Thursday, January 14, 2010

Mitindo tofauti ya kuonyesha hasira

Ana hasira

Hebu fikiria kuhusu mwanao huyu. Wamekuja wageni nyumbani kwenu na unamwambia mwanao awaletee wageni kinywaji. Ukweli ni kwamba hakuna vinywaji huko kwenye jokofu. Badala ya kukuita pembeni na kukueleza hali halisi, mwanao huyo ambaye ni mkubwa kiumri, anakuelewa hapo hapo mbele ya wageni kwamba, hakuna vinywaji. Je, utafanyaje baada ya hatua hiyo?

Kwa sehemu kubwa, baada ya kukerwa kwa kwa namna hiyo, uwezekano ni kuchukua hatua moja kati ya hizi tatu zifuatazo. Hii ina maana kwamba, huwa tunaonyesha hasira zetu kwa njia kuu tatu. Kuna kukasirika, ambako hufuatwa na utulivu baada ya mkasirikaji kukagua na kufanya tathmini ya mazingira. Baada ya kutathmini huko, mkasirikaji huamua kuahirisha hasira zake hadi pale mazingira yatakaporuhusu. Kwenye huu mfano wetu, mkasirikaji atasubiri wageni waondoke ndipo amkaripie mwanaye.

Bila shaka hata wewe (kwa kutegemea malezi au kiwango chako cha hasira) umeshawahi kuahirisha hasira. Kama siyo wewe, umewahi kuona mtu akiahirisha hasira. Mara nyingi wanandoa wenye busara wanapokuwa kwenye hali ya hasira na akaingia mgeni huwa wanaahirisha hasira zao.

Kuna kukasirika ambako hakuangalii mazingira. Mtu huonyesha hasira zake popote na kufanya mambo ya ajabu mahali ambapo kamwe asingetarajiwa kufanya hivyo. Mtu kishakasirika anaropoka au kufanya mambo mengine yenye kufedhehesha sana. Hapa mkasirikaji hajali matokeo ya kauli na vitendo vyake vya hasira.

Kuna kukasirika ambako kila mtu anweza kubaini kwamba fulani amekasirika, lakini mtu huyo aliyekasirika hatoi kauli wala kutenda jambo lolote lenye kuonyesha kukasirika. Pamoja na ukweli kwamba, kuna kila dalili kuwa mtu amekasirika, hafanyi au kutoa lkauli yoyote yenyewe kuthibitisha kukasirika kwake. Hata kama atatoa kauli yoyote itakuwa tu ni ya kuonyesha kukereka bila kutoa maneno makali.


Kuna wale ambao wanapokasirika hulia sana, huvunja vifaa, hupiga ngumi ukutani au hupiga mateke hovyo. Ni kwa kufanya hivyo tu, ndipo hasira zao zinapopungua au kwisha. Lakini wapo ambao wanapokasirika hucheka sana, badala ya kununa au kulia. Wanapomaliza kucheka hununa ghafla na hapo hufanya chochote.

Ni wazi kila mmoja kati yetu anayo namna yake ya kuonyesha hasira, ingawa hata hivyo uonyeshaji huo hutegemea hali na mazingira tofauti. Je, ni nani aliyemuudhi mtu, wapi, kwa sababu ipi na mengine. Lakini bado ukweli unabaki palepale kwamba, mara nyingi namna ya mtu kuonyesha hasira yake huwa ni ileile bila kujali mazingira au hali.

Makala hii nimeichukua kutoka kwenye kitabu cha Maisha na Mafanikio kilichoandikwa na Hayati Munga Tehenan ambaye alikuwa ni Mwalimu mzuri wa maarifa ya Utambuzi akitoa elimu hiyo kupitia magazeti yake ya Jitambue, vitabu na semina zake nchini Tanzania kabla ya kufariki dunia

12 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Yasinta: weye uko kundi gani kati ya hayo matatu?

na wale akina Koero ambao wakiudhika kidogo wanazira wako kundi gani katika hayo matatu?

Unadhani hasira ni nzuri ama ni ujinga?

Ngoja niende kwanza labda naweza kurudi na majibu...lol

Simon Kitururu said...

Nukuu ``Hebu fikiria kuhusu mwanao huyu. Wamekuja wageni nyumbani kwenu na unamwambia mwanao awaletee wageni kinywaji. Ukweli ni kwamba hakuna vinywaji huko kwenye jokofu. Badala ya kukuita pembeni na kukueleza hali halisi, mwanao huyo ambaye ni mkubwa kiumri, anakuelewa hapo hapo mbele ya wageni kwamba, hakuna vinywaji. Je, utafanyaje baada ya hatua hiyo?´´ sijui kwanini sielewi mfano huu kwa kuwa sioni katika hili ni nini cha kumkasirisha mtu.

Nachojaribu kusema.

Moja- Watu tunatofautiana.


Pili- Mimi naamini watu wengi huonyesha hasira kwa asiye mhusika kwa kawaida.

Nikiwa na maana - Mwalimu aliyekasirishwa nyumbani hasira zake kirahisi huenda kwa wanafunzi wake na Mzazi aliyekorofishwa kazini hahitaji akorofishwe sana nyumbani kumkaripia mwanawe na hiyo ni moja wapo ya kitu kinachonisaidia kuelewa mfano huo hapo juu wa Mzazi kuelezwa ukweli vinywaji hakuna halafu iwe nongwa.

Ni mtazamo tu wangu !

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

@Mt. Simon: sina hakika unachojaribu kusema ni kuwa kuna baadhi yetu tuna kitu kiitwacho hasira za mkizi.

kwa maana ya kuwa tuko rahisi sana kuchokozeka kihisia kiasi kwamba kitu kidogo tu tunalipuka. Kwa msingi huo mara nyingi huwa tunaingia katika migogoro ya kifamilia na kutokuelewana kati ya ndugu, marafiki na majamaa.

lakini nini suluhisho la hali kama hizo?

Simon Kitururu said...

@Kadinali Ng'wanambiti: Dawa ya hasira za mkizi ni KUFIKIRIA kwanza.


Kwa kufikiria kwanza mtu atastukia duniani kuna vichache sana vya kumkasirisha mtu. Anaweza hata kugundua matusi kama

-Mbwa weee!

-Sura kama tako !

Wala sio matusi.:-(


Ila kukasirika ni afya na naamini ni moja ya kitu muhimu sana kwa binadamu ili awe binadamu.

Cha kusikitisha ni udhaifu wa nini binadamu wanachagua kuvikasirikia.

Ila fashenni ya kukasirikia CCM au tu Wanasiasa huwa najikuta hatamie inaninogea.:-(

Nachoshauri lakini ni kwa mtu kukasikia kinacho wakasirisha. Sio tu umechacha siku ya Hepibesidei ya mtoto kwa hasira unaanza kukasirikia alivyofeli mitihani mwaka jana mtoto.

Au bosi kakukasirisha na hasira zote unaliamishia kwa mama watoto nyumbani na kususa chakula cha usiku kwa kuwa anachelewa kuvua gwaguro.:-(

Kwa kifupi HABARI ndio HIYO!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Chacha Wambura mimi sipo katika kundi lolote hapo mimi ni yule mtu mwenye hasira za haraka sana na haziishi haraka. Yaani napatwa na hasira bila kujijua na pia huwa sipendi kuwa na mtu wala kusema na mtu wala kula nataka niwe mimi tu. Nimeanza kufikiria kama kweli nipo sawasaw au vipi? Nadhani hii ndio sababu nimeandika hii mada hapa kupata majibu.

Mt.Simon!Mifano yako ni kweli kabisa na yaani mtu unapata hasira kazini na zinaishia kwa watoto au mume au kinyume nyumbani na zinaishia kwa wafanyakazi wengine. Na pia nimesoma katika kitabu hiki cha maisha na mafanikio ni kwamba. Nanukuu " Kuna maelezo ya kitafiti kutoka nchini India ambayo yaonyesha kwamba, akina mama walio kwenye hasira kali waliwahi kuwauwa watoto wao wadogo, baada ya kuwanyonyesha wakiwa kwenye hali hiyo (Hasira kali) Inaelezwa kwamba, hii ilitokana na ukweli kuwa hasira hizo zilisababisha sumu kwenye mfumo wa damu na kuharibu maziwa".

chib said...

Inategemea na mazoea, iwapo unapenda kutuma mtu a huku unajua ulimchomtuma hakipo unategemea nini. Fikiria mgeni wako ni Mtakatifu, unaagiza kwa sauti lete bia bariiiidi kabisa ilhali jokofu lipo patupu, anaweza kukukomesha kwa kukujibu mbele ya mtakatifu akionyesha hasira yake kistaarabu

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Mkuu Chib: duh! Kwa Mt patakuwa haatoshi :-(

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta nakushukuru kwa mada hii. Pia ni bora nimechelewa kutoa maoni ili walionitangulia waseme waliyoyasema. Kimsingi hasira hutofautiana. Nikijitolea mfano mimi mwenyewe, nina hasira kwa kiwango fulani, lakini huwa ninaahirisha hasira mara nyingi kama mazingira hayaruhusu hususani kunapokuwa na watu wengi.
Lakini nikishafanikiwa kuziahirisha hasira hizo huwa najikuta nimeamua kupuuzia na hivyo mahusiano na mtu aliyenitia hasira yakaendelea kuwa mazuri. Kama jambo hilo nadhani lina athari basi nitamwambia kwa hali nzuri. Kama halina, nitaamua kupotezea.
Lakini nakiri kuna nyakati huweza kutokea ustahimilivu ukanishinda, basi humvuta mhusika pembeni muda huohuo na kumwambia short and clear "Umenikwaza" akichukia asipochukia kwangu imetoka, na hasira imeshuka.
Ni hayo tu.

Yasinta Ngonyani said...

Mtani Fadhy! ipo kazi naona karibu tunalingani ila mwenzangu afadhali mie inawezekana ikatimia mwezi bila kusema na yule niliyemkasirikia.

Markus Mpangala. said...

swali>< @la nakukumbusha? JE SIKU ILE ULIPOBANJA PAAAAAAAAA HALAFU NIKAMWAMBIA ERIK MLETEE MAMA YAKO BAKULI TUKINGE, ULIKASIRIKA? ha ha ha ha ha DONGO LA MWAKA HILOOOO UNALO LEO MCHARUKOOOOOOOOO HUO H ha ha ha ha ha ha ha.

kabala hujakasirika mtu unatakiwa kufikiria kama asemavyo MTAKATIFI KITURURU

Mija Shija Sayi said...

Da Yasinta umenikumbusha yule dada yako aliyekunyima kanga...lol

Makala safi sana imenikumbusha nikikasirika ninavyopata Migrane.

Yasinta Ngonyani said...

Da Mija! we acha tu yule dada basi tu.
Na pia nafurahi kusikia kumbe tupo wengi.