Friday, January 15, 2010

HILI LIMENITATIZA, NAOMBA MSAADA WENU

Habari zenu wanablogu na wasomaji wa blogu hii. Kama wengi waniitavyo Kapulya kutokana na maswali yangu niwaulizayo.

Ni juzi juzi tu nilikuwa naongea na rafiki mmoja wa nyumbani Tanzania. Akaniambia kuwa atakuwa off (hatafanya kazi kwa muda wa siku kadhaa) kwa vile alifanya kazi wakati wa sikukuu. Nikamuuliza kama zile siku za sikukuu alizofanya kazi hakulipwa? Akanijibu hakulipwa. Nilishangaa sana na nikaona kweli dunia ni ya ajabu kwani hapa Sweden mtu kama unafanya kazi siku za sikukuu mshahara unaongezeka yaani kama unapata 100kr kwa saa basi utapata 200kr kwa saa.

Na mimi nilikuwa nafikiri sheria hii ipo sehemu zote ulimwenguni. Swali langu ni hili je? hii sheria ya kutolipwa wakati wa sikukuu TZ tu na kama ipo je? ni kwa wafanyakazi gani? nina maana hata wafanyao kazi serikalini?

8 comments:

Simon said...

bwana wee, hapa Tanzania mambo yanavyoenda ni shaghara baghara tu, hakuna usimamizi wa maana wa serikali kuhusu mambo kama haya ya mafao ya watu na vitu kama hivyo, matokeo yake ni kuwa wananchi ndio wanaonyanyaswa tu, na hii ni kwa wafanyakazi wale wa kima cha chini;maofisa tena serikalini huko..aje siku ya sikukuu ofisini..hela atakayo lipwa ni balaa; mbunge au waziri aingie ofisini siku ya sikukuu..hizo allowance atakazoondoka nazo(i.e payee zetu)ni aibu!!!`

Baraka Mfunguo said...

Sheria ya kazi Tanzania iliyofanyiwa marekebisho na kuboreshwa kwa kuongezewa baadhi ya vipengele mwaka 2004, inafafanua kwamba kila mfanyakazi anawajibika kufanya kazi muda wa masaa 45 kwa wiki, masaa 9 kwa siku na siku 6 kwa wiki. Sasa sheria inaweka makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa kwamba mwajiriwa anaweza kufanya kazi kwa masaa mengi bila kupata posho lakini akafidiwa masaa yake ya kazi kwa kupumzika ama kufanya masaa pungufu. Kimombo inaitwa "compressed working Week" Mfano siku ya kwanza amefanya masaa 12, siku ya pili masaa 12, siku ya tatu masaa 12, siku ya nne inapungua masaa 6. Hivyo hivyo.

Kwa ufafanuzi mzuri unaweza kupitia sheria ya kazi na mahusiano ya Tanzania ya mwaka 2004.

HERI YA MWAKA MPYA.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

sijawahi kufanya kazi serikalini ila nimejiajiri hivo ntafikiria nikiwa na wafanyikazi kuwapa tusenti kidogo wakati wa sikukuuu...lol

Markus Mpangala. said...

WAFANYAKAZI TUSAIDIENI

Markus Mpangala. said...

OOOHH SMAHANI NIPO BIZE NA MCIHUANO HUKO angola

nyahbingi worrior. said...

Kwa mtazamo wangu.

Binadamu tunapenda kuweka pesa mbela kuliko maendeleao.Katika nchi kama hii ya dunia ya tatu ni heri kufanya kazi siku zote na bila kulipwa hadi pale maendeleo yatakapo patikana.

Bennet said...

Kama unalipwa kwa masaa basi siku ya sikukuu inakuwa mara mbili, kama unalipwa mshahara wa kawaida yaani sio kwa masaa basi utajaza form (overtime claim form) pia unaweza kupewa off kama huyo jamaa kufidia siku uliyofanya kazi (sikukuu) lakini pia kuna malipo yanaitwa shift allowance ambayo utalipwa kwa kuwa kazini sikuhiyo ingawa bado watakufidia kwa kukupa off zaidi

Anonymous said...

Samahani kama nimechelewa kujibu mjadala huu lakini mimi kama mwajiri Tanzania napenda kujibu kwa wazi kabisa. Kwanza sehemu kubwa watanzania hatufanyi kazi kwa juhudi. Level ya uvivu iliyopo kwa kweli inatisha. Wakati huo huo kuna madai kibao. Mimi nimeshirikiana na marafiki hapa marekani kuanzisha shule (www.maguschool.org) kwa kweli walimu kila siku wao ni watu wa kudai tuu mafao na overtime bila hata kuangalia mchango wao nini. Shule hii ipo kijijini na lengo kubwa ni kusaidia vijana wapate elimu lakini unaona walimu wanataka kila siku waondoke na kila siku wapewe chai na chakula cha mchana. Ukiwambia wachangie vitu hivyo wanakuja juu.
Nakubaliana nchi ya tanzania ni masikini sana sasa tukitaka kila kitu kiwe kama ilivyo swedeni au ujerumani hatufiki. Lazima kuwe na sacrife fulani ili twende mbele. Ndiyo maana inauzi sana unavyoona mbunge wa tanzania anadai kwamba na yeye lazima asafiri first class kwa sababu wabunge wa marekani wanasafiri first class (kwanza sidhani kama wabunge wa marekani wanasafiri first class) lakini ukweli ni aibu mtu kutaka kupewa benefit sawa na nchi zingine wakati hakuna chochote kinacholingana na nchi hizi. Wachina sasa hivi wanakwenda mbele kwa sababu hawakufocus kwenye benefit wakati wanaruhusu investors wawekeze. Walifocus kwamba watu watapata kazi na watakuwa na kipato na baadaye uchumi ukiwa mkubwa ndipo benefit zinapokuja. Hivyo hivyo hata ukiangalia Japan miaka ya 50 na south korea miaka ya 90. Nchi hizi zote sasa zipo mbele na wananchi wake sasa wanapata benefit zote tofauti na miaka wakati uchumi wa nchi hizi unaanza. Sisi watanzania hatuna hicho tunataka vyote kwa pamoja.

Kiongozi ambaye alikuwa na vision nzuri ya Tanzania ni mkapa. Pamoja na mapungufu alikuwa nayo mkapa lakini kweli lazima umpe pongezi kwa kuwa focused kwa long term development ya uchumi wa Tanzania. Mkapa anastahili pongezi kwa kuuza NBC na mashika yote ambaye yalikuwa kila mwaka yanapata hasara tuu. Leo hii ukienda NBC unafurahi unahudumiwa mapema, unaheshimiwa kama mteja na unathaminiwa. Zamani unakuta watu wamejaa counter lakini wanapiga tuu story na mteja wanakuangalia tuu. Ndiyo wafanyakazi walipunguzwa lakini ukweli NBC walikuwa wanatupa hasara kila mwaka.