba yake. Mtoto wa kiume hupenda kulala na mama yake na mtoto wa kike pia huwa hivyo hivyo hupenda kulala na baba yake (interest of opposite sex). Mtoto wa kiume humchukia baba yake bila kujua na kumuonea wivu mama yake na kuona kama anamfaidi baba yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake, pia mtoto wa kike humchukia baba yake na kumuonea wivu baba yake na kuona kama anamfaidi mama yake jambo ambalo hulitaka liwe kwake. Watoto waliokosa kuwa karibu na wazazi wao wa jinsia tofauti katika hatua hii, wengi hupata matatizo, lakini hulipiza kisasi kwa sababu hawakuwa karibu na jinsia tofauti wanapohitaji kufanya hivyo. Usishangae kumkuta binti akiwa kwenye kundi la wavulana au mvulana akiwa kwenye kundi la wasichana.

Hatua ya nne – latency stage: Hatua hii huwahusu watoto wa miaka sita, minane na wakati mwigine mpaka miaka 12, ambapo mtoto macho yake yote huwa katika michezo ya kawaida na kwenda shule. Hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika hatua hii kati ya jinsia ya kike na ya kiume.

Hatua ya tano - genital stage: Hatua hii huwahusu watoto wa kuanzia miaka 13. katika kipindi hiki vijana wengi huanza kubalehe na kuvunja ungo. Katika hatua hii ndipo mtu hukabiliwa na vitu vingi katika maisha yake yote. Huanza kujishuhulisha na kutafuta maisha yake mwenyewe na ndipo hatua nyingine zote huanza kujirudia tena kama hazikufanywa vizuri katika umri huo. Raha ya mwanadamu yoyote katika kipindi hiki huwa ni mapenzi, lakini hutofautiana kiwango cha kupenda au kutamani kutokana na jinsi alivyolelewa katika hatua nne za mwanzo. Nakuomba sana kila unapokutana na watu waongo, wambeya, wakimya, wapenda ngono kupita kiasi n.k. waulize maisha yao ya utotoni.

11 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hatua ya pili bado inanitatiza kidogo kwa ufupi sielewi labda nipewe mfano.

Nanukuu..,
Katika hatua hii, mtoto hupendelea zaidi kutumia sehemu zake za haja kwa kukojoa au kwenda haja kubwa mara kwa mara. Katika kipindi hiki wazazi wengi hufanya makosa. Mzazi anashauriwa kuwa makini kwa kutoa mafunzo mazuri kwa mtoto wake, kumfundisha jinsi ya kujisaidia...

Aliyeelewa naomba anisaidie. Ina maana kabla ya hatua hii mtoto hutumia njia gani kujisaidia, na mzazi unamfundishaje mtoto kujisaidia?

Majaliwa said...

Hii ni poa sana!Ingawaje sijabahatika kuwa na mtoto,nasema asante dada Yasinta.

MARKUS MPANGALA said...

NITAJIFUNZA PALE NITAKAPOZAA LITOTO LENYE JINA LA MWANA BLOGU MWENYE MAKEKE YA FULANI YA.... HALAFU NITAANZA KUJIFUNZA KULEA MTOTO KAMA VILE LITOTO LA KIGOGO LAKINI SITAKI LIWE FISADI.

LAKINI MALEZI YA ERIK NA CAMILLA, naona adabu imekuwa bomba la miakili, sijui kama kweli baba yake na mama yake walilelewa kwayo.
unaweza kuzaa na kulea halafu ukashindwa kumudu kukuza kwa kupitia hatua hizohizo.

wanautambuzi wanadai mtoto anazotaarifa nyingi kuhusu maisha yako Yasinta hivi unawasoma wao kama wanakupatia bomba la miakili ya kumpiga chenga shetani asikupitie halafu mzee matetereka anashtukia dili nawe uombe radhiiiii weweeeee SHETANI ALINIPITIA.

hivi kitu gani kinaonyesha hayo ni ukuzi wa watoto? labda sijaelewa. ngoja nikizaa nitajifunza kulea...Lol

malkiory said...

Unajua mimi ni mojawapo wa walevi kama ulivyosema, lakini kama mtaalamu aliyebobea katika maswala ya elimu, nisingependa huu mjadala ufikie kilele bila kumgusia mwanasaikololojia aliyebobea katika makuzi ya watoto, si mwingine bali ni JEAN PIAGET.

malkiory said...

Samahanini wadau, sehemu ya posti yangu naona haijawa posted, nilichotaka kusema ni kwamba kwa wale wadau ambao hawajawahi kumsikinki JEAN PIAGET basi wajaribu kuli google majina yake kama nilivyoyataja hapo. Ni matumaini yangu kuwa baada ya kusoma nadharia za Jean Piaget tutaweza kupata elimu kuhusu hatua muhimu ambazo watoto hupitia toka tu anapozaliwa hadi anapofika utu uzima. Hongera dada kwa kulichokonoa hili li mada. Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto wetu.

Unknown said...

Ahsante kaka Malkiory kwa mchanganuo mzuri, nitajaribu kumsoma huyo gwiji na mwanasaikolojia wa makuzi ya watoto ndugu Jean Piaget.

Mimi ndiye mwandishi wa hii mada na ilikuwa ndio makala zangu za mwanzo kabisa kubandika pale kibarazani kwangu wakati nilipoanza kublog, nasikitika kuwa mjadala huo haukushika kasi na kupata changamoto kama aliyotoa dada Mija Shija Sayi.
Naamini inawezekana ni kutokana na ugeni wa blog na ndio maana mada hii ilipita bila kupata changamoto.

Namshukuru dada yangu Yasinta Ngonyani kwa kupekua na kuurudisha mjadala huu katika tasnia ya blog, na hivyo kupata changamoto ambazo inabidi nizifanyie kazi.

Dada Mija, kwanza nakupa heshima yako, labda ili kujibu swali lako, ningependa kukiri kuwa mada hii niliitoa katika vyanzo mbalimbali mtandaoni, na kama unavyojua kuwa lugha inayotumika katika mada za kisaikolojia ni ya kiingereza, hivyo unalazimika kutafsiri katika lugha ya kiswahili na nyepesi ili wasomaji waweze kuelewa.

Wakati mwingine nakutana na misamiati migumu ambapo hata kamusi ya kiswahili inakuwa ni vigumu kupata tafsiri sahihi, lakini hata hivyo nafurahi kusema kuwa namudu kufikisha ujumbe.

Dada Mija katika kipengele ulichokinukuu, nadhani kulikuwa na mgongano wa lugha. Lakini kuweka mjadala huu vizuri ni kwamba nilikuwa namaanisha kuwa katika hatua hiyo mtoto hufanya udadisi sana na viungo vyake vya kujisaidia, yaani cha haja kubwa na ndogo, huo ndio wakati mzuri wa mzazi kumfundisha mtoto namna ya kujisaidia.

Naamni maelezo yangu yanaweza kujibu swali lako, na kama kuna changamoto nyingine nazikaribisha, kwani huu ndio wakati wa kueleimishana.

Mija Shija Sayi said...

Asante kaka Kaluse kwa maelezo nimekuelewa kuhusu mambo ya tafsiri. Lakini hebu tuliweke jambo jili bayana tunapoongelea kumfundisha mtoto kujisaidia tunamaana ya kwamba msichana achuchumae akikojoa na mvulana kusimama au tuna maana kumfundisha mtoto kazi za viungo vyake yaani kipi ni cha haja kubwa na kipi ni cha haja ndogo?

Sijui kwa nini, lakini naona kama maelezo hayajakamilika halafu mbaya zaidi nashindwa kuhisi unalenga wapi. Tusaidiane kwa mifano jamani.

Halafu nadhani mada hii inamhusu Maiko Jackson kwa njia moja au nyingine.

Unknown said...

Dada mija uko sahihi kabisa, ni kweli maelezo yangu hayakukamilika.
kama ulivyosema kuwa ni kumfundisha mtoto namna ya kujisaidia yaaani kwa mtoto wa kike kuchutama na wa kiume kusimama, na pia ni vyema akafahamu tofauti ya viungo hivyo viwili katika matumizi na umuhimu wake.

mambo mengine mtoto atafundishwa kulingana na umri, lakini kwa kuwa watoto wa siku hizi ni wadadisi, naamini ni vyema wakaelekezwa vizuri na kwa uwazi lakini kwa tahadhari asije akajaribu mambo mengine kabla ya muda wake.

namini mpaka sasa maelezo yangu yamekamilika.

cytotec said...

obat telat bulan i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat cytotec

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

Unknown said...

Hatua hii humtaka mzazi amwelekeze motto wake namna ya kutumia choo....kwa kuzingatia kumaliza haja yote na siyo kuwa anaenda mara kwa Mara....